MAAJABU YA AKIBA

Hivi ulishawahi kuona aina
hizi mbili za watu? 1.watu ambao wanaheshimika na kuthaminiwa sana katika
jamii. Yaani, hawa watu kwenye masuala muhimu yanayo hitaji ushauri, uamuzi, na
mchango wowote wenye tija ni lazima wahusishwe katika kufanya hivyo. Iwe katika
vikao na matukio mengine muhimu hapo utasikia wakisema kamwiteni fulani, mwandikieni
barua fulani au mpigieni simu fulani atasaidia sana katika hili.
2. Upande mwingine Kuna watu ambao
huwa wanapuuzwa sana na kuonekana hawana mchango wowote katika jamii, watu hawa ni ngumu sana kukuta wemeombwa hata
ushauri au kushirikishwa kwenye masuala muhimu katika jamii. Utasikia tu hamuna
chochote hapo, mtapoteza hela bure tu.Watu hawa wanapuuzwa na kuchukuliwa poa
sana pengine kutokana na matendo yao, manrno yao, tabia na mionekano yao katika jamii. Zipo
sababu nyingi zinazofanya mtu kupuuzwa na kuonekana wa kawaida sana, hizi tutaziangalia
wakati mwingine.
Lakini leo nataka tuangalie mambo ya yanayosababisha thamani ya mtu kupungua katika jamii anayoishi. Hapa chini
ni mambo yanayoshusha thamani yako katika jamii yako ambayo ni;
1.
KULALAMIKA
(LAMENTING).
Tabia hii ya kulalamika si nzuri hata kidogo, kuna watu ni wazuri wa kulalamika, huwa wanalalamika hata kama kitu ni kidogo sana kimemtokea atalalamika usiku na
mchana. Iwe ni tatizo limemkuta atalalamika kweli kweli. Watu wa aina hii wakikutana
na changamoto kidogo tu utasikia kwanini mimi linipate hili, kwanini Mungu
nilizaliwa Tanzania? Yaani, ni full kulalamika na unakuta mtu anamlalamikia hadi
Mungu hivi ni kweli jamani. Kwa lugha fupi mtu huyu anawaombea watu wengine
wapate mabaya. Ndugu yangu changamoto zitakuja tu hata kama uwe mwema au muovu
kiasi gani zitakuja kwako na kama hautakuwa tayari kuzikubali na kuzikabili
utapata tabu sana,lakini pia nikwambia changamoto inapokuja inatabia ya
kukufundisha na kukuimarisha, hivyo jitahidi kupata funzo kwa changamoto yako
ili uimarike kuliko kulalamika sana. Rafiki tabia hii ukiendekea nayo watu
watakudharau sana na thamani yako itashuka kabisa. Hapa badala ya kulalamika
uwe ni mtu wa leta suluhu katika changamoto zako na watu wenginebkuliko kulalamika
muda wote.
2.
KUOMBA
OMBA (DEMANDS).
Nakubali kwamba hakuna binadamu aliyekamilika hayupo. Ndiyo
maana katika dunia hii tunaishi kwa kutegemeana hivyo kutoa na kuomba ni swala
la kawaida kabisa. Lakini unapokuwa mtu wa kuomba omba kila wakati
na kwa kila mtu utashusha thamani yako mapema sana. Omba kwa utaratibu na
heshima tena kwa watu unao dhani kuwa watakusaidia na siyo kuonba kwa kila mtu. Ulisha wahi
kuona mtu kila ukikutana naye au kupiga simu au kuona sms yake anaonba yaani, unajua kabisa
kwamba hii simu siyo bure na kweli ukipokea utasikia boss nipe teni nimekwama hapa mkuu tena bila hata kuomba kama ni yake vile, au mwingine anakwambia boss
niazime 60000 kesho kutwa narudisha mapema sana, kesho kutwa yenyewe sasa ikifika. Rafiki
unapokuwa na uhitaji tafuta msaada lakini isiwe ndiyo tabia yako wakati
mwingine wasaidie na wengine usiwe ni mtu wa kuomba tu.Badala ya kuomba omba
uwe mtoaji mzuri pia.
3.
VISINGIZIO
(EXCUSES).
kunamsemo unasema mbaazi akikosa maua husingizia jua. Watu
hawa huwa wanasababu katika kila kufeli kwao na wanazifanya kuwa halali
kabisa, ukimwambia kwanini hujalima mwaka huu atakwambia mvua
haikunyesha, kwanini hukumaliza kazi atakwambia nilipata imejensi, kwanini hukuja
kwenye kikao atakwambia nilikuwa nafua na wakati huo mtu anafahamu kabisa kuwa
wakati fulani anatakiwa awepo kwa kikao au afanye kazi fulani lakini inakuwa
tatizo. Hii inatokana na uwezo mdogo wa kusema hapana. Rafiki badilika acha
visingizio kama mbaazi wakosavyo maua na kusingizia jua isiwe kwako asee piga
kazi achana na excuses na kama kitu
huna uwezo nacho wa kukifanya mwambie mtu ukweli kwa kusema hapana kwa heshima
kuliko kukubali ili kumridhisha kisha baadaye ukaleta visingizio vya kutosha
kumbe hata kitu hicho ulikuwa hukiwezi asee. Sasa badala ya kuwa na visingizio
viepuke kwa kuanza kufanya na kuendelea kufanya mpaka kieleweke.
4.
SIFA
NA MAJIVUNO.
Tabia hii pia si nzuri sana hasa kwa jamii inayo kuzunguka, lakini
imekuwa ni hulka ya watu wengi kupenda kujisifia au kusifiwa kwa maendeleo
yao, tabia zao, hatua wanazo zipiga. Ukweli ni kwamba hakuna mtu ambaye
hapendi kusifiwa hayupo sijaona kwakweli, lakini kuna watu wamezidi sana kutaka
sifa, utashangaa mtu kupiga hatua na kufanikiwa kidogo tu mtaa mzima watajua,
akipata pesa kidogo tu watu wote watajua, akiongea kingereza kidogo tu mtaani
watajua, yaani, ni full kutamba na kujivuna. Ajabu kubwa ni kwamba mtu huyo huyo
aliyekuwa anajivuna utashangaa jioni anakuomba pesa akamwagilie moyo. Ukimuuliza
imekuwaje tena, anakwambia ni lazima watu wajue kuwa unazo hata kama unapumulia
mpira. Nikaja gundua kumbe watu hawaishi uhalisia wa maisha yao badala yake
wanaishi ili kuwaridhisha watu wengine tu. Hii nayo ni hatari na itashusha thamani
yako.
Ndugu yangu kama kuna kitu kizuri umekifanya wacha watu
waseme wenyewe na mambo yatakaa vizuri tu. kuliko kuanza kujisifia mwenyewe kufanya
hivyo ni kupoteza muda kama walivyo sema wataalamu kuwa “Be a better person but don’t waste time to prove it”. Kuwa mtu bora
lakini usipoteze muda kuthibitisha asee.
5.
UONGO
NA KUKOSA UAMINIFU.
Kuna watu uongo wameufanya kuwa ni sehemu ya maisha
yao. Yaani, wanaongea ongea tu bila hata kufikiria, wanatoa ahadi ambazo si halisi
katika maisha yao na matokeo yake wanashindwa kuzitimiza na wanakuwa waomgo, hivyo kuvunja uaminifu. Ndugu uaminifu ni kutunza na kusimamia maneno yako. Kushindwa
kufanya hivyo unakuwa muongo na unakosa
uaminifu. Tambua kuwa “truth and loyalty
are the best policies” yaani ukweli na
uaminifu ni sera bora sana. Pia kuna msemo mmoja mzuri sana unasema “When
you don’t keep your words you lose credibility, when you lose
credibility, you break the bond of trust. And breaking the bond of trust
ultimately leads to a string of broken relationships” tafisiri yake ni kwamba ukishindwa kutunza
maneno yako unapoteza uaminifu wako na ukipoteza uaminifu una vunja uaminifu . Na kuvunja uaminifu hupelekea mahusiano kuvunjika.
kujua zaidi kuhusu ukweli na uaminifu bonyeza hapa
6.
KUWAPUUZA
NA KUTOKUWASIKILIZA WENGINE.
Hiki ni kitu kidogo sana ukikifanya lakini madhara yake ni
makubwa mno . Watu wengi wamekuwa wakiwapuuza na kutokuwasikiliza kabisa wengine, mara nyingi wamekuwa ni watu wa kutaka kujaliwa na kusikilizwa wao tu. Hiki kitu ni ngumu kutokea hata kikitokea ujue wanakunafikia tu ukiondoka watakusema
kweli kweli na kukuita majina yote yatakayokufaa. Kubwa kabisa hapa jifunze kuwajali watu wengine, jifunze kusikiliza watu tena kwa makini, utapata faida mara mbili ya utakavyoongea. Sikiliza na kuwajali wengine hasa wanapohitaji msaada wako, ukitaka
kusikilizwa wasikilize kwanza watu wengine, ukitaka kuheshimiwa waheshimu kwanza
watu wengine, ukitaka kuthaminiwa wathamini kwanza watu wengine. Kwani, “what goes around comes around”.
Rafiki! ni matumaini yangu kuwa umejifunza kitu.
Na kama unachangamoto katika hili pengine namna gani ya
kuondokana na adha hii wasiliana na mimi moja kwa moja kupitia mawasiliano hapo
chini naamini utasaidika.
GeT tO ThE nExT lEvEl!
Makala hii
imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO ELIAS Mshauri & Mwalimu Wa
Saikolojia, Uchumi na Maisha. Mwanzilishi na Mwendeshaji wa mtandao wa addvaluetz karibu sana ujiongezee thamani yako.
Kwa mawasiliano;
Whatsapp &
Sim >>+255767653697 /+255783327456
Email>>
eliasmigongo120@gmail.com.
Facebook>>
MIGONGO ELIAS.
LinkedIn>>Migongoe.
Pinterest>>eliasmigongo.
Kama
umejifunza kitu,niachie maoni yako nitafurahi kujifunza pamoja nawe.
Sort by: Date Rating Last Activity
Comments by IntenseDebate
Posting anonymously.
Migongo 9p · 104 weeks ago
Marco · 104 weeks ago
Migongo 9p · 104 weeks ago
Scholastica Ernest · 104 weeks ago
Migongo 9p · 104 weeks ago
Jacob · 103 weeks ago
Migongo · 103 weeks ago
Julian Alistides · 99 weeks ago
Migongo · 99 weeks ago
Aishkel · 54 weeks ago
Elias Migongo · 54 weeks ago
Joga heke · 54 weeks ago
Elias Migongo · 54 weeks ago
NESTA · 54 weeks ago
Migongo Elias · 54 weeks ago
Chy · 54 weeks ago
Migongo Elias · 54 weeks ago
Christina · 51 weeks ago
Migongo · 50 weeks ago