Posts

Showing posts from June, 2023

MAAJABU YA AKIBA

Image
MAAJABU YA AKIBA Akiba (saving) ni kiasi cha fedha au rasilimali ambacho kimewekwa kwa matumizi ya baadaye, hata sasa kingeweza kutumika lakini umuhimu wake kwa kutumika baadaye ni mkubwa kuliko matumizi yake ya sasa. Hata katika biblia ``Mwanzo 41:35-36`` kama umewahi soma utaona Farao baada ya kutafsiriwa ndoto yake na kufahamu kuwa, imempasa kuweka akiba alilifanya hilo kwa uharaka ili kuhakikisha linaendelea vizuri ndio akamweka Yusufu kama msimamizi wa hili. Farao aliona kabisa kuwa nidhamu yake ya kujiwekea akiba haipo sawa hivo alihitaji msaidizi wa kumsaidia kama yeye alivyokuwa ndivyo tulivyo baadhi yetu siku za leo hatuwezi kujiwekea akiba ya vile tulivyo navyo. yaani huwa tunapenda kusema kesho itajisumbukia yenyewe,  Hata hivyo tangu zamani hata leo mataifa mbalimbali yamekuwa yakijiwekea akiba kwa manufaa na matumizi ya baadaye. Ukiangalia nabii Samweli alikuwa akijiwekea akiba na aliitoa pale Sauli alipomtembelea wakaila ile akiba ya chakula. Ni muhimu kujiw...

SIMULIZI YA KUSISIMUA KUHUSU “HATIMA YA KIMUNGU”. >>SEHEMU YA TATU.

Image
  SIMULIZI YA KUSISIMUA KUHUSU “HATIMA YA KIMUNGU”. >>SEHEMU YA TATU.   Ilipoishia....,.. Editrin baada ya kutulia alimsimulia kisa kizima mama yake tangu alipotoroka kwao, hadi kufikia hapa alipo na namna amba v yo El vine alivyopotea. Eliana alionesha kuumia sana kwani kwa namna nyingine tunaweza kusema yeye ndi y e aliyekuwa bibi wa mtoto yule. Wakiwa wanaendelea na mazung u mzo y ale Editrin akaanza kukumbuka kisa chote kilichomkuta kwenye maisha yake hata kupelekea yeye kutoroka kwao Dar es salaam na kuamua kuja kuishi Iringa.......   Kama hujasoma sehemu ya kwanza na ya pili bonyeza hapa. Sasa inaendelea...,.... Editrin alizaliwa Katika familia ya kitajiri sana. Baba yake alikuwa akiitwa Mr. Edward na mama yake aliitwa Eliana . Katika familia yao walizaliwa watoto wawili tu! ambao ni Editrin na Edger. T angu utoto wao walipendwa sana na wazazi wao wote wawili. Editrin na k aka yake Edger hawakuwahi kuyajua maisha ya shida ma an a baba yako ali...

JIFUNZE KUJIFUNZA (PART 1)

Image
JIFUNZE KUJIFUNZA (PART 1) Siku moja nikawa nimetulia natafakari   nikawaza na kuwazua kuhusu binadamu. Nikaona kuwa ni kawaida kabisa kwa binadamu yeyote kuzaliwa, kulelewa, kwenda shule au kutokwenda kabisa, kuoa/kuolewa wakati mwingine kutokuoa/kuolewa kabisa, kufanya kazi, kuzeeka na hata kufa. Lakini unaweza kufa hata kabla ya wakati wa kuzeeka kwako. Nikagundua kuwa katikati ya utoto na uzee/ kifo. Mwanadamu huyu atajikuta amefahamu vitu vingi sana. Aidha kwa kujifunza mwenyewe kwa kuona kusikia au kwa njia yeyote ile, au kwa kufundishwa na watu wengine nyumbani au kwa kwenda shule. Kwa kifupi   tumejifunza au tumefundishwa mambo kemkemu. Ukienda shule za St. Kayumba utafundishwa habari ya 3K   yaani, kusoma, kuandika, na kuhesabu. Na, ukibahatika ukapanda magari ya njano utafundishwa kuhusu, 3R s yaani, Reading, wRiting, and aRithmetic. Hata kwa wale hawakukanyaga kabisa umande wa asubuhi nao wamejikuta wamejifunza vitu vingi sana huko nyumbani na mtaani pia. ...

Popular posts from this blog

NJIA 7 ZA KUOSHA UBONGO WAKO.

VITU 9 MUHIMU KWA MTU YEYOTE KUJIFUNZA KWENYE MAHAFALI.

SIRI ILIYOPO NYUMA YA TABASAMU.