Posts

Showing posts from September, 2023

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29

Image
  Nashukuru kwa kushiriki nami link ya Hadithi hii tamu na Nzuri ya Hatima ya Kimungu Sehemu ya 29. 🙏 Nilichosoma katika sehemu hii, simulizi imeendelea  kwa mvuto mkubwa sana – linaonyesha mapambano ya ndani ya Elvine kati ya imani yake, hofu yakuwaza kumpoteza mkewe Elimina, na hatia ya makosa ya zamani. Kuna mambo yafuatayo nimeona  yaliyobeba msingi   wa  sehemu hii: 1. Mgongano wa nafsi ya Elvine 👉Anapokuwa mbele ya Malaika Elvila, anatakiwa kufanya maamuzi magumu: kati ya mke na mtoto. 👉Uamuzi wake unaonyesha upungufu wa mwanadamu, uchungu, na jinsi maumivu yanavyoweza kuathiri fikra na maamuzi. 2. Adhabu na Neema 👉Kupotea kwa mtoto na kutozaa tena kwa Elimina ni matokeo ya makosa ya Elvine, lakini bado neema ya Mungu inaonekana kwa kumrejesha mkewe. 👉Malaika anamkumbusha kuwa Mungu si mkatili, bali anamfundisha kupitia mateso na changamoto. 3. Ugeuzi wa Maisha (Turning Point) 👉Elvine sasa anaitwa kuwa mchungaji wa kondoo wa Bwana, ishara ...

SIMULIZI YA KUFURAHISHA, “KUHUSU HATIMA YA KIMUNGU”. SEHEMU YA KUMI NA TANO.

Image
SIMULIZI YA KUFURAHISHA, “KUHUSU HATIMA YA KIMUNGU”.   SEHEMU YA KUMI NA TANO.  Ilipoishia... Usisogee maana hapo unaposogea ndipo nataka kudondokea kwahiyo pishaaa!!" Kabla hajayatafakari yale maneno yule mtu alijiachia makusudi kabisa na kujitupa chini. Elvine alishangaa zaidi. Alitaka kusogea ili akatoe msaada lakini yule mtu ghafla alipotea.         Elvine alipata hofu zaidi. Akakimbia mpaka chumbani kwake na akajihisi kabisa hadi ile kiu imekata. Lakini alipofika chumbani kwake alipigwa na butwaa kwa kile alichokuwa anakiona mbele yake na wala hakuamini kwa haraka.... Kusoma sehemu ya 14 bonyeza hapa Inaendelea...     Alipotazama kitandani kwake alimuona kijana yule aliyekuwa kaanguka mchana na ndiye aliyemuona kajiangusha muda sio mrefu kutoka kwenye ngazi tena akiwa anacheka sana.       "Kumbe ni wewe? Unajua nilikuwa najiuliza sana kuwa ni kijana yupi ambaye anakaa hapa na anauwezo wa kufanya mambo makubwa. Kwakwel...

SIMULIZI YA KUFURAHISHA, “KUHUSU HATIMA YA KIMUNGU”. SEHEMU YA KUMI NA TATU.

Image
  SIMULIZI YA KUFURAHISHA,   “KUHUSU HATIMA YA KIMUNGU”. SEHEMU YA KUMI NA TATU.     Ilipoishia..   Aligundua kuwa kumbe Elimina anamachungu sana moyoni mwake. Aliacha kumfokea na kuanza kumwomba msamaha huku akitamani kujua tatizo ni nini hasa. Wakati akiwa anambembeleza alikaa pembeni ya Elimina kwenye sofa huku akisema samahani. Ghafla mama aliingia na kushangaa kwa kile alichokiona "Nyie watoto ni upuuzi gani mnafanya hapo?....." kusoma sehemu ya kumi na mbili bofya hapa   Sasa inaendelea....   Elvine hawakujua wamjibi nini maana walijua kabisa mama atakuwa kaelewa kwa tofauti sana.     "Samahani mama sio kama unavyofikiria. Ni kwamba Elimina hajisikii vizuri. Na alikuwa akilia na mimi sijui shida ni nini na ndio maana nilitaka aniambie" Elvine alijaribu kujitetea       "Jiandaeni kwaajili ya kikao cha familia akija baba yenu" mama aliongea kwa mkato kisha akaondoka na kuelekea chumbani. ...

Popular posts from this blog

MAAJABU YA AKIBA

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29