Posts

Showing posts from March, 2024

MAAJABU YA AKIBA

Image
MAAJABU YA AKIBA Akiba (saving) ni kiasi cha fedha au rasilimali ambacho kimewekwa kwa matumizi ya baadaye, hata sasa kingeweza kutumika lakini umuhimu wake kwa kutumika baadaye ni mkubwa kuliko matumizi yake ya sasa. Hata katika biblia ``Mwanzo 41:35-36`` kama umewahi soma utaona Farao baada ya kutafsiriwa ndoto yake na kufahamu kuwa, imempasa kuweka akiba alilifanya hilo kwa uharaka ili kuhakikisha linaendelea vizuri ndio akamweka Yusufu kama msimamizi wa hili. Farao aliona kabisa kuwa nidhamu yake ya kujiwekea akiba haipo sawa hivo alihitaji msaidizi wa kumsaidia kama yeye alivyokuwa ndivyo tulivyo baadhi yetu siku za leo hatuwezi kujiwekea akiba ya vile tulivyo navyo. yaani huwa tunapenda kusema kesho itajisumbukia yenyewe,  Hata hivyo tangu zamani hata leo mataifa mbalimbali yamekuwa yakijiwekea akiba kwa manufaa na matumizi ya baadaye. Ukiangalia nabii Samweli alikuwa akijiwekea akiba na aliitoa pale Sauli alipomtembelea wakaila ile akiba ya chakula. Ni muhimu kujiw...

SIMULIZI YA KUFURAHISHA, “KUHUSU HATIMA YA KIMUNGU”. SEHEMU YA 17.

Image
HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA KUMI NA SABA Ilipoishia.... Siku moja akiwa amelala aliota moto mkubwa unawaka ndani ya maji lakini ule moto ni kama unaofifia kwa kuzidiwa na yale maji. Alipoamka akaikumbuka ndoto aliyowahi kuota utotoni ikamkumbusha kuwa hatakiwi kuzima namna hiyo na akajikuta kakumbuka sana vile viusumbufu vya kivita na maadui. Lakini hakujua kumbe kuna bomu kubwa kaandaliwa.....  Kusoma sehemu ya 16 bonyeza hapa. *.   *.    *.   *.    *.    *.   *.  Elvine alikuwa ameketi juu ya mti katikati ya poli fulani akiwa na amani sana. Akiwa pale aliweza kuona umbali mrefu sana. Alishangaa baada ya kumuona mtoto wa kiume mwenye umri kama wa miaka 7 hivi anazunguka zunguka mule polini. Akacheka sana halafu akasema "Kuna vitoto vya ajabu Duniani jamani. Sasa angalia huyu mtoto anataka nini huku polini muda huu?" Akatabasamu akachuma embe lililoiva kwenye ule mti na kuanza kulila. Yule  mtoto alikuwa akijiimb...

SIMULIZI YA KUFURAHISHA, “KUHUSU HATIMA YA KIMUNGU”. SEHEMU YA 16.

Image
  SIMULIZI YA KUFURAHISHA, “KUHUSU HATIMA YA KIMUNGU”.   SEHEMU YA 16.  Ilipoishia.....      Sherehe zilianza na watu wengi sana walikuja tena wachungaji walikuwa wengi sana. Elvine alifurahi baada ya kumuona baba yake na mama yake wamekuja tena wakiwa wazima wa afya. Elvine pamoja na kufurahi lakini bado alikuwa na wasiwasi  k usoma sehemu iliyopita bonyeza hapa. Sasa inaendelea.... Alitazama Elimina namna alivyopenda akasema kimoyomoyo 'hakika malkia wangu usife mapema bado natamani kuona ulipendeza hivihivi daima'. Wakaingia kanisani ambapo aliyesimamia ibada ya send-off alikuwa ni mchungaji wa kanisa jilani. Lakini Elvine alikuwa na wasiwasi sana na yule mchungaji maana tangu alipofika alikuwa hawatazami watu usoni bali mda mwingi alitazama chini kama anayetunza sheria za familia.  Elvine hakutaka kujaji saana lakini kuna namna alimkazia macho sana yule mchungaji maana kwa mauzauza tu yanayomuwinda aliona ni lazima amchunguze kila mtu ana...

Popular posts from this blog

NJIA 7 ZA KUOSHA UBONGO WAKO.

VITU 9 MUHIMU KWA MTU YEYOTE KUJIFUNZA KWENYE MAHAFALI.

SIRI ILIYOPO NYUMA YA TABASAMU.