Posts

Showing posts from September, 2025

LEVEL ZA MAFANIKIO SEHEMU YA KWANZA.

Image
  LEVEL ZA MAFANIKIO SEHEMU YA KWANZA. Watu wengi wana ndoto za mafanikio. Wanatamani maisha bora, uhuru wa kifedha, na heshima katika jamii. Lakini kuna ukweli mmoja ambao wengi hawautaki kuukubali: Mafanikio siyo ajali wala tukio la siku moja, hii ni SAFARI boss. Ni safari: yenye milima na mabonde yenye maumivu na changamoto yenye hatua (levels) zinazopaswa kupitiwa moja baada ya nyingine kama ilivyo katika ngazi boss. Huwezi kuruka ngazi hatua ya kwanza na kufika hatua ya juu moja kwa moja. 👉 yaani, ni unapanda hatua kwa hatua. Na uzuri ni kwamba, kila mtu duniani, yupo kwenye hatua fulani sasa hivi. Na leo nataka tuzamie kwenye hatua ya kwanza kabisa. HATUA YA KWANZA NI HATUA YA  UTUMWA (SLAVERY LEVEL). Hii ndiyo hatua ya mwanzo kabisa ya safari ya mafanikio. Ni hatua ambayo mtu: anauza muda wake, anauza nguvu zake. Anauza ujuzi wake, anauza uwepo wake. 👉 Ili tu aweze kuishi. Hii ndiyo hatua ya “SURVIVAL” Kwa lugha fupi hii level ni survival level. Uha...

HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 31

Image
  HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 31 Ilipoishia………. Elvine alipoteza amani kuliko hata mkewe maana kila alipomtazama mkewe basi moyo wake ni kama ulikuwa unachomwa na mwiba uliojishikiza huko kwenye mishipa ya moyo. Nafsi yake ilitaabika na ndipo alipoamua kutafuta muda mzuri, baada ya chakula cha jioni, azungumze na mkewe, maana ule ukimya wa siku mbili ulikuwa adhabu kubwa sana kwake. Kusoma sehemu ya 30 bonyeza hapa Sasa inaendelea………. Elimina mamy naomba kujua kwanini hutaki kuniuliza kuhusu sababu ya haya yote? Maana najua unajua kuwa kuna mahali mimi nilikosea, sasa unapokaa kimya hivyo… kiukweli unazidi kunichanganya maana ni kama hutaki kujua, sasa unadhani mimi roho yangu itatulia kweli?. Hata kama ungekuwa wewe lazima usingepata amani, ungekuwa hata unawaza hivi nakuwaziaje, nakuonaje na ninajisikiaje ninapokuona, sasa kwanini wewe umekaa kimya, sema neno tafadhali? (Elvine alikuwa akiongea bila kumtazama mkewe usoni maana moyo wake haukuwa katika hali ya utulivu). Pamoja na ...

Popular posts from this blog

UKIJUA HILI KUHUSU WATU UTAFANIKIWA SANA.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.