KAMA UNASAHAU MARA KWA MARA, SOMA HAPA KWANZA.

Image
  KAMA UNASAHAU MARA KWA MARA, SOMA HAPA KWANZA. Boss! Siyo  kila mara, kusahau ni ishara ya Ubongo dhaifu, mara nyingi ni namna tunavyojifunza ndugu. Nimekutana na watu wengi wakisema: "Mimi sina akili kubwa." Wengine "Kumbukumbu yangu ni mbaya." Mara "Ubongo wangu hauhifadhi vitu." Lakini ukweli ni kwamba, mara nyingi tatizo si ukubwa wa akili yako wala uwezo wa ubongo wako. Tatizo ni kwamba watu wengi hawajawahi kufundishwa jinsi kumbukumbu (memory) inavyofanya kazi boss. Sikia ndugu; Ubongo wa binadamu umeumbwa kwa ustadi mkubwa. Kazi yake si kuhifadhi kila kitu unachokiona au kukisikia, bali ni kuchagua filtering taarifa muhimu na kuacha zisizo muhimu wala matumizi. Kwa hiyo, kusahau si kasoro ya ubongo ni sehemu ya kawaida ya jinsi unavyofanya kazi. Hebu tuangalie sababu kuu zinazowafanya watu kusahau mara kwa mara. 1. Kukariri Bila Kuelewa (memorising without understanding). Hili ndilo kosa kubwa zaidi ambalo wanafunzi na hata watu wazima...

LEVEL ZA MAFANIKIO SEHEMU YA KWANZA.

 


LEVEL ZA MAFANIKIO SEHEMU YA KWANZA.

Watu wengi wana ndoto za mafanikio.
Wanatamani maisha bora, uhuru wa kifedha, na heshima katika jamii.
Lakini kuna ukweli mmoja ambao wengi hawautaki kuukubali:
Mafanikio siyo ajali wala tukio la siku moja, hii ni SAFARI boss.

Ni safari: yenye milima na mabonde
yenye maumivu na changamoto
yenye hatua (levels) zinazopaswa kupitiwa moja baada ya nyingine kama ilivyo katika ngazi boss.
Huwezi kuruka ngazi hatua ya kwanza na kufika hatua ya juu moja kwa moja.

πŸ‘‰ yaani, ni unapanda hatua kwa hatua.
Na uzuri ni kwamba, kila mtu duniani, yupo kwenye hatua fulani sasa hivi.
Na leo nataka tuzamie kwenye hatua ya kwanza kabisa.

HATUA YA KWANZA NI HATUA YA  UTUMWA (SLAVERY LEVEL).

Hii ndiyo hatua ya mwanzo kabisa ya safari ya mafanikio.
Ni hatua ambayo mtu:
anauza muda wake, anauza nguvu zake.
Anauza ujuzi wake, anauza uwepo wake.
πŸ‘‰ Ili tu aweze kuishi.
Hii ndiyo hatua ya “SURVIVAL” Kwa lugha fupi hii level ni survival level.

Uhalisia wake ni kwamba,
Katika hatua hii, maisha yanazunguka mahitaji ya msingi: Mfano Chakula, Kodi ya nyumba,
Bills za maisha, Mavazi, Gharama za kila siku.
Hapa ni, Unafanya kazi ili uishi.
... Ukisimama kufanya kazi,  maisha yanasimama pia.
Hii ndiyo ile hali ya kusema:
“Leo nikipata,  ndiyo nakula.”

MFUMO WA HII LEVEL UKO HIVI,
πŸ‘‰ Usipotoka kufanya kazi → hupati kitu
πŸ‘‰ Usipojituma → hakuna matokeo
πŸ‘‰ Usipovuja jasho → hakuna chakula
Mkono hauendi kinywani bila jasho boss wangu.

Kwasababu ya mikikimikiki ya level hapa ndipo watu wengi wanapopitia:
Msongo wa mawazo, hofu ya kesho, kukosa uhakika wa maisha na
Kuishi siku kwa siku.
πŸ‘‰ Mtu anahangaika leo…
lakini hajui kesho itakuwaje.

KOSA KUBWA AMBALO WENGI HUFANYA
Watu wengi wakiwa bado wapo hatua hii:
πŸ‘‰ Wanataka kuishi maisha ya level za juu
πŸ‘‰ Wanataka mafanikio ya haraka
πŸ‘‰ Wanatafuta shortcuts za maisha
Lakini ukweli ni huu:
Ndugu, huwezi kujenga juu bila msingi imara.
Halafu boss, uzuri ni kwamba,
Hii siyo sehemu ya kudumu.
Ni hatua ya mpito.
Ni kipindi cha: kujifunza,
kujijenga katika misingi,
kuimarisha uwezo wako.
kuweka msingi wa maisha yako.

NAMNA YA KUSHINDA HAPA
Badala ya kulalamika, fanya haya:
1. JIFUNZE KUPITIA HALI ULIPO
Usione kama umekwama ona kama unajengwa. Hapa boss naaanisha usikate tamaa.
2. JENGA UJUZI
Hii ndiyo silaha itakayokutoa hapa.
3. VUMILIA MCHAKATO
Usikate tamaa mapema.
4. WEKA MSINGI IMARA
Unachofanya sasa kitaamua kesho yako.

Tatizo kubwa katika level hii,
Watu wengi hapa:
πŸ‘‰ Hukata tamaa mapema,
πŸ‘‰ Hupoteza imani,
πŸ‘‰ Huacha ndoto zao kabisa,
Na hapo ndipo wanapobaki hapa maisha yao.
yote.

Kama ningepata nafasi ya kukushauri,
Ndugu yangu.
Kama upo hapa:
usione aibu, usijidharau, usijilinganishe na wengine,
usijione umechelewa.
πŸ‘‰ Hii ndiyo sehemu ambayo wengi huanzia.
Lakini tofauti ni hii:
Wengine hukaa hapa milele, wakikata tamaa, kulalama na kulaumu, lakini,  wengine hupita na kupanda juu.
Na kwa wewe uliye vuka hatua hii hongera jipange kwa hatua inayofuata. Lakini pia tungependa utuambie ni kivipi umetokaje katika hatua hii ya SURVIVAL MODE.

Kuhitimisha,
Ndugu usichukie hatua hii.
Usikimbie mchakato huu.
πŸ‘‰ Jifunze. Vumilia. Jenga msingi na uwezo.
Kwa sababu:
Msingi wako ukikomaa,  mafanikio yako yatakuwa imara na utakuwa na uwezo wa kuyahimili na kuyabeba.

KUMBUKA HILI DAIMA
“Usikimbilie juu wakati bado hujajenga chini.”


Share na na mimi kupitia comment. Ikiwezekana share na wengine ujumbe huu ili wajifunze pia.

Kujifunza tembelea,
https://addvaluetz.blogspot.com/2026/04/misingi-ya-uwekezaji-part-two.html

#SelfAwareness (#Kujitambua). #Investment (#Uwekezaji). #PersonalDevelopment (#Maendeleobinafsi). #MigongoElias. #AddValueNetwork. #SeeYouNextLevel
+255767653697.


Popular posts from this blog

UKIJUA HILI KUHUSU WATU UTAFANIKIWA SANA.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29