SIRI MUHIMU WANAYOITUMIA WATU WANAOSHINE.
SIRI MUHUMU WANAYOITUMIA WATU WANAOSHINE. Watu wengi wanapenda mafanikio, lakini ukweli ni kwamba wachache sana wanafika juu kwenye hayo mafanikio. Kila mtu anatamani: kuwa bora kwenye kazi yake, kung’ara kwenye kipaji chake, kutambulika kwenye kile anachofanya na mengine kibao. Lakini ukiangalia katika uhalisia bila kupepesa, ๐ Wengi hubaki kuwa watu wa kawaida (average persons). SWALI MUHIMU LA KUJIULIZA: Kwa nini watu wengi hubaki wa kawaida, badala ya KUSHINE? Hapo kuna sababu nyingi unaweza kutoa. Lakini leo nataka nikupe KIINI halisi ambacho wengi wanakipuuza: KUKOSA MWENDELEZO (CONSISTENCY) HAPA NDIPO WENGI WANAPOANGUKIA. Unakuta mtu: Leo anaanza kitu kwa nguvu Kesho anabadilisha mwelekeo, Baada ya muda anaanza kitu kingine kabisa. ๐ Hapo hakuna kitu kinakomaa. ๐ Walakuna kitu kinatoa matokeo. Kila analoamza anaishia njiani. MWENDELEZO(Consistency) NI NINI HASA? Mwendelezo siyo kufanya kitu kwa siku mbili au wiki moja au mwaka mmoja boss. ๐ Mwendel...