SIRI MUHIMU WANAYOITUMIA WATU WANAOSHINE.


 SIRI MUHUMU WANAYOITUMIA WATU WANAOSHINE.

Watu wengi wanapenda mafanikio, lakini ukweli ni kwamba wachache sana wanafika juu kwenye hayo mafanikio.

Kila mtu anatamani: kuwa bora kwenye kazi yake,
kung’ara kwenye kipaji chake, kutambulika kwenye kile anachofanya na mengine kibao.
Lakini ukiangalia katika uhalisia bila kupepesa,
πŸ‘‰ Wengi hubaki kuwa watu wa kawaida (average persons).

SWALI MUHIMU LA KUJIULIZA:
Kwa nini watu wengi hubaki wa kawaida, badala ya KUSHINE?
Hapo kuna sababu nyingi unaweza kutoa.
Lakini leo nataka nikupe KIINI halisi ambacho wengi wanakipuuza:
KUKOSA MWENDELEZO (CONSISTENCY)
HAPA NDIPO WENGI WANAPOANGUKIA.

Unakuta mtu: Leo anaanza kitu kwa nguvu
Kesho anabadilisha mwelekeo,
Baada ya muda anaanza kitu kingine kabisa.
πŸ‘‰ Hapo hakuna kitu kinakomaa.
πŸ‘‰ Walakuna kitu kinatoa matokeo.
Kila analoamza anaishia njiani.

MWENDELEZO(Consistency) NI NINI HASA?
Mwendelezo siyo kufanya kitu kwa siku mbili au wiki moja au mwaka mmoja boss.
πŸ‘‰ Mwendelezo ni: Kukomaa na kitu kimoja hadi kilete matokeo. Yaani, hauachi hadi mambo yaeleweke.
Hapo ni sawa na kusema:
Hata nikishindwa → nitaanza tena,
Hatanikikosea → nitarekebisha tena,
Hata nikichoka → nitaendelea.
Hapa hakuna kuacha kabisa.

Nakumbuka mentor wangu kuna kanuni muhimu aliwahi kunifundisha hii mimi ninaiita ni
KANUNI YA MAFANIKIO: (SCF).
START – CONTINUE – FINISH
Hii ni sheria ambayo ukiifuata, maisha yako hayawezi kubaki kama yalivyo. Hebu tuaicheck kidogo.

1. START (ANZA).
Usikae na ndoto kichwani tu boss wangu. Acha kuwazawaza na kufikiri sana hilo lindoto.
Anza kufanya hata kama hujawa tayari 100%. Mambo mengine yatajipanga mbele ya safari.

2. CONTINUE (ENDELEA)
Hapa ndipo watu wengi wanaanguka.
Wanakata tamaa mapema,
Wanachoka kufanya
Wanapoteza mwelekeo na mwendelezo. Hawa ndio wale watu wengi wanaoshindwa na kubaki wa kawaida sana.
πŸ‘‰ Lakini washindi wanaendelea kupambana na kusonga mbele.

3. FINISH (MALIZA)
Hii ndiyo hatua inayotenganisha watu wa kawaida na watu wakubwa.
πŸ‘‰ Watu wengi wanaanza kufanya vizuri kabisa, lakini ni wachache wanamaliza.
Hapa na sema finish what you started.
Kama utagundua kuwa kitu hiki ni kizuri na kina manufaa kwangu anza kufanya, endelea kufanya kisha kimalize, nasema malizana nalo boss hakuna kuishia njia. Never.

LAKINI SIO KILA KITU UENDELEE NACHO
Kuna vitu: havikujengi, havina faida kwako,
vinakupotezea muda.
Hapa ndipo mentor aliniambia kutumia kanuni ya pili:
SQO — START, QUIT, OMIT
πŸ‘‰ Ukigundua kitu ulichoanza au unachotaka kukianza hakina thamani: ACHA mara moja
KIONDOE kabisa kwenye maisha yako.
Usiwe busy na vitu visivyokupeleka popote.

UKWELI MCHUNGU UNAOHITAJI KUSIKIA
Unaweza kuwa na: ndoto kubwa,
mipango mikubwa,
kipaji kikubwa.
Lakini kama huna mwendelezo CONSISTENCY.
πŸ‘‰ Hutafika Mbali boss.

JEBU ANGALIA MAISHA YAKO KWA UAMINIFU MKUBWA,
Ni mara ngapi: umeanza kitu ukaachia njiani?
umebadilisha direction katikati mwendo?
umekata tamaa mabema kabla ya matokeo?
πŸ‘‰ Hapo ndipo unapopoteza ushindi wako boss wangu.
Goja nikwambie
WATU UNAOWAONA WAKO JUU  KATIKA ENEO LOLOTE WALIFANYA NINI TOFAUTI?
Hivi unajua hawakuwa: na akili za ajabu sana
wala bahati ya kipekee.
πŸ‘‰ Walikuwa na kitu kimoja makini:
MWENDELEZO USIOYUMBA
Walikaa kwenye njia yao:
kipindi kigumu hawakuteteleka,
kipindi cha maumivu walivumilia,
kipindi cha kutokupata matokeo walijipa moyo.
πŸ‘‰ Hawakuwahikuacha. Hatimae na mwisho,  ikawalipa matokeo.

HII NI NGUVU YA MWENDELEZO.
Ukifanya kitu kwa mwendelezo:
Unajenga brand yako,
Watu wanakujua kwa hicho ukipendacho na ukifanyacho,
Una-jenga trust boss. Na kubwa kuliko
Unaongeza thamani yako boss.
πŸ‘‰ Na hatima yake: matokeo yanakuja yenyewe tena katika muda mwafaka.

Ndugu yangu, watu wengi walio fanikiwa na kupiga hatua katika maeneo yao wamewekeza nguvu zao, juhudi zao, pesa na akili zao angalau kuanzia miaka 5-10  ndipo wakawa manguli katika maeneo yao. Wengine katika ualimu wao, uchungaji wao, biashara, kazi, kibaji n.k.

Na hii haimaanishi na wewe lazima uchukue muda kama huo, lakini unaweza kuupuguza zaidi kadiri unavyoweka juhudi na nguvu kubwa.
Walikomaa na kujiambia,
“HAPA SITOKI WALA SIACHI NG'OO.
IJE MVUA, LIJE JUA, HADI KIELEWEKE NI LAZIMA NIFIKE MWISHO.”.

KWA KUHITIMISHA
Tatizo siyo kwamba huwezi.
Tatizo siyo kwamba huna uwezo.
πŸ‘‰ Tatizo ni: Umezoea kuachia njiani unakosa mwendelezo boss.
Hebu badilisha hiyo tabia leo.
ANZA. ENDELEA. MALIZA. Ikiwezekana ANZA. ACHA. ONDOA KABISA.
Na utakachokiona baada ya muda,  kitakushangaza hata wewe mwenyewe. Na watu wataanza kusema kuwa unabahati.

HEBU NIJIBU HII CHALLENGE KAMA UKOTAYARI KWA MABADILIKO.
Je ni eneo gani 1 au 2–3 tu unaamua kuanza nayo, iwe ni: Biashara, Kazi, Ujuzi, Kipaji, Huduma, n.k ambayo utawekeza muda, pesa, na  nguvu zako zote, na hautaHAMA hadi uone matokeo. IJE MVUA, LIJE JUA?.


Share na na mimi kupitia comment. Ikiwezekana share na wengine ujumbe huu ili wajifunze pia.

Kujifunza zaidi tembelea,
https://addvaluetz.blogspot.com

#SelfAwareness (#Kujitambua). #Investment (#Uwekezaji). #PersonalDevelopment (#Maendeleobinafsi). #MigongoElias. #AddValueNetwork. #SeeYouNextLevel
+255767653697.

Popular posts from this blog

UKIJUA HILI KUHUSU WATU UTAFANIKIWA SANA.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.