NGUVU YA TATHMINI KATIKA KUBORESHA MAISHA YAKO.

Image
  NGUVU YA TATHMINI KATIKA KUBORESHA MAISHA YAKO. Kuna jambo moja muhimu sana katika safari ya mafanikio ambalo watu wengi hulipuuzia, lakini lina uwezo mkubwa wa kubadilisha kabisa mwelekeo wa maisha ya mtu yeyote. Jambo hilo si lingine bali ni TATHMINI. Ndiyo tathmini boss. Boss in short tathmini ni uwezo wa kusimama kwa muda, kuangalia ulipotoka, ulipo sasa hivi, na kule unakoelekea. Yaani ni sawa na kujiuliza hivi; Je, njia ninayotumia inanifikisha ninapotaka kwenda? Nimefanikiwa kwa kiwango gani? Nimekosea wapi? Nini kimefanya mambo yasiende kama nilivyopanga? Nifanye nini tofauti ili kupata matokeo bora zaidi? Kwa sababu huwezi kuboresha kitu ambacho hukijui wala hujakipima boss. Ndugu, TATHMINI SI KUSHINDWA HII NI HEKIMA Watu wengi wakiona mipango yao haijafanikiwa haraka huamua kuiacha na kuibwaga ghafla tu. Kibaya zaidi wengine huanza kulaumu: mazingira, watu wengine, bahati, hali ya maisha au kujilaumu wao wenyewe. Lakini mtu mwenye hekima hufanya kitu cha to...

HUWEZI KUBADILIKA BILA KUJITAMBUA.


HUWEZI KUBADILIKA BILA KUJITAMBUA.

Watu wengi hutamani kubadilisha maisha ya tabia, kipato, mahusiano, au jinsi wanavyojiona. Wengine husoma vitabu, huhudhuria semina, na kuweka malengo mapya kila mwaka. Lakini, pamoja na juhudi zote hizo, hujikuta wakirudia hali ileile.

Sababu si kukosa bidii, no. Mara nyingi ni kukosa #KUJIJUA wao kama wao.

Kujiboresha bila kujitambua ni kama kujenga bila ramani.

Unapojaribu kubadilika bila kuelewa wewe ni nani, unaishia kuiga maisha ya wengine tu. Utaweka malengo yasiyoendana na hali yako, uwezo wako, au hali yako ya ndani.

Ndiyo maana baadhi ya malengo huonekana mazuri kwa macho ya watu, lakini moyoni hayana uzito wowote. Unapoanza kuchoka haraka, si uvivu tu, wakati mwingine ni ishara kwamba njia uliyopo siyo yako.

Kujitambua kunahitaji ujasiri wa kukubali ukweli kuhusu wewe.

#Kujitambua siyo kujipongeza kila wakati. Ni kukubali ukweli wote mtamu na mchungu.

Ni kuona #NGUVU zako bila kiburi, na #UDHAIFU wako bila kujilaumu. 

Ni kujiuliza maswali magumu kama: Mimi ni nani? Ninakwenda wapi? Kwa nini narudia makosa yaleyale? au Ni hofu gani inaniongoza bila kujua?

Huwezi kurekebisha kile ambacho hujakikubali.

Kujitambua huzaa mabadiliko ya kudumu

Unapojifahamu, maamuzi yako yanabadilika. Unaacha kuishi kwa mazoea na kuanza kuishi kwa #MAKUSUDI.

Unaacha kuhiuliza, “Watu watasemaje?” na kuanza kuuliza, “Hili linaendana na mimi?”

Mabadiliko yanayotokana na #SAUTI na #UELEWAwa ndani hudumu kwa sababu yanajengwa juu ya #UKWELI, si msukumo wa muda mfupi tu!.

Namaliza kwa kusema,

Kama kweli unataka kubadilika na kubadilisha chochote kwenye maisha yako, anza kwa kujifahamu wewe kwanza. Kaa kimya mara kwa mara tafakari, jisikilize kitokea ndani yako, na ukubali ukweli wako bila #KUHOFIA WALA #KUKIMBIA.


Kujitambua si mwisho wa #SAFARI—ni mwanzo wa #MABADILIKO ya #KWELI. Chukua muda mchache ujiulize swali hili:

Ni eneo gani la maisha yangu najidanganya

 mwenyewee na ninahitaji mabadiliko gani?


Add Value Network 

Migongo Elias 

#SeeYouNextLevel

Popular posts from this blog

UKIJUA HILI KUHUSU WATU UTAFANIKIWA SANA.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29