MAAJABU YA AKIBA

JIFUNZE KUJIFUNZA PART II
JINSI UBONGO WA MWANADAMU UNAVYOFANYA KAZI.
Kama hujasoma part I bonyeza hapa.
Kabla hatuja zamia mbali sana kwenye somo letu la jifunze
kujifunza, ni muhimu tuelewe kwanza ni kwa namna gani ubongo wa mwanadamu
unavyofanya kazi. Kwa kuwa ubongo ni sehemu muhimu sana na inahusika katika
kujifunza, ni muhimu tufahamu ni kwa jinsi gani unafanya
kazi. Kutokana na kamusi sanifu ya kiswahili ubongo ni ogani laini na
tepetevu yenye mishipa ya fahamu iliyopo ndani ya fuvu la kichwa yenye kazi ya
kudhibiti fikra, kumbukumbu, hisia na shughuli za mwili. Na hii ndiyo nyumba ya akili. Lakini akili ni uwezo
wa mtu wa kujua Kitu au jambo. Akili ni kitu muhimu sana kwa binadamu hasa katika mada
yetu ya jifunze kujifunza
Kama akili ya binadamu ingefananishwa na mashine ingekuwa
ni mfano wa mashine tata yaani, complex
machine na huu ni mfano tu, na uhalisia ni kwamba inazidi hapo. Ubongo kwakweli
unavitu vingi na vya ajabu mno! Na kama ningeambiwa kufananisha ubongo na mfumo
bado isingefaa.
Na kama mtu akijua namna ubongo wa mwanadamu unavyofanya
kazi, atafanikiwa sana kufikia malengo yake, kuwa mbunifu, ataweza kujifunza
kwa haraka, atabadili namna anavyojioona ataweza kuondosha tabia mbaya na kujenga
tabia nzuri ambazo mtu huyo anataka awenazo. Kiujumla mtu akifahamu namna mfumo
wake wa akili unavyofanya kazi ataweza kufanya makubwa sana na hata kuwa mfano wa kuigwa katika dunia hii. Kutenda miujiza ni swala la
kawaida sana, lakini siyo miujiza ya kutoa pepo hahahahahahaa!
Tafti zinaonyesha kuwa watu wote waliofanya mambo makubwana yaajabu duniani, wametumia chini ya asilimia 10% tu! Ya akili zao. Na hii, inamaanisha
kwamba watu wana uwezo mkubwa sana lakini bado hawajaufahamu na wala hawautumii
kabisa. Ndiyo maana charles aliwahi kusema “mind is like a ten speed bicycle; most
of us have gears we never use.” Kwa tafsiri yake ni sawa na kusema akili ni kama baiskeili yenye spidi kumi na na
miongoni mwetu tuna gia lakini hatujawahi kuzitumia kabisa.
Katika hili nimepokea malalamishi kutoka kwa watu wengi
sana wakidai kuwa hawana akili, wanauwezo
mdogo, wengine wakidai kuwa hawana vipaji, hawana uwezo wowote, hawana bahati
na vitu vingine kama hivyo. Naomba nikwambie kuwa, jambo hili ni uongo na siyo
kweli kabisa. Hakuna mtu ambaye hana akili dunia hii hayupo! Hakuna mtu ambaye
hana kipaji, ambaye hana akili, hawa wote hawapo. Watu wote tunaakili na uwezo
mkubwa, na wa kipekee ndani yetu, sema tu shida ni namna gani tunazitumia
akili zetu. Katika hili tuseme kuwa “if you’re intelligent you’re good at
using your mind in many different ways.” Yaani kama una akili unajua kutumia
vyema ubongo wako katika namna tofauti tofauti. Ukiona mtu anakuzidi akili, ujue
anakuzidi kuitumia tu! Akili, ukiona mtu anakipaji na uwezo mkubwa amekuzidi kutumia
akili tu! Changamka asee. Kama hivyo ndivyo, ni muhimu tukafahamu namna gani akili
zetu zinafanya kazi ili tuweze kujifunza kwa wepesi sana. Si unajua kujifunza
kujifunza wengi hawajafundishwa eeh!
Goja turudi kwenye akili kwanza ambayo wazungu wanaiita intelligence
(mind) ambapo napenda mtu mmoja amewahi kuielezea na kusema “intelligence is
what you use when you don’t know what you want to do.” Yaani, akili ni kile
unacho tumia pindi hujui nini unataka kufanya. Hii ni dhana pana sana, na hapa
nifupishe kwa kusema kwamba, akili ya binadamu imegawanyika katika makundi makuu
mawili ambayo ni, Conscious mind na Subconscious mind. Hapa ijulikane
kuwa inaweza kugawanywa kwa namna tofauti tofauti, lakini hapa goja tutumie
hizi mbili mana yake ndizo kuu. Na kwa leo tutaangalia kuhusu conscious mind
kwanza. Hata hivyo ifahamike kuwa tuna ubongo mmoja lakini umegawanyaka katika
sehemu kuu mbili katika utendaji kazi wake.
Conscious mind, hii
ni sehemu ya ubongo ambayo tupo na uelewa nayo . ni sehemu ya ubongo ambayo inashughulika na matendo yote ya hiali ambayo
mtu mtu anaweza kuyazuia au kuyaruhusu yafanyike, wakati mwingine wamombo
wanasema its a logical portion of our mind, na inauwezo wa kufikri kwa
mantiki(logically), kuchakata na kufanya maamuzi kupitia matukio. Mfano kujifunza
kupitia makosa, kuweka malengo. Kwa ujumla tunaweza kusema mambo na matukio
yote ambayo unaweza kufikri na kuamua kwa utashi wako mwenyewe mfano, unaweza
kuamua kutembea, kusoma kuoga, kukimbia, kupiga makofi, kunyosha mkono na
mengine kama hayo. Sehemu ya ubongo inayohusika na mawazo, na matendo ya hiali inaitwa
conscious mind. Sehemu hii hutusaidia kuyaweka pamoja mawazo na mipango
ili kuyatekeleza kama tulivyoamua(kupanga). Lakini pia, sehemu hii ni muhimu
sana katika kufanya maamuzi na kuchukua hatua.
Mapungufu(limitations) ya conscious mind
Pamoja na umuhimu wote huo, conscious mind bado haijajikamilisha
kwani, bado inamapungufu kadhaa katika utendaji kazi wake ambayo ni;
1.
Inaukomo wa kumbukumbu (limited
memory). Kuna namna akili zetu huwa zinasahau hata kwa vitu
ambavyo tunavifahamu au tulishawahi kuviona mfano; ulishawahi kumwona mtu anatafuta
shoka lipo begani? , Anatafuta funguo zipo mkononi?, Anasahau majina ya watu, au
alipo weka ile buku tano? Mifano ya matukio kama haya hutokea kwasababu
vilifanyika kwenye conscious mind ambayo inalimited memory.
2.
Inaweza kufanya kitu kimoja tu kwa
wakati mmoja. (It can do only a single task at a time).
Ukweli katika sehemu hii ya ubongo inahusika sana na kazi
moja tu kwa wakati mmoja. Yaani haiwezi kubeba kazi mbili kwa muda uleule na
kama mtu akijaribu kubeba mambo mawili kwa wakati mmoja itaachana na jambo lingine
na kushughulika na jambo moja tu ambalo mara nyingi linakuwa linafurahisha au jepesi. Mfano unaweza
ukawa unalima huku mtu anakupigisha stori, hapo akili itachagua kitu kimoja
mara nyingi huwa chepesi na kukomaa nacho ahapo yaweza kuwa ni kupiga stori, au
unaweza kuwa unasoma huku unachati, hapa lazima tu utatelekeza kimoja wapo. Na hapa
ndipo usemi wa mshika mawili moja humponyoka.Wakati mwingine conscious maana yake ni kwamba huwezi kufanya chochote nje ya
ufahamu wako. Mambo haya pia yamezungumzwa na mwanasaikolojia James Thomson.
Ndugu ninachotaka uelewe kwanza, namna akili yako ilivyo
na jinsi inavyofanya kazi hapo ndipo utajua namna gani ucheze nayo, uifanyishe
vipi mazoezi na hata kuiamuru jinsi wewe upendavyo. Harafu wakati mwingine
akili yako ni kama kompyuta ujue!, Ambayo hufanya kazi kulingana na utaalamu wa
mtumiaji. Kama unajua kutype tu basi kompyuta yako itakuwa na uwezo wa kutype
tu, kama unauwezo wa kuangalia muvi tu basi kompyuta yako itakuwa na uwezo wa
kuangalia muvi. Ndivyo ilivyo kwa akili yako inafanya mambo madogo au ya kawaida
kwasababu uwezo wako wa kuitumia umeisha hapo. Lakini ukweli ni kwamba, akili
yako ni kubwa sana kuliko unavyofikri inaweza kufanya mambo makubwa na yaajabu
sana. Tatizo litakuja palepale hujui namna gani ya kuitumia.
Rafiki masomo haya ni mfululizo ambayo yamelenga
kukufahamisha namna ya kujifunza kwa kutumia akili yako, kuifahamu akili yako
na hata kufanya makubwa pindi utakapojua
uwezo ulionao na hata kuitumia akili yako. Hivyo, usikose kufuatilia.
Rafiki, ni matumaini yangu kuwa umejifunza
kitu.
na kama unachangamoto katika hili pengine
namna gani ya kuondokana na adha hii sasa waweza kuwasiliana na mimi moja kwa
moja kupitia mawasiliano hapo chini naamini utasaidika.
GeT tO ThE nExT lEvEl!
Makala hii, imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO
ELIAS Mshauri & Mwalimu Wa Saikolojia, Uchumi na Maisha.
Mwanzilishi na Mwendeshaji wa Mtandao wa addvalue. Karibu sana
ujiongezee thamani yako.
Kwa mawasiliano;
Whatsapp & Sim >>+255767653697
/+255783327456
Email>> eliasmigongo120@gmail.com.
Facebook>> MIGONGO ELIAS.
LinkedIn>>Migongoe.
Pinterest>>eliasmigongo.
Kama umejifunza kitu, niachie maoni yako nitafurahi kujifunza pamoja nawe.