MAAJABU YA AKIBA

JIFUNZE KUJIFUNZA PART III.
JINSI AKILI YA BINADAMU INAVYOFANYA KAZI.
U hali gani ndugu msomaji! Mimi niko vyema na ninaendelea
vizuri kabisa. Kama utakuwa unafuatilia somo hili la jifunze kujifunza kwa makini nadhani leo tupo part 3 ambapo tuliamua
tufahamu kinaga ubaga kwa namna gani akili ya mwanadamu hufanya kazi ilikuweza kulowea
ndani kabisa ya somo letu la jifunze kujifunza.
Na, kama utakumbuka part 2 iliyopita tulizungumza kuhusu
sehemu ya kwanza ya ubongo ambayo ni, Conscious mind (CM). Na hii,
tulisema kuwa ni sehemu ya ubongo ambayo tupo na uelewa nayo . ni sehemu ya
ubongo ambayo inashughulika na matendo
yote ya hiali ambayo mtu anaweza
kuyazuia au kuyaruhusu yafanyike, wakati mwingine wamombo wanasema its a
logical portion of our mind, na inauwezo wa kufikri kwa mantiki(logically),
kuchakata na kufanya maamuzi kupitia matukio. Mfano kujifunza kupitia makosa,
kuweka malengo. Kwa ujumla tunaweza kusema mambo na matukio yote ambayo unaweza
kufikri na kuamua kwa utashi wako mwenyewe mf, unaweza kuamua kutembea au
usitembee, kusoma au usisome, kuoga au usioge, kukimbia au usikimbie, kupiga
makofi au laah, kunyosha mkono na mengine kama hayo. Sehemu ya ubongo
inayohusika na mawazo, na matendo ya hiali inaitwa conscious mind (CM).
Kwa kuwa conscioius mind ipo na mapungufu
kadhaa(limitations) ambayo kama vile; Inaukomo wa
kumbukumbu (limited memory) na Inaweza kufanya kitu kimoja tu kwa wakati mmoja
(It can do only a single task at a time). Sasa hapo ndipo sehemu ya pili
ya ubongo huingilia kati kuziba mapungufu ya conscious mind. Twende pamoja
tuangalie ni kwa namna gani subconscious mind inavyofanya kazi.
SUB-CONSCIOUS MIND (SCM): Hii
ni, sehemu ya ubongo ambayo hatuna uelewa nayo. Wazungu wanasema is the portion of our mind that we’re unaware of. Na
hii, ni toufauti na conscious mind ambayo hufanya kazi pindi bindamu akiwa
macho tu, lakini hii, hufanya kazi muda wote yaani, saa 24, siku saba za wiki.
Inahusika na matendo yasiyo ya hiali kama vile; mapigo ya moyo, kupumua n.k.,
inahusika na hisia pamoja na tabia ya mtu husika. Pasipo kusaidiwa na conscious
mind, hufanya kazi muda wote na inawasiliana na kila seli kwenye mwili wa
mwanadamu huku ikipokea na kutuma taarifa na maelekezo mbalimbali akilwa macho
au amelala ndiyo maana, hata kama mtu amelala ukimchoma sindano ana shituka au
ukimwita mara kadhaa anaitika. nd Sub conscious mind huwa inajifunza na kupokea
vitu kutoka kwa conscious mind kupitia kitendo cha kujirudia
rudia (repeation) ambapo ndani yake huunda seli ya kitu hicho na kisha,
baadaye kitu hicho kinakuwa ni sehemu yake. Kwa mfano mtoto anapo jifunza
kutembea anaanza kidogo kidogo na kwa maelekezo na usimamizi maalumu. Kisha
hufanya hivyo mara kwa mara na hapo ndipo seli zake huundwa hata kuanza
kutembea au kukimbia pasipo kufikiria au kujiuliza uliza tena. Kitendo hiki chaweza
kuambatana na maumivu kadhaa (painstaking process)
Sifa za sub-conscious mind
1.
Haina ukomo wa kumbukumbu (has no
limited memory). Sub-conscious mind haina ukomo wa kumbukumbu kama
ilivyo kwa conscious mind ambapo kama kitu kikikaa ndani ya sub-consciius mind
kukisahau sahau inakuwa ngumu sana. kwani, huwa inageaka na kuwa tabia. Mfano,
ukianza tabia ya kuwasema watu (kusengenya)
na ukafanya mara kwa mara utashangaa itakavyokuwa tabia yako ya
kusengenya watu. Kwa ufupi, hii ni memori ya mtu ambayo inahifadhi matukio yote
kutoka kipindi anazaliwa hadi anakufa ambayo mtu amewahi kuyafanya. Yaani, vitu
alivyowahi kusikia na vitu alivyowahi kuona. Sasa utajiuliza sijui ni GB ngapi
vile? Ndiyo maana, unaweza kukutana na mtu mara ya kwanza hata mkimaliza miaka
mingi ikakata hamjaaonana siku ukimwona hata kama ulikuwa ulishasahau sub-consious
mind itakukumbusha na kukwambia kuwa hii sura siyo ngeni machoni kwangu. Hii ni
sawa na kusema kuwa, taarifa za mtu huyo zilikuwepo kwenye kompyuta ya ubongo
wako.
2.
Ni sehemu ya ubongo inayo
husika na hisia za mtu. Hisia za kila namna ndani ya mtu huweza
kuzalishwa ndani ya ubongo, kuendeshwa na kuhifadhiwa hapa. Hisia hizi ni kama
vile, upendo, wivu, chuki, hasira, furaha, nyinginezo. Amygdala ndipo hisia
hupatikana.
3.
Hufanya shughuli nyingi kwa
wakati mmoja. Kwa kimombo
tunaweza kusema “it can perform multiple tasks per time”. Sehemu hii
haichagui ni kwa kiwango gani kazi zipo yenyewe hujali kufanya kazi hasa zile
muhimu na ambazo imezihifadhi. Hii ni sawa na kusema hufanya kazi saa 24 hata
kama mtu amelala huendelea kumeng’enya chakula, kusukuma damu, huendelea
kupumua, huendelea kufanya kazi tu. Yaani, ni kama kompyuta ndani ya mtu.
4.
Inahifadhi tabia, hisia na imani.
Kwa manahiyo, tabia, hisia na imani ambayo
mtu ameshikilia na kuweka msimamo kwayo. Hii hutokana na vitu ambavyo
ameshikilia ndani yake.
Katika hili, kwa kuwa ukifanya kitu kwa kurudia rudia
tena kwa hisia hupandikizwa ndani yake na mwisho wake huwa tabia yake. Pasipo
kujua wengi wamejikuta na tabia ambazo hata hawajui zimetoka wapi. Uhalisia ni
kwamba watu wengi wamepandikizwa maneno machafu na mabaya kutoka utotoni na
vimesemwa kwa hisia hata kuingia ndani
ya sub- conscious mind na kutengeneza picha ambayo hutoka nje kama tabia. Na
ndiyo maana James Thomson alisema “your reality will altermately match the
sub- conscious image you have of your self” tafsiri yake ni kusema
“uhalisia wako utafanana na picha uliyo nayo kwenye ufahamu wako”. Kwahiyo,
picha uliyo nayo ndani ya akili yako ndiyo hujulisha uwe mtu wa namna gani. Kama
umejaza maneno hasi ndani yako sub-conscious mind yako itaanza kufanya hadi
kufananania picha uliyo nayo ndani yako.
Katika upande huu ni sawa na kusema kama umejaza maneno
ya utajiri ndani yako, sub-conscious mind itaanza kufanya na kufanania kile
kilichomo ndani yako ambacho ni utajiri. Vivyo hivyo, kama uliambiwa kuwa wewe,
ni mvivu, wewe ni masikini, wewe ni jasiri, muoga na mengine kama hayo, mambo
hayo yalisemwa kwako kwa kurudia rudia hadi yakatengeneza picha ambayo ipo
ndani ya SCM yako. Hata maandiko matakatifu yanasema “Maana
aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo” soma(mithali23:7) hichi kitu
ndo alikuwa anakisemea sasa.
Kwa maana hiyo, kama ukiona mtu anafanya mambo na tabia mbaya
huna haja ya kutafuta mchawi ni nani. Bali ni maneno ya hovyo yaliyojazwa ndani
ya SCM yake. Kwa kutokulitambua hilo
wazazi wamewatukana sana watoto wao wamesema maneno ya kikatili sana,
majina ya ajabu sana utakuta mzazi
anamwambia mwanaye mbwa wewe, nyau, jambazi, maneno haya yamezalisha picha
ambayo imewajeruhi hata ukubwani.
Hivi ulisha wahi kujiuliza kuwa kwanini maswala ya imani,
tabia na hisia ni ngumu sana kuyashinda au kuyaacha? Pengine ni ngumu sana
kubadilisha hisia za mtu, au tabia za mtu, imani ya mtu ndo usiseme sasa. Hii ni
kwasababu, tabia, imani, na hisia
hukaa ndani ya sub-conscious mind ambayo hatuna uelewa nayo ni tofauti na conscious
mind tunayoifahamu na kuamua juu yake. Ndiyo maana ni rahisi sana mtu kumchoma
mtu kisu kwaajili ya mapenzi, au kumuua mtu kwaajili ya imani yake, au utashangaa
mtu anatamani sana kuacha ulevi au uchawi lakini hawezi kuacha hii ni sababu
ile ya sub-conscious mind ambayo hujiongoza yenyewe. Lakini unaweza kuiendesha
na kuiamuru Scm kwa vyovyote unavyotaka mwenyewe kwa kupitia maneno. Na hata
kuwa vile wewe unavyotaka. Kama unatabia au maneno hasi ndani yako unaweza
kuyaondosha kwa wepesi kabisa na kuweka tabia yeyote unayotaka mwenyewe.
Nadhani tumeona japo kwa uchache kuhusu CM na SCM kwa namna zilivyo na zinavyo husiana. Ya kwamba, kitu ili kiingie SCM kinaanzia kwenye CM ambapo mtu mwenyewe anaamua kujizoesha pengine hata kuzoeshwa na watu bila yeye kujua mara kwa mara na hata kuwa tabia yake ambayo ipo kwenye SCM. Kumbuka neno kurudia rudia ni muhimu sana. hapo ndiyo utakuja kuona waswahili wanasema mazoea hujenga tabia. Part 4 tutaona njia rahisi ya kupandikiza maneno au tabia yeyote unayo itaka, au kuondosha tabia yeyote usiyoitaka ndani yako na hapo utashangaa itakuwa ni rahisi sana kwako na kwa watu wanaokuzunguka kuwasaidia kujenga tabia wanazozipenda au kuachana na tabia wasizozipenda katika maisha yao. Hivyo usikose kufuatilia masomo haya mazuri na ikiwezekana mshirikishe na rafiki yako si unajua kizuri kula na mwenziyo!
kusoma sehemu inayofuata bonyeza hapa
Rafiki, ni matumaini yangu kuwa umejifunza kitu.
na kama unachangamoto katika hili pengine namna gani ya kuondokana na adha hii sasa waweza kuwasiliana na mimi moja kwa moja kupitia mawasiliano hapo chini naamini utasaidika.
GeT tO ThE nExT lEvEl!
Makala hii, imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO ELIAS Mshauri & Mwalimu Wa Saikolojia, Uchumi na Maisha. Mwanzilishi na Mwendeshaji wa Mtandao wa addvalue. Karibu sana ujiongezee thamani yako.
Kwa mawasiliano;
Whatsapp & Sim >>+255767653697 /+255783327456
Email>> eliasmigongo120@gmail.com.
Facebook>> MIGONGO ELIAS.
LinkedIn>>Migongoe.
Pinterest>>eliasmigongo.
Kama umejifunza kitu, niachie maoni yako nitafurahi kujifunza pamoja nawe.
Sort by: Date Rating Last Activity
Comments by IntenseDebate
Posting anonymously.
Ezekiel Tulyanje · 91 weeks ago
Migongo · 90 weeks ago