MAAJABU YA AKIBA

JIFUNZE KUJIFUNZA PART IV.
JINSI AKILI YA BINADAMU UNAVYOWEZA KUIAMURU.
“The greatest revolution in our generation is the discovery
that human beings by changing the inner attitudes of their minds can change the
outer aspects of their lives”. Maneno haya aliwahi kusema mwanasaikolojia maarufu
nchini marekani Willium James. Akimaanisha kwamba mageuzi makubwa katika
kizazi chetu ni kugundua kuwa kwa kubadili mtazamo wa ndani ya akili zetu,
tunaweza kubadili mitazamo yetu ya maisha ya nje.
Tupo katika mfululizo wa somo letu pendwa la JIFUNZE
KUJIFUNZA na hii ikiwa ni part iv, kama utakuwa unafuatilia
tumejifunza mengi huko nyuma, ikiwemo consicious, sub- conscious mind na
mengine kibao. Na kama hujasoma kabisa, nikushauri usome tena kwa makini
itakusaidia sana asee. Na, ikiwezekana umwalike na kumshirikisha jirani yako.
Sasa leo tuna kwenda kujifunza ni kwa namna gani mtu
anaweza kuiamuru akili yake kufanya chochote anacho kitaka, iwe ni maneno
mazuri, tabia nzuri au pengine kuondokana na tabia mbaya ambayo mtu hazitaki. Kutoka
part iv utaweza kupandikiza maneno yeyote yawe mazuri au mabaya kwenye akili
yako, pia utakuwa na uwezo wa kupandikiza tabia yeyote unayoitaka mwenyewe na
kufanya namna yeyote ya kuzungumza na ubongo au akili yako, hivyo nikusihi
ufatane nami katika safiri ya somo hili muhimu.
Katika kupandikiza maneno au tabia yeyote kwenye akili yako ni kitu rahisi sana na hapo tunakwenda kutumia hatua hizi tatu ambazo ni
i. Andaa sifa au tabia unazotaka mwenyewe;
ii. Andika kwenye karatasi sifa zote unazotaka
iii. Pandikiza kwenye akili yako.
Karibu
tujifunze kwa pamoja ni kwa namna gani hatu hizi tatu unaweza kuzifaulu hatua
kwa hatua na hata kupandikiza sifa, maneno au tabia ambazo mwenyewe unaitaka.
Andaa sifa au tabia unazotaka uwe
nazo mwenyewe;
Katika hatua hii ni muhimu kukaa na kufikiria
kwa mapana kuhusu maisha yako kwa ujumla, hapa utaweza kutengeneza maneo, sifa
au tabia nzuri ambazo wewe unazitaka uwe nazo, pia ni muhimu kufahamu wewe ni nani
wa sasa na unataka kuwa nani wa baadaye na hapo ndipo unaweza kutengeneza tabia
yeyote unayoitaka. Mfano unaweza kuandaa na kujisemea maneno kama;
ii. Mimi ni baba bora wa familia,
iii. Mimi ni tajiri mkubwa,
iv. Mimi ni jasiri na ninajiamini,
v. Mimi ni mwenye ushawishi mkubwa duniani,
vi. Mimi ni kiongozi bora duniani, nina afya njema,
vii. Nina mahusiano yenye furaha na upendo mwingi.
Hiii ni mifano tu ya namna unavyo weza kuandaa maneono au
sifa ambazo wewe unataka, haijarishi ni maneno kiasi gani utaweka kikubwa tu ni
wewe kuangalia sifa au tabia unazozitaka mwenyewe, na kitu cha kuzingatia hapo
ni kwamba sifa hizo ni muhimu zikahusisha kila nyanja ya maisha yako na hapa ni
pamoja na afya yako, mahusiano yako, uchumi wako, biashara, familia, elimu na
sehemu nyingine muhimu za maisha yako.
Vitu viwili muhimu vya kuzingatia unapo andaa sifa aua
tabia unazozitaka.
a) Zote
ziwe katika wakati uliopo.
Kama
utaangalia kwa makini sifa hapo juu zote zipo katika wakati uliopo. Hata wewe
unashauriwa unapoandaa vigezo au sifa unazo zitaka ni lazima uviweke katika
wakati uliopo yaani iwe kama tayari umeshapata au umeshakuwa mtu unaye taka. Hii
ni kwasababu wanasaikolojia wengi wanasema kuwa Subconscious mind inaishi katika
wakati uliopo tu. Mfano unaweza kusema mimi ni mchezaji bora ulimwenguni, mimi
ni mfanyabiashara mkubwa duniani. Ninacho maanisha ni kwamba hata kama kitu unachokitaka
hujakipata bado kiweke kama vile umeshakipata tayari.
b) Zote ziwe chanya.
Hata
ukiangalia mifano yetu hapo juu utakuja gundua kuwa yote ipo katika hali ya uchanya
wala siyo hasi. Usiandike maneno ambayo yapo kinyume na unavyotaka, baadhi ya
wanasaikolojia wanaamini kuwa subconscious mind inaelewa na kusikia maneno
chanya pekee yake na haielewi wala kusikia maneno hasi kama vile “siyo”,
mfano hauhitaji kusema mimi siyo masikini. Hapo SCM haitaelewa neno siyo hivyo itatafsiri kama
mimi ni masikini. Hivyo badala yake waweza kusema mimi ni tajiri, mimi ni
sumaku ya fedha na mengine kama hayo.
Andika kwenye karatasi sifa zote
unazozitaka.
Ukishajua sifa au tabia gani unatamani uwenazo ambazo
pengine kwa sasa huna, ni muhimu kuziandika
kwenye daftali hapa pia itakubidi uwe na daftali na kalamu ilikuandika kama
vile wewe unavyotaka uwe. Na hii, itarahisisha wewe kukumbuka kwa wepesi sifa
gani umeweka na sifa gani umesahau. Unaweza kuandika na kuya kagua mara kwa
mara na hapo unawea kuongeza mengine au kupunguza kutokana na mahitaji yako.
Anza kupandikiza ndani ya SCM.
Kutoka katika sifa ulizoziandaa na kuziandika kwenye
hatua ya kwanza na ya pili sasa ni hatua muhimu ya kuamuru na kupandikiza maneno
au sifa hizo. Na hii ni rahisi sana kama utatuliza akili na kusafisha akili
yako(relax), waweza kutafuta sehemu tulivu ukafanya hivyo mara kwa mara na hapo
pia, unaweza kusoma kwa sauti au kimya kimya. Katika hali ya kutulia sana
waweza kufumba macho au ukafumbua inategemeana na wewe mwenyewe.
Inashuriwa pia utumie muda wa kabla ya kulala au asubhi
baada ya kuamka kwasababu muda huo Subconscious mind inakuwa makini sana kupokea
kitu kipya, ndiyo maana haishauriwi sana
kusikilia, kutazama au kufuatilia taarifa mbaya asubhi badala yake utumie muda
huo kupandikiza kitu kizuri na chenye manufaa ndani yako kwani wakati huo SCM
inakuwa ACTIVE sana kupokea vitu. Hivyo ni muhimu kufahamu hali kama
hiyo ili kufanya kwa uhakika bila
kubahatikasha.
Yote kwa yote haijalishi ni muda gani utapitia sifa na
tabia ulizoziandaa kitu kikubwa ni kutafuta utulivu wa akili(relax) na
kusafisha akili na hii unaweza kufanyaa
kwa kutafuta sehemu tulivu kisha fumba macho, vuta pumzi kwa nguvu na anza
kuiachia kidogo kidogo huku ukihesabu 1 hadi 5. Hakikisha upo katika hali ya
utulivu kwani utulivu yaani, relaxation ni mlango wa kufungulia SCM si unajua
hii inatumia sana hisia basi na wewe uwe katika hali ya utulivu na hisia.
Na ufanyavyo hivyo hakikisha unajenga taswira ya kile
unachokitaka na uwe kana kwamba unakiona. Weka matarajio hayo na pitia mara kwa
mara kila siku kadiri utakavyo weza, rudia tena na tena hadi scm itakapo
ikubali hali hiyo na kuwa mtu ndoto zako.
Kadiri utakavyo kuwa unafanya hivyo utakuwa unaona mabadiliko
kidogo kidogo hadi picha uliyo ijenga ndani inakuwa uhalisia wako. Na utashangaa
kuona tabia za nyuma unaanza kuachana nazo kabisa kwani, tunasema SCM haiwezi
kushikiria tabia mbili zinazokinzana kwa wakati mmoja mfano uoga na ujasiri,
umasikini na utajiri, enye akili na mjinga kwa hiyo itachangua kitu kimoja
ambacho huwa unakifanyia kazi mara kwa mara
na hapo ndipo itakapoishinda tabia nyingine. Hapo utakuja kuona mtu
alikuwa na tabia mbaya mf ulevi na mara baada ya kuweka mikakati ya kuacha na
ulevi huo utashangaa huyu mtu anabadilika kabisa na watu wataesma huyu jamaa
amebadilika kweli kweli. Katika hatu zote utaona madabiliko yanatokea na
mabadiliko hayo yanawezaonekana au hayaonekani lakini mwisho wake matokeo
huonekana.
Kitu kikubwa tufahamu kuwa kutengeneza sifa na tabia
tunazo zitaka kwaajili ya kuzipandikiza kwenye akili zetu na kuwa sehemu ya
maisha yetu au kuachana na baadhi ya tabia mbaya ambazo hatuzitaki. Siyo kazi
nyepesi hivyo itahitaji muda, kurudia mara kwa mara (repeatation), patience(uvumilivu),
kufanyia kazi na utekelezaji wa kile tunachokitaka kiwe ndani yetu. Yaani, ninachotaka
uelewe ni kwamba kama utasema wewe ni mchezaji bora duniani anza kutafuta na
kufanya vitu na mbinu zitakazo kufanya kuwa bora kama kufanya mazoezi n.k.
vivyo hivyo kama wewe ni tajiri anza kuchukua hatua na kufanya kazi kwa bidiii
matokeo utayapenda na hakika utakubali.
Kwa leo itoshe kusema tuonane part v usiache kufuatilia.
Rafiki, ni matumaini yangu kuwa umejifunza kitu.
na kama unachangamoto katika hili pengine namna gani ya kuondokana na adha hii sasa waweza kuwasiliana na mimi moja kwa moja kupitia mawasiliano hapo chini naamini utasaidika.
GeT tO ThE nExT lEvEl!
Makala hii, imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO ELIAS Mshauri & Mwalimu Wa Saikolojia, Uchumi na Maisha. Mwanzilishi na Mwendeshaji wa Mtandao wa addvalue. Karibu sana ujiongezee thamani yako.
Kwa mawasiliano;
Whatsapp & Sim >>+255767653697 /+255783327456
Email>> eliasmigongo120@gmail.com.
Facebook>> MIGONGO ELIAS.
LinkedIn>>Migongoe.
Pinterest>>eliasmigongo.
Kama umejifunza kitu, niachie maoni yako nitafurahi kujifunza pamoja nawe.
Sort by: Date Rating Last Activity
Comments by IntenseDebate
Posting anonymously.
Cheyo, · 89 weeks ago
Migongo · 89 weeks ago