MAAJABU YA AKIBA

JIFUNZE KUJIFUNZA PART V
SIFA NA SHERIA ZA AKILI YA MWANADAMU KATIKA KUJIFUNZA.
Hallo uhali gani ndugu msomaji! Ni matumaini yangu kuwa
unaendelea vyema vinginevyo Mungu akusaidie sana. Nikukaribishe tena katika
mfululizo wa somo letu pendwa la JIFUNZE KUJIFUNZA na leo tupo katika (part/sehemu)
ya tano. Somo hili watu wengi wamekubali kuwa ni ufunguo tosha wa akili na
maisha yao kwa ujumla. Hivyo ni muhimu sana, kwako kujumuika nasi ili kujifunza
pamoja nikukaribishe sana.
Kama umefuatilia somo hili tumezungumza mengi sana juu ya
namna gani akili ya binadamu inavyofanya kazi, mugawanyo wa akili ya binadamu
katika utendaji kazi wake, namna gani unaweza kuuamuru ubongo wako na namna nzuri
ya kupandikiza tabiia au sifa yeyote kwenye ubongo wako na mengine kibao. Kama hujasoma huko nyuma ni
wazi kuwa umekosa mengi, lakini habari njema ni kwamba unaweza kufuatilia somo
hili toka mwanzo kupitia linki hapa chini.
Sasa leo nahitaji tupige hatua kidogo kwa kuangalia sifa
na sheria kadhaa za akili yako katika kujifunza, ili kujua namna nzuri ya
kujifunza kwa wepesi chochote utakacho. Bila shaka kwa kufamu tabia, sifa na
nini akili yako inapendelea utaweza kujifunza kwa haraka na wepesi zaidi. Hivyo
fuatana nami tujifunze kwa pamoja sifa
hizi;
Namba moja: Akili yako inapenda taarifa.
Binadamu ameumbiwa milango mitano ya fahamu yaani, pua, ulimi,
ngozi, masikio na macho. kwaajili ya kupitisha taarifa kutoka mazingira ya nje
kwenda ndani. Ndani ya ubongo wa mwanadamu kuna homoni kadhaa zinazohusika na
kuleta furaha ndani yake pindi anajifunza kitu kipya, dopamine na cytokinin hutoa
kemikali za furaha juu ya mtu. Ukweli ukijifunza kitu kipya utafurahia kutokana
na kuwepo kwa homoni hizo. Ndiyo maana, mfano boss wako, mpenzi wako, au mtu
yeyote akikuahidi kukwambia kitu, unakuwa na shauku sana ya kupata kusikia na
kujua ni kitu gani hicho. Hivi ulisha wahi kujiuliza kwanini walevi huwa
wanaenda kulewa baa wakati wanauwezo wa kunywa na kulewa nyumbani? Ni muhimu
katika kujifunza tafuta taarifa mpya chanya, kwa kusoma vitabu, kusikiliza video,
na kujifunza kutoka kwenye vyanzo vingine muhimu. Usiwekeze kupata taarifa mbaya
au hasi.
Namba mbili: Akili yako inapenda miunganiko (connections).
Kwenye ubongo wa mwanadamu kuna Axons na dendrites ambazo zimeungana pamoja
ilikuwezesha na kujifunza kuweze kupita kwa wepesi kutoka neuron moja kwenda
neuron nyingine. Vivyo hivyo katika kujifunza mtu anapojifunza taarifa mpya,
pamoja na kuwa ubongo wake hufurahia sana lakini kipindi cha kujifunza huwa inafanya
muunganiko wa taarifa mbali mbali katika
kipindi hiki utakuta mtu anaelewa kitu hadi anaanza kusema anhaa, kumbe au
ndiyo maana, n.k. wakati mwingine unakuta mtu anakuelezea au kukusimulia tukio/hadithi
fulani lakini utashangaa kunapicha ya mazingira fulani unakuwa umeijenga juu ya
hiyo hadithi mahali ilipo tokea wahusika na mandhari. Au kama ulisha wahi
kuangalia muvi utaanza kubashiri na kutabiri jinsi kipande kinachofuata
itakavyo kuwa kuhusu muvi hiyo. Kitu hiki tunasema connecting the dots.
Namba tatu: Akili yako inapenda kuiga.
Ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya kujifunza kwa
mwanadamu hufanyika kutokana na kuwatazama wengine yaani, kwa kuona hapo ndipo
kuiga huanzaia. Na hii utaona kuwa tumezaliwa na kukua huku tumejifunza mambo mengi kwa kuwaiga
wengine wanavyofanya mfano ulizaliwa hujui kuongea wala kufanya kazi, lakini
ulijifunza kutoka kwa wazazi wako na watu wengine kwa namna wanavyofanya na wewe ukajikuta
umefahamu kuongea na kufanya mambo mengine. Hivi ulishawahi kuona darasani
wanafunzi wamefananisha majibu wote? Utashangaa kuona kipanga wa darasa akijaza
njia fulani darasa lote litajaza njia hiyo. Tumejifunza elimu lugha na hata
maisha kwa kuwaiga wengine. Hii ndiyo imekuja kuzalisha kanuni moja inaitwa copy
cut principle ambayo inadai kuwa kitu chochote mtu yeyote akikianziasha
baada ya miezi sita kitaenea maeneo mbali mbali kama anavyofanya yeye. Kwa maana
hii ndiyo maana watu huwa wanakuwa na mentors, coaches na wakufunzi mbali mbali
kwaajili ya kujifunza kwao. Jitahidi kujifunza kutoka kwa watu na usiwaige
watu!
Namba nne: Akili yako hunawili na kufanya
kazi kupitia mifumo(patterns).
Kama utakumbuka habari ya conscious mind na subconscious
mind na sifa kubwa na kupandikiza sifa au maneno tunafanya kwamurudio rudio repteation
kitu hiki hutengeneza njia au mifumo /partterns. Ambapo baadaye hugeuka na kuwa
njia yake na mtu hufanya jambo hilo kama kawaida. Kitu hiki kujenga mazoea na
mwisho huwa kama tabia, mfano hivi ni nani alikwambia kuwa moto ni hatari? Au baadhi
ya wanyama au wadudu ni hatari? Hii ni mifumo parterns ambao mfumo huwa hujijengea
na kuufuata katika maisha ya kila siku. Ndiyo maana wanafunzi husoma na kupitia
notisi zao kabla ya kuingia kwenye mtihani. Hivi kwanini mtu akizungumza lugha
yako unamwelewa? Au akikuita jina lako unageuka na kuitika, hii ni kwasababu ya
patterns ambazo akili yako imejifanyia kwa mara ya kwanza unajifunza yaani
ilikuwa inatengeneza njia. Unaweza usielewe kitu fulani au somo au lugha fulani
si kwasababu huna akili bali ni vile tu hujatengeneza njia ya hicho kitu,
changamka!
Namba nne: Akili yako haifanyi kazi vizuri
kwenye stress.
Lucas Bill aliandika kuwa “When your brain is under
severe stress, it can only think of survival”. Waswahili husema akili yako iikiwa katika mawazo makali, huwa
inawezakufikiri kujinusuru tu. Wataalamu
wanashauri sana usifanye maamuzi yatakayo gharimu maisha yako ukiwa na stress (msongo
wa mawazo) akili yako haifanyi vyema katika kipindi hiki, msongo wa mawazo na
hatari zingine zikitokea au zikitarajiwa kutokea akili ya mtu huwaza namna ya
kujiokoa tu na sivinginevyo, na hii hutokana na kuwepo kwa homoni kama adrenaline
ambazo huajilia nguvu ya kupambana na hatari au kuikwepa hatari. Na katika
kipindi hiki utashangaa kiwete kuruka kwenye kiti pale hatari inapotokea.
Ndugu msomaji yapo mengi sana ya kufahamu kuhusu ubongo
wetu kuliko vile tunavyofahamu kuhusu injini za magari na mifumo mingine
mikubwa duniani ndiyo maana Bill alisema “When it comes to our mind, most of us
know less about it than we do about the engine of our car.” Yaani lipokuja suala la akili watu wengi
tunafahamu kidogo kuhusu akili kuliko tunavyofahamu kuhusu injini za magari
mbalimbali.Kwa maana hiyo tuendelee kufuatilia na kujifunza kwa manani juu ya
hili. Ukiyafahamu haya utaweza kutumia vyema akili yako katika kujifunza na
kufanya jambo chanya kwako na kwa wepesi sana si unajua hakuna mtu ambaye hana
akila kama wengine wanavyo jiitaga kwamba hawana akili.
kusoma mwendelezo wake bonyeza hapa
Rafiki, ni matumaini yangu kuwa umejifunza
kitu.
na kama unachangamoto katika hili pengine
namna gani ya kuondokana na adha hii sasa waweza kuwasiliana na mimi moja kwa
moja kupitia mawasiliano hapo chini naamini utasaidika.
GeT tO ThE nExT lEvEl!
Makala hii, imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO
ELIAS Mshauri & Mwalimu Wa Saikolojia, Uchumi na Maisha.
Mwanzilishi na Mwendeshaji wa Mtandao wa addvaluetz. Karibu
sana ujiongezee thamani yako.
Kwa mawasiliano;
Whatsapp & Sim >>+255767653697
/+255783327456
Email>> eliasmigongo120@gmail.com.
Facebook>> MIGONGO ELIAS.
LinkedIn>>Migongoe.
Instagram>>migongo_elias.
Pinterest>>eliasmigongo.
Kama umejifunza kitu, niachie maoni yako
nitafurahi kujifunza pamoja nawe.
Sort by: Date Rating Last Activity
Comments by IntenseDebate
Posting anonymously.
Gody · 90 weeks ago
Migongo · 90 weeks ago