MAAJABU YA AKIBA

NGUVU YA ZAWADI KATIKA KUJIFUNZA.
Ndugu msomaji wasalaamu! Nikukaribishe tena katika mwendelezo wa somo letu pendwa la jifunze kujifunza, ambapo tumeona na kujifunza mengi sehemu zilizopita. Hadi sasa tupo katika sehemu ya sita. Lengo kubwa likiwa ni kufahamu akili zetu, zinafanyaje kazi, namna gani tunaweza kuzitumia, huku tukigundua kuwa Kujifunza kujifunza ni eneo muhimu sana ambalo limesahaulika sana katika jamiii zetu. Vitu kama hivi mara nyingi haviwekwi kabisa kwenye mitaala ya elemu, siyo afrika wala kule kwa mabeberu. Hivyo kwasababu ya umuhimu wake ADD VALUE NETWORK imeamua kuzamia ili kukutafunia na kukuletea kwako kupitia hapahapa add value network kazi yako ni kumeza na kula tu!
kusoma sehemu iliyopita bofya hapa
Sasa twende pamoja tujifunze kwa pamoja;
Sehemu ya leo tunakwenda kuangalia nguvu ya zawadi katika
kujifunza kwakuwa tunazungumzia kuhusu
zawadi, ni muhimu tukafahamu maana halisi ya zawadi. Katika hili kamusi ya
kiswahili inasema kuwa, “zawadi ni kitu chochote ambacho anapewa mtu aliyeshinda
jambo fulani au kwaajili ya kuonyesha urafiki, upendo, au shukurani kwake.”
Wakati mwingine Lucas Bill alisema “we only reward
or value what our theories tell us are mportant”, kwamba huwa tunazawadia au
kuthamini kile ambacho nadharia zetu hutuambia kuwa ni cha muhimu. Kumbe watu
wakati mwingine hutoa zawadi kwaajili ya kuonyesha thamani au umuhimu wa kitu au
mtu katika maisha ya mtu.
Tumeona mashirika, familia, taasisi, na sehemu zingine
watu hutoa zawadi kedekede kwa wafanyakazi wake ambao hufanya vizuri zaidi katika
kufanya kazi. Na lengo likiwa ni kutambua juhudi zao na mchango wao katika kampuni
husika. Lakini imekuwa tofauti kabisa katika kujifunza wengi hawajui umuhimu wa
kujifunza ndiyo maana hawalipi kipaumbele eneo hili.
Ujue zawadi inanguvu katika kutia hamasa eeh! Ndiyo
maana maandiko matakatifu yanasema “zawadi ya mtu humpatia nafasi; humleta
mbele ya watu wakuu” soma mithali 18:16, kuna namna fulani hivi mtu akikupa
zawadi labda tusema ya birthay, au shelehe anakuwa kama amekukopesha vile yaani
nawewe unakuwa unatafuta namna ya kumlipa zawadi yake siku akiwa na tukio. Tunasema
the best gain is to lose. Yaani, njia bora ya kupata kitu ni kutoa kitu.
Goja nikutonye kidogo kuhusu mfumo wa akili yako, mfumo wa akili yako hufanya kazi katika mifumo
miwili ambayo ni limbic system mfumo
huu unahusika na raha pamoja na starehe hapa
raha na starehe zote mtu anazozipata huratibiwa na mfumo huu, mfumo huu hukomaa
akiwa anazaliwa ndiyo maana watoto hupenda kulala na kubebwa. Mfumo wa pili
ni cortex system huu ni mufumo
ambao unahusika na kufanya maamuzi na kuratibu shughuli zingine za mwili. Mfumo
huu ni tofauti na limbic ambao hukomaa kadiri mtu anavyokua. Kama akili haitaongozwa
kufanya mambo yenye tija hukimbilia kufanya mambo ya raha na furaha tu! Mfano kulala,
kukaa, kuangalia tv, kuchati na mengine kama hayo.
Pia katika kujifunza ni muhimu kuwa na zawadi pindi
unapojifunza na zawadi ya weza kuwa ni nzuri kama kutoa kitu upendacho au kukupa
raha mfano kucheza, kutoka out, au kuchati endapo tu utajifunza kitu kipya. Je wewe
huwa unajipongeza kila ukijifunza kitu kipya? Basi anza leo, waweza kusema leo
sitachati au kuingia online hadi nisome kitabu fulani, au leo sitenda kutembea
hadi njifunze kitu fulani na ukifanikisha waweza kuchati, kutembea au kula kama
zawadi. Lakini pia, yawezakuwa kwa mfumo wa adhabu kama hutokamilisha lengo ni
kutia hamasa nakuushinda limbic system ambao unahitaji kudekezwa.
Kujifunza ninaakokuzungumzia hapa siyo kule darasani tu,
bali hata namna ya kufahamu au kujifunza chochote katika maisha yetu ya kila
siku. Na zawadi nninayoizungumzia hapa ni hamasa. Na lengo lake ni kumotivate
yaani, kuhamasisha.
Na hamasa hii imegawanyika katika aina kuu mbili ambazo
ni hamasa ya ndani(intrinsic motivation) ambayo ni sawa na zawadi kutoka ndani,
na hamasa ya nje (extrinsic motivation) ni sawa na zawadi kutoka nje
Zawadi kutoka ndani ni hii huzalishwa kutoka ndani ya mtu
husika mara baada ya kujifunza kitu kipya. kama tiulivyoona katika sehemu
ya nne ya somo letu. Kutokana na kuwepo
kwa homoni kama dopamine n.k zinazotoa
furaha pindi mtu anapojifunza kitu kipya. Hii ni zawadi kubwa mnoo kwanza
unapata kufahamu vitu vingi, pili unaongeza thamani yako, unapunguza au
kuondosha msongo wa mawazo hivyo
utajikuta umepata furaha na amani ya moyo baada ya kujifunza. Hamasa hii ni
msukumo kutoka ndani unaomsukuma mtu kujifunza au kufahamu kitu kutokana na
umuhumu wake wa hapo baadaye.
Zawadi kutoka nje hii huchochewa na vishawishi kutoka nje
ya mtu utakuta vitu kama pesa, chakula, mavazi, mali, na vitu vingine kama
hivyo. Na hiii hutumiwa sana na taasisi mbali mbali kwaajil ya kuhamasisha
wafanyakazi wake ilikufanya zaidi ya pale. Hata wapendanao huitumia sana hii
zawadi au hamasa hii huwa ni nzuri na huwafanya watu kufanya kazi kwa bidii
huku wakitegemea kupewa chochote kitu. Lakini changamoto yake ni moja hasa pale
unapofanya kitu kwa hamasa toka nje, pindi utakapokosa au kuondokewa na hamasa hutokuwa
na hamasa ya kuendelea au kusonga mbele na katika hili ni seme kuwa usianze
kufanya au kuanzisha kitu kwa msukumo wa nje bali, tumia msukumo na hamasa ya
ndani kitu hicho kitadumu. Yaani,
usianzishe biashara kwasababu rafiki yako anafanya biashara, usiaanzishe kitu
et kwasababu jirani yako anafanya bali fanya
kwakuwa unamsukumo na hicho kitu kisha jifunze kwa watu waliofanikiwa katika
eneo hilo.
Kanuni ya hamasa katika
kujifunza
Watu wengi wamefundishwa vitu vingi hata huko shuleni
lakini wakati mwengine vitu hivyo havitumiki kabisa katika maisha yao pengine
hii ni kutokana kutokufahamu kanuni ya hamasa katika kujifunza kujifunza, na
kanuni hii Andrea Spurling and Jim Smith walipendekeza
namna nzuri ya kuangalia hamasa na kuitumia katika kujifunza, hebu tuangalie
kwa pamoja kanuni hii;
R + V + P + I = M
Motivation halisi yaani, hamasa katika kujifunza inabeba vitu vinne ambavyo ni,
R = Readiness.
Hiki ni kiwango cha utayari wa kujifunza.
Ifahamike kuwa unapijifunza kitu hakili yako ni muhimu iwe tayari katika
kujifunza, mazingira pia yawe tayari n.k hata unapofanya kitu, ni muhimu kuwa na
utayari kwani hii itakuongezea hamasa na uthubutu wa kusonga mbele. Je unataka
kusoma vitabu? Kuwatayari. Unataka kufanya biashara? Kuwa tayari, unataka
kujifunza kingereza? Kuwa tayari. Unataka kujifunza kompyuta? Kuwa tayari nasema
kuwa tayari.
V = Value : hii
in thamani na faida ya kujifunza. Wakati mwingine na mara zote tunajifunza ili
kuongeza maarifa yatakayo onngeza
thamani katika maisha yetu. Si unajua watu muhimu katika jamii zetu ni wale
wanatoa thamani eeh. Wakati mwingine kabla hujaamua kujifunza kitu au kufanya
kitu ni muhimu kuangalia ni thamani gani
utaipata kwa kufanya kitu hicho , si unajua hata kuwasaidia watu kunafaida eeh.
P = probability of
learning being successful. Hii ni uwezekano wa kufanikiwa na kufikia unachokitaka.
Hapa ni sawa na kusema uwezekano wa kitu
unachojifunza kuhusiana na jamii au mazingira upo au laah. Njia za kujifunza zinahusiana
na ninachojifunza au ninachokitaka?
I = Impact of the learning on your life. Hapa tunasema
kitu unachojifunza unaweza kukitumia itumia ilikilete matokeo tarajiwa kwako na kwa jamii?
Hapa swali hili litaamua tujifunze nini na tuache nini kitakacho tunufaisha
sisi na jamiii zetu wala siyo kila kitu kusoma soma tu.
M = is the amount
of motivation you have toward a particular learning opportunity. Kiwango
cha hamasa unachokipata juu ya fursa ya kujifunza. Na hii inabebwa na vitu vinne tajwa hapo juu.
Hivyo kama utaweka utayari kujifunza, na kama kitu
unachojifunza kipo na thamani kwako na kwa ulimwengu kwa ujumla, na kama
utakuwa na uwezo wa kukifanya na kukifikia kitu unchokifanya au kujifunza, na kama kujifunza kwako kutakuwa na matokeo chanya
kwako na kwa jamii nzima nadhani utakuwa umehamasika kwa upande chanya. Tena ,
msukumo kutoka ndani intrinsic motivation hii itakupa nguvu ya kuthubutu
na kuanza kufanya, na hapo ndipo utatumia hamasa ya nje kujiongezea thamani na
kusonga mbele hali hii itakupeleka mbali sana na hutakuwa mtu wa kawaida. Na hapo
ndipo utakuwa umetumia zawadi kubwa katika kujifunza.
Kupata mwendelezo wake bofya hapa
Rafiki, ni matumaini yangu kuwa umejifunza kitu.
na kama unachangamoto katika hili pengine namna gani ya
kuondokana na adha hii sasa waweza kuwasiliana na mimi moja kwa moja kupitia
mawasiliano hapo chini naamini utasaidika.
GeT tO ThE nExT lEvEl!
Makala hii, imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO ELIAS
Mshauri & Mwalimu Wa Saikolojia, Uchumi na Maisha. Mwanzilishi na
Mwendeshaji wa Mtandao wa addvaluetz. Karibu sana ujiongezee thamani yako.
Kwa mawasiliano;
Whatsapp & Sim >>+255767653697 /+255783327456
Email>> eliasmigongo120@gmail.com.
Facebook>> MIGONGO ELIAS.
LinkedIn>>Migongoe.
Instagram>>migongo_elias.
Pinterest>>eliasmigongo.
Kama umejifunza kitu, niachie maoni yako nitafurahi
kujifunza pamoja nawe.
Sort by: Date Rating Last Activity
Comments by IntenseDebate
Posting anonymously.
Cheyo · 88 weeks ago
Migongo · 88 weeks ago
Jofrey Joram Andeshi · 88 weeks ago
Migongo · 88 weeks ago