MAAJABU YA AKIBA

JIFUNZE KUJIFUNZA PART VII.
VIKWAZO KATIKA KUJIFUNZA .
Rafiki wasalaamu! Karibu katika mwendelezo wa somo letu
pendwa la ajifunze kujifunza
ambapo, tunazidi kuchanja mbuga na sehemu ya saba sasa, huku tukiwa tumejifunza
mambo kedekede hapo nyuma. Na kama hujafuatilia nikusihi ufanye hivyo ili upate
kujifunza mengi zaidi hapa hapa ADD VALUE NETWORK.
Leo tunayo sehemu
yetu nzuri ya saba ambapo tunakwenda kutazama kinaga ubaga vikwazo na changamoto katika kujifunza. Kwani,
watu wengi wanaofahamu na wasiofahamu kuwa wanapaswa kujifunza kila leo na
pengine wanafahamu kabisa ni kipi wajifunze na wapi wajifunzie lakini bado
wengi wao imekuwa ni changamoto kwao kujifunza vitu ambavyo wanatamani
kuvifahamu lakini kwakujua au kutokujua wanakutana
na changamoto kibao ambazo huwafanya wasianze kabisa au pengine wasisonge mbele
mara baada ya kuanzisha zoezi la kujifunza kwao. Kitu hiki kimekuwa kama adui
wa kujifunza na kusonga mbele kwa watu wengi katika mambo yao ambayo hutamani
kuyafanya au kusonga mbele kwayo.
Kwasababu huwezi kupigana na adui yako ikiwa humfahamu au
hujui ni njia gani au uwezo gani yupo nao katika pambano hilo. Si unajua
kumfahamu vizuri adui yako tayari ni ushindi kwa asilimia 50% wa vita yako! Kwa
kugundua hilo Addvaluenetwork imeamua kuzamia
kindaki ndaki ili kubaini vikwazo hivyo na kuviweka wazi iliuvifahamu na kisha
uchukue hatua, na hapo ndipo utakapo kuwa mshindi wa vikwazo vyako na utakuwa
umetoboa katika kujifunza kwako. Vikwazo
hivyo ni pamoja na ;
..............................................................
Umri umeenda sana kujifunza; hii
utakutana nayo sana hasa kwa watu wenye umri wa makamo au wazee wakidai kuwa
wao hawana haja ya kujifunza kwani umri wao umeenda sana hakuna haja ya
kujifunza. Hiki tunaweza kukiita ni kikwazo hasa katika eneo la kujifunza. Ukweli ni kwamba kadiri mtu anavyokua ndivyo
cell zake hufa na kuzoofu, lakini ubongo
hufanya kazi kwa connnections na patterns kama tulivyoona siku ile, kwahiyo
kadiri unavyo jifunza vitu vipya na kuufanyisha mazoezi akili yako hunawili na
kuwa imara zaidi. Ndiyo maana maarifa pekee yanaweza kukufanya kuwa kijana hata
kama unamiaka 80, au mzee hata kama unamiaka
20. Au haukusikia wahenga waliposema kuwa elimu haina mwisho? Na kwa
maisha na akili ya mwanadamu ilivyo ni kwamba upende usipende utajifunza tu. Sasa
kama ni hivyo kwanini usijifunze kujifunza kwa hiali yako mwenyewe pengine
ukawa mzee mwenye busara zake??
..............................................................
Kukosa muda wa kujifunza; muda imekuwa ni kisingizio kwa watu wengi, na
wengi wakisema hawana muda wa kujifunza, kuanzisha au kufanya vitu vyao vya msingi
walivyopanga kufanya. Na wakati mwingine utashangaa kuona mtu analalamika muda
wa kufanya mambo yake ya msingi haupo, lakini utaona ana muda wa kutosha kupiga
soga kijiweni, kushinda mtandaoni kutafuta umbea. Hapa ni muhimu kuelewa kuwa muda hautoshi kufanya
kila kitu lakini unatosha kufanya vitu vya muhimu. Hivyo jitahidi kuweka vipaumbele vya nini ufanye
na kipi usifanye, kipi uanze nacho na kipi kifuate. Tambua muda haujawahi
kutosha.
..............................................................
Maneno hasi kutoka kwa watu; utake
usitake kama ukitaka kuanzisha kitu, kufanya au kujifunza kitu chochote
utakutana na maneno hasi kama vile, utaweza kweli, wengi wameshindwa ,
hautafika mbali, achana na hicho kitu na maneno mengine hasi kama hayo ambayo
kwa uhalisia yatakukatisha tamaa au kukuvunjua moyo ili tu usisonge mbele na
mpango wako hasa katika kujifunza au kufanya kitu chochote chenye tija kwa
maisha yako. Bila kujua maneno mengine yatakuja kama ushauri tena kutoka kwa
watu, wakati mwingine watu wako wa karibu kabisa, pengine unaweza kuwa na
mpango wa kujifunza lugha za kigeni au mpango wa kuanzisha biashara, kampuni n.k
tambua kuwa utakutana na maneno lukuki
ya kukurudisha nyuma, nikwambie tu usiwape sikio lako. Hata katika maneno na ushauri tambua kuwa maneno na ushauri mara nyingi hutolewa bure lakini, kuwa
makini kuchagua unaofaa tu.
..............................................................
Ukosefu wa rasilimali;
kwa kweli katika sehemu yeyote ile hakukosi kuwa na changamoto. Ilwe ni
shambani, shuleni, katika biashara, safari na sehemu zingine, changamoto
hazikosi kabisa. Hata katika suala letu la kujifunza utakutana na uhaba wa
vifaa na rasilimali za kujifunzia ambapo yaweza kuwa vitabu, fedha, muda,
wakufunzi, sehemu, n.k. mfano pengine mtu anataka kujenga tabia ya kusoma vitabu
utashangaa analalamika kua hana vitabu vya kusoma. Ukweli ni kwamba pamoja na kuwepo kwa changamoto kama
hizo loakini katika karne hii mambo yamerahisishwa
sana kwani vitabu na rasilimali zingine zinapatika kwa urahisi sana pengine
mtandaoni kwa bei ndogo sana tena wakati
mwingine bure kabisa kwa hiyo ushindwe mwenyewe tu, tena kunakozi
na masomo ambayo gharama zake zipo chini sana na utakapo jifunza na kufuatilia mwanzo mwisha
huta baki kama ulvyo. Tatizo ni kwamba
watu tuko bize mitandaoni lakini hakuna tunachopata zaidi ya habari nyepesi
nyepesi. Unaweza ukawa unailalamikia mitandao ya kijamii kuwa imeharibu na
kupoteza muda wako mwingi kumbe wewe ndo changamoto hujui usome nini na uache
nini unapakia kila kitu goja hili nalo
ni somo la wakati mwingine lakini muhimu kuliko ni kubadilika
Yaani, anza na kile upo nacha kwa wakati huo tena
hapohapo ulipo utashangaa mengine utakavyokuwa unayapata mbele ya safari, huna
haja ya kulalamika huna mtaji anza na kidogo ulicho nacho, hunahaja ya kulalamika
kwamba huna vitabu wakati upo kwenye magurupu 30 ya wasap. Anza na kile upo
nacho....
..............................................................
Ujuaji wa kujiona kama unajua kila kitu;
Kuna namna hii imekuwa kama kikwazo katika kusonga mbele, kwani kuna wakati mtu
anatakiwa kujifunza na pengine kutengeneza sabuni, kulima, kompyuta, udereva na
vitu vingine ambavyo ni muhimu sana kwake lakini utashangaa, kuona akijitapa na
kudai kuwa yeye anajua kila kitu, hivyo hana haja ya kujifunza wala kujiimarisha
mwenyewe katika maisha yake sasa kitu kama hicho haki siyo kizuri, wakati mwingine
utakuta eti kwasababu mtu anadigrii fulani, ataanza kubweteka na kushindwa
kujifunza vitu vingine ambavyo ni muhimu kwake katika kusonga mbele , na hapo
atajiona kama anajua kila kitu na hana haja ya kujifunza vitu vingine. Kitu hiki
siyo kizuri kwani unatakiwa, kujifunza kila siku si una jua ubongo wako
unapenda taarifa eeh! Kama ni hivyo huna haja ya kuridhika na kitu kimoja tu
ulichosoma badala yake endelea kujinoa na kujiimarisha kila iitwapo leo.
..............................................................
Mazingira hayaruhusu kujifunza; kuna
nyakati utapita na utashangaa kuona kuwa mazingira hayaruhusu, kujifunza, hayaruhusu
kuanzisha biashara, hayaruhusu kufanya kitu ulichojipangia kufanya, nimekuwa
nikipokea changamoto hii kutoka kwa watu wengi sana wakisema kuwa siku hizi
hawasom vitabu mazingira ya nyumbani hayaruhusu, mazingira hayaruhusu kufungua biashara, na vitu vingine kama hivyo. Kwa kweli nyakati kama hizi zipo si unajua siyo
kila siku ni jumapil eeh! Lakini tambua kuwa hakuna siku hata moja mambo
yatakuja yakamilike yote sawa kabisa kwa asilimia 100 kama unavyotaka ili uanze,.
Pengine utasubiri sana kitu kama hicho na wala kisitokee. Lakini pamoja na
mazingira kugoma na kutokuwa kama unavyotaka ndiyo uanze kitu kikubwa hapo ni
kuanza na kile ulicho nacho mengine yatakukuta mbele kwa mbele. Lakini wakati mwingine ukiona mambo yamegoma kabisa
waweza kubadili mazingira na kuendelea na kazi lakini isiwe kiivyo. Pambana hadi
kieleweke inawezekana.
Kwaleo itakuwa vyema kama tukisema itoshe lakini
tutaendelea kujifunza mengi na mazuri ya
kujenga. Na vikwazo hivyo katika kujifunza au kufanya mipango yetu vipo vingi
sana na hivi ni kwa uchache tu zichukue ikawe ni changamoto kwako katika
kujifunza na kuzifanyia kazi. Na kama zipo nyingine usiache kushiriki nasi
kupitia comments hapo chini au tutumie ujume kupitia namba hapo chini, uwe na
wakati mwema asee.
Rafiki, ni matumaini yangu kuwa umejifunza kitu.
na kama unachangamoto katika hili pengine namna gani ya
kuondokana na adha hii sasa waweza kuwasiliana na mimi moja kwa moja kupitia
mawasiliano hapo chini naamini utasaidika.
GeT tO ThE nExT
lEvEl!
Makala hii, imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO ELIAS
Mshauri & Mwalimu Wa Saikolojia, Uchumi na Maisha. Mwanzilishi na
Mwendeshaji wa Mtandao wa addvaluetz. Karibu sana ujiongezee thamani yako.
Kwa mawasiliano;
Whatsapp & Sim >>+255767653697 /+255783327456
Email>> eliasmigongo120@gmail.com.
Facebook>> MIGONGO ELIAS.
LinkedIn>>Migongoe.
Instagram>>migongo_elias.
Pinterest>>eliasmigongo.
Kama umejifunza kitu, niachie maoni yako nitafurahi
kujifunza pamoja nawe.
Sort by: Date Rating Last Activity
Comments by IntenseDebate
Posting anonymously.
Cheyo · 87 weeks ago
Migongo · 87 weeks ago