HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 31
.jpeg)
SIMULIZI
YA KUFURAHISHA, “KUHUSU HATIMA YA KIMUNGU”.
SEHEMU
YA SITA.
Ilipoishia.....
Mungu
nisamehe kwa huu uamuzi lakini no matter what, lazima nimjue aliye na mtoto
wangu na aliyemuua mume wangu. Mungu ni rehemu Kwahaya maamuzi lakini naomba
baraka zako maana siwezi kukaa kimya tena. Mpaka hapa nilipofikia basi inatosha
Mimi kuumia, maana nahisi hata mtoto wangu hawa watu ndio wanajua aliko. Huu
ndiyo mwanzo, nipo tayari kufa, maana Sina cha kupoteza. nisamehe sana ila niruhusu tu mimi nifanye
hivi please..."
Kama hujasoma sehemu iliyopita bonyeza hapa.
Editrin alijiapiza kulipa kisasi kwa wote waliosababisha
familia yake sambaratika. Alionekana kama mtu aliyedhamilia kufanya jambo
fulani ili aweze kutimiza kisasi chake.
Alipotoka kanisani alirudi nyumbani, ambako
alimkuta baba yake kawahi sana kurudi jambo ambalo halikuwa la kawaida kutokea.
Mr. Edward baada ya kumwona Editrin, alionekana kama aliyefurahi kumwona binti
yake karudi salama nyumbani. Alishusha pumzi nzito kisha akasimama na kuanza
kuondoka kuelekea chumbani kwake.
"Baba!"
"Yes Editrin"
"Hauna chochote cha kuniambia?"
"Kama nini?"
"Mbona kama unahofu kuhusu mimi
sikuizi?"
"Unamaana gani?"
"Ok, sawa, kama huna cha kuniambia,
basi mimi ninacho cha kukuambia". Mr. Edward aliahirisha safari yake na
kuja kukaa tena mahali alipokuwa amekaa mwanzo. Editrin naye alisogea karibu na
baba yake kisha akaketi.
"Nataka kutimiza haja yako"
"Ipi?"
Nataka kuolewa, tena mtu ambaye wewe
unataka". Mr. Edward alishituka kidogo kisha naye akauliza
"Ninayemtaka? Nani?"
"Yeyote tu, nimechoka kukaa hapa ndani,
tena kwa wakati kama huu ambao mimi na wewe hatuelewani bora nikaolewe"
"Nipe muda wa kufikiria kuhusu
hilo". Mr. Edward alisimama na kuelekea chumbani kwake akiwa kama
asiyeamini kitu, Editrin katamka kwa mdomo wake.
Usiku huo Mr. Edward aliwaza sana, usingizi
ulipaa na akawaza ni nani ampe binti yake. Kwa upande wa Editrin alikosa
usingizi pia maana aliwaza namna ya kulipiza kisasi maana alihisi kabisa Esau
atakuwa ndiye muhusika wa kifo cha mumewe.
Asubuhi Mr. Edward aliondoka mapema sana
na hakujulikana alikokwenda. Alirudi jioni akiwa na kijana mmoja aliyeitwa
Emiliano. Emiliano alikuwa kijana aliyejulikana sana jijini Dar es salaam kwani
alifahamika kwa namna alivyokuwa tajiri. Emiliano alikuwa ni kijana mdogo sana
aliyemiliki kampuni ya ndege za masafa marefu yaani, kutoka Dar es salaam
kwenda Marekani, China na India. Aliweza kumiliki kampuni hiyo baada ya wazazi
wake kupoteza maisha kwa ajali ya gari. Alikuwa akiishi na mdogo wake aliyeitwa
Emily maana ndiye ndugu pekee aliyekuwa naye, na hakuwahi kuwaza kuoa maana
alipohojiwa na waandishi wa habari alisema sababu kubwa ni kuwa alihofia
kumtelekeza mdogo wake.
Emiliano na Editrin walisoma pamoja
katika shule ya sekondari st. Claudy, na walikuja kutengana baada ya yeye
kwenda kusoma India mara baada ya kumaliza form four.
Editrin alishangaa sana kumuona Emiliano,
na hakujua baba yake kamtoa wapi kijana yule. Hakujua kwanini Emiliano yupo
kwao na wala hakutaka kuuliza. Emiliano alionyesha kufurahia sana kumuona
Editrin.
Baada ya chakula cha jioni Editrin na
Emiliano walipata muda wa kukumbushana vihoja na matukio mbalimbali ya shule.
Emiliano alikuwa kijana mstaarabu sana na mpole mno toka akiwa shule.
Walipiga stori kwa muda mrefu sana mpaka
wakajikuta 'wametoboa ozon' maana ilifika saa 11:30 asubuhi wakiwa bado
subuleni wanachekacheka tu.
Walishituka na kuagana kwa kicheko baada ya kugundua
wamekesha usiku kucha. Kila mmoja alikwenda kulala chumbani kwake na hakuna
aliyeamka mpaka ilipofika saa 9:15 alasiri. Mr. Edward alifurahi kuona binti
yake anafuraha sasa hivyo akaadhimia kumwozesha Editrin kwa Emiliano.
Emiliano alikaa kwao kwa muda wa siku tano
na hakuna aliyejua kwanini yupo pale
zaidi ya Mr. Edward. Baada ya siku tano kupita Editrin aliitwa na kuambiwa kuwa
Emiliano yupo pale kwakuwa alihitaji kumuoa. Alishangaa maana hakujua kama
itakuwa hivi maana adhima yake ilikuwa ni kuolewa na Esau ili aweze kupata
nafasi ya kulipiza kisasi chake. Kwake hili lilikuwa jambo gumu kukubaliana
nalo. Wakati akiwa anasitasita kutoa jibu baba yake alimpa stori fupi kuhusu
Emiliano.
"Emiliano akiwa shule alimpenda sana
Editrin kwakuwa walikuwa wadogo aliona atajiaibisha tu, hivyo hakusema lolote.
Walipomaliza sekondari Emiliano alipelekwa kusoma India na familia yake. Baada
ya kurudi alikwenda kwa Mr. Edward na kumwambia kuwa anampenda Editrin na yupo
tayari kumuoa, lakini alisikitishwa sana na taarifa alizopewa maana Editrin
alikuwa amekwisha olewa na Edwin. Kiukweli alilia sana mbele ya Mr. Edward
lakini Edward akamwambia Editrin kalazimisha ndoa.
Kwakua hakuwa na chakufanya aliamua
kukubali lakini alisema yupo tayari kumsubiria Editrin maana ndiyo binti pekee
anayeweza kuishi na mdogo wake Emily vizuri vinginevyo basi yeye hatoweza kuoa.
Stori hii ilimshangaza sana Editrin. Na
ndipo alipoamua kukubali kuolewa na Emiliano na akaona itakuwa vizuri kama
atamtumia Emiliano kumsaidia kulipiza kisasi chake.
Editrin alimwambia Emiliano kuwa atakuwa
tayari kuolewa naye kama atakuwa tayari kuokoka na kuanza kusali maana alitaka
kufunga ndoa ya kanisani tena kwa heshima sana. Emiliano hakuwa na shida
kabisa, alikwenda jumapili kanisani na kuokoka. Ndoa ikafungwa.
Esau baada ya kusikia zile habari
alichukia mno na akaanza kumsumbua Mr. Edward kwa fujo mbalimbali.
Siku moja baada ya Emiliano kuja
kumtembelea baba mkwe wake alitekwa na Esau na kupigwa sana. Esau baada ya
kumpiga sana Emiliano alisema tu "unabahati mimi siwezi kuua mtu maana leo
ungekuwa mwisho wako" baada ya maneno hayo alimchukua Emiliano na kwenda
kumtupa karibu na ofisi ya Mr. Edward.
Kwanamna
Emiliano alivyokuwa akijulikana watu walimtambuana kumuwahisha hospitali. Baada
ya kupona aliulizwa kuwa ni nani kamfanyia vile, lakini alisema hata yeye
hamjui. Ukweli ni kuwa hakuwa tayari kusema.
Editrin alikaa miaka mingi sana na
Emiliano lakini hakuweza kupata mtoto jambo ambalo lilisababisha kukosekana kwa
furaha ndani ya familia ile.
Siku moja Editrin aliota ndoto na ndani
ya ndoto hiyo alimuona Edwin akimuita huku akisema "huwezi kupotea kama
hivi Editrin, huwezi!". Ndoto ile ilimshangaza sana na ikamkosesha
amani kabisa. Alipomsimulia Emiliano,
Emiliano alionyesha hali ya kukosa amani pia.
Waliishi miaka yote bila mtoto na wakati
huo walikuwa wakiishi na Emily mdogo wake Emiliano. Emily na Editrin walikuwa
wanapendana sana na hawakuwahi kugombana.
Siku moja Editrin akiwa nyumbani pekeyake
baada ya mumewe na Emily kuondoka, alitoka nje ya geti kwaajili ya
kuzungukazunguka nje ya nyumba yao. Ghafla alitaka kutekwa lakini kwa msaada wa
walinzi wa nyumba yao ambao hakuwa mbali naye waliokuwa na silaha waliweza
kumsaidia.
Emiliano alipopata taarifa alirudi
nyumbani haraka sana na alionyesha kuumia kana kwamba yeye ndiye aliyekuwa
kavamiwa.
Baada ya tukio lile kupita Emiliano
aliongeza ulinzi kwa mkewe maana alihofia kuwa Esau ndiyo chanzo cha haya yote.
Editrin aliamua kumsimulia Emiliano kuhusu kifo cha Edwin na kupotea kwa mumewe
na mwisho alisema kuwa anahisi Esau ndiye aliyehusika.
Emiliano alimuuliza Editrin swali
"hivi ukithibitisha kuwa Esau ndiye aliyemuua mume wako
utamfanyaje?".
"Namfunga jela yaani lazima
alipe"
"Kwani huwezi kumsamehe?"
"Hapana siwezi kumwacha kirahisi
hivyo"
"Kwani wewe bado unampenda Edwin au
unanipenda mimi?. Kila siku humu ndani ni Edwin tu, kwani huwezi kumsahau
Edwin?, Basi nenda kamtafute huyo Edwin na mtoto wako". Emiliano aliongea
kwa kufoka hadi Editrin akashangaa.
Baada ya miaka sita kupita Editrin
alipewa taarifa kuwa Esau kafa pia. Tena kafa kwa kuuwawa na watu waliosemekana
kuwa ni majambazi. Kwake taarifa zile zilimvutia maana aliona kama Mungu
kamsaidia kulipa kisasi chake, hivyo alisema "kwakweli malipo ni hapahapa
duniani'.
Aliamua kuanza maisha kwa amani sasa,
aliamua kumsamehe baba yake na kuachilia kila kitu. Wakiwa wanaendelea na
maisha siku moja usiku aligumdua kitu ambacho hakuamini kabisa na kikamfanya
atoroke pale ndani usiku na kukimbia mtaani huku akilia sana.
*
*. *. *.
*. *. *
Elvine
alirudi nyumbani akiwa na hasira sana. Na alipofika nyumbani alikwenda sebuleni
na kukaa sebuleni akiwa na mawazo sana. Ghafla alikuja mdogo wake Elvila na
kumkumbatia akiwa na furaha sana. Kwaasila na uchungu aliokuwa nao alimfokea
mdogo wake na kumwambia hataki usumbufu. Elvine Alishangaa sana naye kwaasila
alizila na kuondoka.
Wakati anajutia kitendo cha kumfokea
Elvila, baba yake alitoka. Elvine baada ya kumuona tu Mr. Ezhu yang alisimama
na kumkunja baba yake kwa kumkaba, huku akihoji "where is my really
mother?(yuko wapi mama yangu wa kweli?).
Mr. Ezhu yang alishangaa sana. Wakati
Elvine akiwa katika hali hiyo ya hasira mama yake Exhao alikuja pale sebuleni
kwakile alichokiona alipiga kelele ambazo ziliwafanya watu watumishi wa mule
ndani kuja kutoa msaada.
Baada ya ugomvi huo kuisha Mr & Mrs
Ezhu yang waliona hakuna haja ya kumficha ukweli Elvine tena maana tayari
Elvine alikuwa na mawazo mabaya juu yao. Walimsimulia ukweli wote pasipo
kumficha jambo. Elvine alilia mno na akasema baada ya kumaliza tu chuo
alihitaji kurudi Tanzania. Wazazi wale waliumia sana maana hawatamani kumwacha
Elvine aondoke lakini hawakuweza kumzuia tena.
Elvine alikwenda kwa rafiki yake Elimina na
kumsimulia kila alichosimuliwa na wazazi wake wale wa kichina. Elimina
alimuuliza kama ataweza kupakumbuka nyumbani kwao siku akirudiTanzania. Elvine
alisema hana uhakika maana tayari ni miaka mingi sana imepita.
Walipomaliza chuo Elvine alimwambia
Elimina kuwa watakwenda wote Tanzania. Elimina alikuwa na uzito kidogo kukubali
maana alihofia pindi akifika Tanzania na Elvine wazazi wake watamuhoji maswali
mengi. Kwahiyo akaanza kumkwepa.
Elvine
aligundua kwanini Elimina anamkwepa maana kila alipokaa naye na kumweleza kuwa
anahitaji waende wote Tanzania. Elimina alikuja na maswali mengi mara utafikia
wapi?, Unakwakufikia?, Unakukumbuka kwenu vizuri?, Kwanini usimwambiye baba yako
Mr. Ezhu yang ndiyo akurudishe alipokutoa?....
Elvine
aliamua kumtumia Elimina vibaya, maana alijua kabisa kuwa Elimina anaifahamu
Iringa vizuri na istoshe walikuwa wakisali kanisa moja. Elvine alianzisha
mazoea sana na Elimina na akaanza kumjali kiasi ambacho Elimina alihisi
anapendwa sana, lakini Elvine alikuwa akiigiza ili tu afike kwa mama yake.
Siku
waliyokuwa wakihitumu chuo kikuu Elvine alimwambia Elimina kuwa anahitaji
kumuoa pindi wakifika Tanzania. Elimina alishangaa sana na akafurahi pia.
Aliamua kutoa taarifa kwao kuwa amepata mchumba na anakwenda naye kwao maana
pia mchumba wake ni mtanzania.
Baba yake
alimshangaa sana na kisha akamuuliza swali kuwa mbona imekuwa mapema sana
kumkubali mtu huyo! Na pia alimwambia asikurupuke amwombe Mungu ili Mungu ndiye
athibitishe hilo jambo lake, lakini Elimina alisema anauhakika na pia Mungu
kasema naye pia kuhusu hilo.
Siku zilifika za wao kuondoka china, Elvine aliwaaga
Mr & Mrs Ezhu yang na Elvila mdogo wake ambaye alikuwa akilia sana maana alimzoea
sana Elvine. Lakini Elvine alimuahidi Elvila kuwa atarudi tena kumchukua waende
wote Tanzania.
Elvine na Elimina waliondoka mpaka Tanzania,
waliposhuka uwanja wa ndege wa Tanzania, walikutana na baba mmoja ambaye naye alionekana
ni mgeni pale. Elvine alimshangaa sana yule baba maana Elimina alimwambia kuwa anafanana
sana na yule baba. Yule baba alishangaa kuona kuna mtu anamtazama sana. Akaamua
kumsogelea yule kijana na kumuuliza sababu ya yeye kumtazama vile. Elvine alimwambia
kuwa anahisi wanafanana sana. Yule baba alicheka sana na akasema "Duniani kuna
Mungu, na ndiye kaumba watu, kwahiyo msemo wa duniani wawili wawili unaweza kuwa
wa kweli".
Yule baba alionekana ni mwenye pesa sana na
alisema kuwa katokea Marekani. Kwa muda mfupi walizoeana na yule baba akawapa lifti
kwenye gari lake maana na yeye alisema anakwenda Iringa kwasababu kuna mtu anaenda
kumtafuta huko. Elimina aliuliza "ni nani?" Yule baba alitabasamu na kusema ni rafiki yangu tu.
Walifika Iringa stendi na ndipo walipoachana,
lakini walipeana namba kwaajili ya mawasiliano zaidi. Elvine alifika nyumbani kwa
kina Elimina na kupokelewa vizuri sana. Elvine alijua kuwa itakuwa nahisi sana kumpata
mama yake akiwa pale kwa mchungaji Moses. Alisubiri jumapili kwa hamu akiwa na . Matarajio
ya kumuona mama yake.
Jumapili ilipofika walikwenda kanisani, muda
wote wa ibada alikuwa akiangaza macho yake kumtafuta mama yake lakini hakujua kuwa
mama yake alikwisha ondoka Iringa muda mrefu sana. Alipoona hajamuona mama yake
aliamua kusema ukweli. Wakiwa katika chakula cha jioni Elvine aliulizwa na baba
yake Elimina kama kweli anamalengo na binti yao.
Elvine alishindwa kujibu na akainamisha kichwa
chini na kutikisa kichwa ikiwa ni ishara ya kukataa. Elimina hakuamini kabisa kinachotokea
pale, Elvine aliwaeleza kuwa alimdanganya Elimina kwasababu alihitaji mtu wakumfikisha
Tanzania. Na akasema alifanya hivyo baada ya kujua kuwa Elimina ni mtoto wa mchungaji
anayelea kanisa ambalo yeye na mama yake walikuwa wakisali, hivyo alihisi itakuwa
rahisi sana yeye kumpata mama yake akiwa kwa kina Elimina maana kutokana na maendeleo
haikuwa rahisi sana kupafahamu kwao.
Elimina alitoka pale sebuleni na kukimbilia
chumbani kwake, ambako huko alilia sana. Mchungaji Moses alimuuliza jina la mama
yake na Elvine akataja kuwa alikuwa akiitwa Editrin. Mchungaji na mkewe walishituka
sana na wakaanza kumuuliza maswali ya mfululizo. "Ulikuwa wapi siku zote hizo?
Nini kilitokea? Ulifikaje China we mtoto? Na mengine mengi.
Baadaye walimueleza namna mama yake alivyochanyikiwa
baada ya yeye kupotea. Na pia walimwambia kuwa mama yake alikuja kumchukua na familia
yake na hawajui taarifa zake maana ni miaka mingi imepita.
Kule chumbani Elimina aliamua kunywa panado na mseto(dawa za malaria)
ambavyo jumla yake vilikuwa ni vidonge 47. Wakati huku subuleni maongezi yakiwa
yanaendea mama Elimina aliona aende chumbani kwa binti yake akamfariji, lakini oooh!!
Hakuamini kabisa alichokiona baada ya kuingia chumbani....
Sehemu ya sita itaendelea jumatatu
>>>>>. Usikose kufuatilia.
Kupata mwendelezo wake bofya hapa.
Hadithi hii imendaliwa na kuandikwa
na JACQUELINE
JOHN.
Mwimbaji na mtunzi wa nyimbo,
mashairi, Hadithi (simulizi) na ngonjera.
Mawasiliano:
Whatsapno.
>>>>> +255789523850. Normal >>>>>+255747313148.
Hadithi hii Imehaririwa na MIGONGO
ELIAS. Mhariri.
Mawasiliano:
Whatsapno.
>>>>> +255767653697. Normal >>>>>+255783327456.
GeT tO tHe NeXt LeVeL!
Kama
umejifunza kitu shiriki nasi katika comment hapo chini, ili kujifunza na
kuboresha zaidi.