KUISHI KUTOKEA NDANI: NGUVU YA KUJISIKILIZA WEWE MWENYEWE.


 KUISHI KUTOKEA NDANI: NGUVU YA KUJISIKILIZA WEWE MWENYEWE.


Mara nyingi sana nimegundua na kuona kwamba, maisha yetu huendeshwa na kelele za nje kuliko sauti ya ndani yetu.
Hebu fikiria, jamii inaongea, watu wanashauri, mitandao inaonyesha kila aina ya maisha pengine yaliyo bora kuliko yako, na mazingira yanatupangia namna ya kufikiri na kuishi.

Sasa hapo unajua nini kinatokea boss? Polepole bila hata kugundua, tunaanza kuishi maisha ambayo si yetu kabisa.
Tunafanya maamuzi kwa sababu: “Watu wataonaje?”, “Jamii inasema hivi”
“Hivi ndivyo wengine wanafanya” yaani mamjo lukuki.
Na hapo ndipo wengi wanapopoteza mwelekeo wao halisi kabisa.

Unajua nini boss wangu? : KUISHI KWA SAUTI ZA NJE Siyo shida sema tu kwamba;

Dunia ya leo imejaa kelele nyingi sana vitu kama:
Mitandao ya kijamii, marafiki na ndugu, Mila na desturi, Shinikizo la kufanana na wengine yaani vitu kedekede boss.

Na hii imepelekea watu wengi wameacha:
Uwezo wao wa kufikiri, Ubunifu wao, Maamuzi yao, hata hatima zao na maisha yao kwa ujumla.
Wameamua kuishi maisha ya kuiga, siyo maisha ya ndani yao hapa ndo tatizo lilipo ndugu angu.

๐Ÿ‘‰ Wanajaribu kufanana na dunia, badala ya kuwa wao wenyewe.

UKWELI USIOUJUA NI KWAMBA, NDANI YAKO KUNA MWONGOZO WA MAISHA YAKO YOTE. Yaani, namaaniaha kuwa ndani ya kila mtu kuna sauti.
Hii ni Sauti ya ndani. Wengine huiita intuition.
Hii siyo sauti ya kawaida ni mwongozo wa ndani unaokuambia: Hii ni sahihi, hii siyo sahihi, hapa endelea, aimama, hapa badilisha mwelekeo..

Na mara nyingi: ๐Ÿ‘‰ Inakuonya kabla hujaingia kwenye kosa.
๐Ÿ‘‰ Inakuongoza kabla hujapotea. Hebu kumbuka hata siku unatapeliwa kunasauti ilikuwainakukataza usifanye hivyo.

Ndugu yangu sauti hii, Inakupa amani unapochagua sahihi, lakini shida ni moja tu
Watu wengi hawaijali kabisa na wanaichukulia poa sana.

HAPA NAPATA KUJIULIZA HIVI KWANINI WATU HAWAJISIKILIZI?
Najua unasababu kibao, lakini sababu ni waanahofia kukataliwa,
Wanataka kufanana na wengine,
Wamezoea kuamini nje kuliko ndani,
Hawajawahi kujifunza kujitambua.
Hivyo wanapuuza ile sauti ndogo ya ndani, na kufuata kelele kubwa za nje hapo ndo kilio huanziq boss.

Kwani, mwisho wake wanaishia;
Maisha yenye majuto,
Maamuzi yasiyo sahihi,
๐Ÿ‘‰ Kukosa amani ya ndani,

KINYUME NA HAPO, KUNANGUVU YA KUISHI KUTOKEA NDANI, kwani;
Unapoanza kujisikiliza kutoka ndani:
Unaanza kufanya maamuzi sahihi kwa maisha yako,
Unapata amani hata katikati ya changamoto,
Unajitambua kwa kina,
Unajenga maisha yenye mwelekeo na maana.

๐Ÿ‘‰ Hapa ndipo maisha halisi yanaanza.
Maisha ya: Uhuru, Uhakika, Furaha
Na utimilifu.

JINSI YA KUANZA KUJISIKILIZA NDANI YAKO
1. Punguza kelele za nje
Punguza muda wa mitandao
Epuka watu wanaokuchanganya
Tafuta muda wa kuwa peke yako boss wangu.

2. Jifunze kuwa kimya
Wakati mwingine majibu hayaji kwa kelele
Yanakuja kwenye utulivu.
3. Jiulize maswali sahihi
Hii ninayotaka kufanya, inanijenga au inaniharibu?
Hii ni mimi kweli au naiga tu?

4. Amini hisia zako
Usipuuze ile feeling ya ndani.
Mara nyingi huwa sahihi kuliko unavyofikiri.

Kwa kumaliziq ndugu yangu,
huwezi kuishi maisha yenye maana kama hujajifunza kujisikiliza wewe mwenyewe.
Dunia itaendelea kupiga kelele.
Lakini maisha yako yataamuliwa na sauti unayoamua kufuata.
๐Ÿ‘‰ Je, utafuata kelele za nje.
AU
utafuata sauti ya ndani inayokuongoza?


Hebu Leo chukua dakika 10 tu:
Kaa kimya
Jiulize maswali ya ndani
Sikiliza moyo wako
๐Ÿ‘‰ Anza kuishi maisha yako. siyo ya watu wengine.

Share na mimi kupitia comment ulichojifunza. Ikiwezekana share na wengine ujumbe huu ili wajifunze pia.

Kujifunza tembelea,
https://addvaluetz.blogspot.com/2026/04/level-za-mafqnikio-sehemu-ya-pili.html

#SelfAwareness (#Kujitambua). #Investment (#Uwekezaji). #PersonalDevelopment (#Maendeleobinafsi). #MigongoElias. #AddValueNetwork. #SeeYouNextLevel
+255767653697.

Popular posts from this blog

UKIJUA HILI KUHUSU WATU UTAFANIKIWA SANA.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29