LEVEL ZA MAFANIKIO SEHEMU YA NNE

 


LEVEL ZA MAFANIKIO SEHEMU YA NNE.


Baada ya kufika hatua ya Business Owner level kama tulivyoangalia sehemu ya tatu.
Watu wengi huendelea kubaki palepale kwa kufanya biashara maisha yao yote.
Lakini wachache sana hupiga hatua na kujiuliza swali hili muhimu:
“Nawezaje kufanya pesa zangu zifanye kazi badala yangu yaani zinifanyie kazi?”
Na hapo ndipo inakuwa ni ticket ya kupanda kwenda hatua inayofuata:
INVESTOR LEVEL (PESA ZINAFANYA KAZI KWA AJILI YAKO).
HII NI LEVEL YA KUBADILI MCHEZO mzima boss wangu.
Hapa hutegemei tena: muda wako, nguvu zako wala uwepo wako.
πŸ‘‰ Unategemea: MTAJI WAKO na MAARIFA YAKO boss.
MAANA HALISI YA HII LEVEL
Investor siyo tu mtu mwenye pesa ndugu angu.
πŸ‘‰ Ni mtu anayejua:
wapi pa kuweka pesa, lini aweke, kwa nini aweke
na namna ya kupunguza hatari za uwekezaji.
BOSS TOFAUTI KUBWA NA LEVEL ZILIZOPITA NI KWAMBA,
Kwenye Slavery mode → unafanya kazi ya mtu kwa pesa boss.
Self-employed → unafanya kazi yako mwenyewe ili upata pesa.
Business owner → watu wanafanya kazi kwako huku unafaidika wewe.
Investor → hapa boss unazituma pesa zinafanya kazi kwa ajili yako.
MFANO RAHISI WA KUELEWA
Badala ya: πŸ‘‰ kufungua biashara wewe mwenyewe
Unaweza: πŸ‘‰ kuwekeza kwenye biashara ya mtu mwingine, anakuwa anaoalangane wewe unapata faida huku unafanya mambo yako boss.
πŸ‘‰ Kitu kingine unaweza fanya ni kununua hisa boss
πŸ‘‰ kuwekeza kwenye assets zinazoingiza kipato
Na ukaendelea kupata mapato bila kufanya kazi ya moja kwa moja boss.

NGUVU KUBWA YA HII LEVEL ni kitu kinaitwa,
PASSIVE INCOME
πŸ‘‰ Unapata kipato:
hata ukiwa umelala, hata ukiwa safarini,
hata usipofanya kazi hata ukiwa unakata mitaa. Inshort unakuwa ni free katika muda, pesa na uwepo boss.

AINA ZA UWEKEZAJI KATIKA LEVEL HII
Boss katika level hii haiji tu hivi hivi kunatargeted areas za kuwekeza na kukuletea matokeo tarajiwa, Unaweza kuwekeza kwenye:
Biashara (equity), Hisa (stocks),
Ardhi na majengo (real estate),
Miradi mbalimbali yenye tija,
Mitandao ya kidigital (online assets) boss.

NDUGU YANGU UZURI WA LEVEL HII.
1. UHURU WA KWELI WA MUDA WAKO.
Hufungwi tena na kazi ya kila siku hapa utaamua wewe matumizi ya muda wako boss. Kwani unakuwa hufungwi na muda tena.

2. UTAJIRI UNAWEZA KUKUA HARAKA
Kwa sababu pesa zinaongezeka juu ya pesa (compounding) kuna nguvu kubwa ya compound effect boss ujue.

3. RISK INAGAWANYWA.
Unaweza kuwekeza sehemu tofauti tofauti.
Yaani unatawanya uwekezaji wako sehemu tofauti tofauti. Difastification.

NDUGU CHANGAMOTO KUBWA ZA LEVEL HII
Hapa ndipo wengi wanapoteza pesa kama hawana uelewa:
1. KUKOSA ELIMU YA UWEKEZAJI.
Boss kila siku naimba hiki kitu maarifa is the key, huwezi kuwa zaidi ya ufahamu wako boss.
πŸ‘‰ Bila maarifa, uwekezaji unakuwa kamari.

2. TAMAA YA FAIDA YA HARAKA.
Hili ni janga kubwa wengi hutamani get rich quick money.

πŸ‘‰ Hii ndiyo chanzo kikubwa cha kupoteza pesa boss.

3. KUTOKULINDA MTAJI
πŸ‘‰ Wengi wanakimbilia faida na kusahau usalama wa pesa zao. Safety first.
KANUNI MUHIMU SANA YA LEVEL HII
LINDA MTAJI WAKO KWANZA  FAIDA ITAFUATA baadae boss wangu.
Hii ndiyo sheria kuu ya investor yeyote makini, tajiri mwenzangu.

MBINU YA KUSHINDA KATIKA LEVEL HII.
Watu wengi hukosa uelewa na kushindwa kufanya mambo yanayotakiwa na mwishowe hubaki hapa hapa au kurudi nyuma. Sasa fanya haya ili usiwe mmoja wao.

1. JIFUNZE KABLA YA KUWEKEZA.
Usiweke pesa kwenye kitu usichokielewa.
Dangote alisema, before you start any business you must understand it full, yaani, in and out. Hii ni siri na kupa boss ya kubaki the yop.

2. ANZA NDOGO, JIFUNZE ZAIDI.
Usianze na pesa nyingi bila uzoefu.
Anza kidogo ili kuusoma mchezo, ramani na kupata uzoefu. Ndipo uweke nguvu yote ukishaelewa in and out.
3. GAWA HATARI (DIVERSIFICATION).
Hii tushazungumza sana boss wangu, inshort
Usiweke pesa zote sehemu moja tajiri, utalia.

4. KUWA NA UVUMILIVU
Uwekezaji siyo wa haraka ni wa muda mrefu.
Muda ni kitu cha thamani sana katika uwekezaji. Watu wengi kabla ya kufika hapo walipo waliwezeza walau miaka mi5 , 10, 15 , n.k hadi ikawalipa boss. Ko kama wewe unataka ma ya chap chap, huku hutaki hata kuwekeza katika maarifa, vitendo na nidhamu itakukost. Make sure tu ni kwamba kitu unachikifanya ni road map yako ishu ya matokeo uachie muda boss.

KOSA KUBWA SANA WATU WANALOFANYA
πŸ‘‰ Wanataka kuja level hii bila kupitia hatua zilizopita kule mwanzo.
Matokeo: wanatapeliwa vibaya mno,
wanapoteza pesa,  wanarudi chini tena ndo shida yake hiyo.

UKWELI WA WAZI BOSS
Itoshe kusema huwezi kuwa investor mzuri bila kuwa na msingi mzuri.

To conclude boss ni kwamba,
Hii ndiyo hatua ambayo:
πŸ‘‰ pesa zinaanza kuwa tool, zinakutumikia wewe
πŸ‘‰ muda wako unakuwa huru,
πŸ‘‰ utajiri unaanza kuwa mfumo wako boss.
Lakini kumbuka:
Investor wa kweli sio anayepata pesa nyingi  ni anayelinda na kukuza alizonazo. Hapa ndo nikijua kuwa unaweza kupata 100M/month lakini ukawa maskini mzuri tu.

UJUMBE WA MWISHO KWAKO BOSS.
“Usifanye kazi kwa pesa maisha yako yote jifunze kufanya pesa zikufanyie kazi.” chukua hii boss.

Share na mimi kupitia comment ulichojifunza. Ikiwezekana share na wengine ujumbe huu ili wajifunze pia.

Kujifunza tembelea,
https://addvaluetz.blogspot.com/2026/05/mambo-muhimu-ya-kuzingatia-kabla-ya.html

#SelfAwareness (#Kujitambua). #Investment (#Uwekezaji). #PersonalDevelopment (#Maendeleobinafsi). #MigongoElias. #AddValueNetwork. #SeeYouNextLevel
+255767653697. 

Popular posts from this blog

UKIJUA HILI KUHUSU WATU UTAFANIKIWA SANA.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29