Posts

Showing posts from July, 2023

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29

Image
  Nashukuru kwa kushiriki nami link ya Hadithi hii tamu na Nzuri ya Hatima ya Kimungu Sehemu ya 29. 🙏 Nilichosoma katika sehemu hii, simulizi imeendelea  kwa mvuto mkubwa sana – linaonyesha mapambano ya ndani ya Elvine kati ya imani yake, hofu yakuwaza kumpoteza mkewe Elimina, na hatia ya makosa ya zamani. Kuna mambo yafuatayo nimeona  yaliyobeba msingi   wa  sehemu hii: 1. Mgongano wa nafsi ya Elvine 👉Anapokuwa mbele ya Malaika Elvila, anatakiwa kufanya maamuzi magumu: kati ya mke na mtoto. 👉Uamuzi wake unaonyesha upungufu wa mwanadamu, uchungu, na jinsi maumivu yanavyoweza kuathiri fikra na maamuzi. 2. Adhabu na Neema 👉Kupotea kwa mtoto na kutozaa tena kwa Elimina ni matokeo ya makosa ya Elvine, lakini bado neema ya Mungu inaonekana kwa kumrejesha mkewe. 👉Malaika anamkumbusha kuwa Mungu si mkatili, bali anamfundisha kupitia mateso na changamoto. 3. Ugeuzi wa Maisha (Turning Point) 👉Elvine sasa anaitwa kuwa mchungaji wa kondoo wa Bwana, ishara ...

SIMULIZI YA KUFURAHISHA, “KUHUSU HATIMA YA KIMUNGU”. SEHEMU YA KUMI NA MOJA.

Image
   SIMULIZI YA KUFURAHISHA,   “KUHUSU HATIMA YA KIMUNGU”. SEHEMU YA KUMI NA MOJA.   Ilipoishia....           Wakiwa pale ghafla mlango ulifunguliwa na aliyeingia alikuwa ni Emiliano. Editrin hakutarajia kwasababu Emiliano siku hiyo hakuja na gari  k ama siku zote hivyo walijisahau. Na pia walinzi hawakumzuia Emiliano kuingia kwakuwa walikuwa wakijua kuwa Emiliano ni mkwe wa ile familia na hawakuambiwa chochote kuhusu kutoroka kwa Editrin kwa mume wake.           "Editrin mke wangu" Emiliano aliita na wakati Editrin kashangaa pale. Emiliano akimkimbilia na kumkumbatia. Huku alionesha kufurahi sana kumuona Kupata sehemu ya kumi bofya hapa         Inaendelea......        "Editrin nisamehe kwa kila kitu lakini kumbuka kuwa mimi bado ni mumeo huwezi kunitelekeza kama hivi nakuomba sana nipo chini ya miguu yako rudi nyumbani" Emiliano aliongea huku a...

JIFUNZE KUJIFUNZA PART IV.

Image
JIFUNZE KUJIFUNZA PART IV. JINSI AKILI YA BINADAMU UNAVYOWEZA KUIAMURU. “The greatest revolution in our generation is the discovery that human beings by changing the inner attitudes of their minds can change the outer aspects of their lives”. Maneno haya aliwahi kusema mwanasaikolojia maarufu nchini marekani Willium James. Akimaanisha kwamba mageuzi makubwa katika kizazi chetu ni kugundua kuwa kwa kubadili mtazamo wa ndani ya akili zetu, tunaweza kubadili mitazamo yetu ya maisha ya nje. Tupo katika mfululizo wa somo letu pendwa la JIFUNZE KUJIFUNZA na hii ikiwa ni part iv , kama utakuwa unafuatilia tumejifunza mengi huko nyuma, ikiwemo consicious, sub- conscious mind na mengine kibao. Na kama hujasoma kabisa, nikushauri usome tena kwa makini itakusaidia sana asee. Na, ikiwezekana umwalike na kumshirikisha jirani yako. Kusoma part iii bonyeza hapa Sasa leo tuna kwenda kujifunza ni kwa namna gani mtu anaweza kuiamuru akili yake kufanya chochote anacho kitaka, iwe ni maneno mazu...

SIMULIZI YA KUFURAHISHA, “KUHUSU HATIMA YA KIMUNGU”. SEHEMU YA KUMI.

Image
  SIMULIZI YA KUFURAHISHA,   “KUHUSU HATIMA YA KIMUNGU”. SEHEMU YA KUMI.   Ilipoishia....   Ile nyumba haikuwa mbali na barabara hivyo akafika barabarani lakini kwa yale maumivu aliyokuwa nayo hakuweza kukimbia zaidi, alidondoka katikati ya barabara, akiwa pale alisikia sauti ya mama mmoja kwambali sana ikimwambia       "Kijana wangu nini shida amka! Nini kimekukuta? Haa! Mungu wangu. Mwanasheria!! hebu tumbebe huyu tumuwahishe hospitali kwanza, maana nahisi kavamiwa na vibaka wa mji wetu huu...."           kusoma sehemu ya tisa bonyeza hapa Sasa inaendelea....       Elvine alipoteza fahamu kwa muda, alipoamka alijikuta yupo hospitali na pembeni yake alimuona mama yake Editrin. Hakuamini kwa haraka kuwa yule ni mama yake maana alihisi anaota ndoto ya mchana. Alitulia kwa muda kidogo akiwa anamtazama mama yake pasipo kuongea chochote bali ni machozi tu ndiyo yaliyokuwa yakiongea kwa kuti...

SIMULIZI YA KUFURAHISHA KUHUSU "HATIMA YA KIMUNGU”. SEHEMU YA TISA.

Image
SIMULIZI YA KUFURAHISHA,   “KUHUSU HATIMA YA KIMUNGU”. SEHEMU YA TISA.     Ilipoishia...   "Mawazo unayoyawaza wewe, sio Bwana anavyokuwazia wewe" Elvila alisema huku kamkazia macho Elvine Niambie basi unamaana gani, Elvine alipiga magoti na kuanza kulia. kusoma sehemu iliyopita bonyeza hapa   Sasa inaendelea....   Elvine alilia na kutia huruma sana. Elvila akamwambia kulia sio suluhisho cha kufanya ni kujitahidi tu kujitambua yeye ni nani kwa Mungu na anatakiwa kufanya nini hiyo ndi y o njia pekee ya kusamehewa. Elvine aliposikia hivyo aliahidi kuwa hatakuwa m kaid i tena na ata yaf ua ta maelekezo yote atakayopewa, ila alihitaji kumuona mama yake kwanza.      Elvila hakujibu chochote bali alipotea ghafla k ama upepo. Elvine alishituka maana hakuelewa sehemu ambayo Elvila kapotelea. Elvine alikaa kitandani kwa muda huku akiwaza cha kufanya. Ilipofika jioni alitoka nje na kuanza kufanya kazi ya kutembelea nyumba za jira...

Popular posts from this blog

MAAJABU YA AKIBA

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29