KWANINI NI NGUMU KUGUNDUA KUSUDI LA MAISHA YAKO?
KWANINI NI NGUMU KUGUNDUA KUSUDI LA MAISHA YAKO?
Kuna vitu vinavyoleta furaha hapa duniani.
Kula chakula unachokipenda…
Kuwa na muda na watu unaowapenda(familiy, friends ect)
Kufanya kazi unayoifurahia.
Lakini zaidi ya vyote, kuna furaha ya kipekee sana, ambayo ni:
๐ kugundua na kuliishi #KUSUDI la maisha yako.
Hata hivyo, ukweli mchungu ni huu,
watu wengi bado hawajui sababu ya wao kuwepo hapa duniani.
Ukijiuliza swali hili: “Kwanini nipo hapa duniani?”
hili ni moja ya maswali magumu zaidi, lakini pia ni muhimu zaidi. Mbaya zaidi, Wengi hulikwepa.
Lakini haliachi kuwatesa KIMYA KIMYA.
Kwa nini basi ni ngumu kulijua kusudi lako?
1. KUIGA MAISHA YA WENGINE
Jamii imejenga mfumo wa kufanana. Watu wanashinikizwa kusoma walichochaguliwa pengine na wazazi, kufanya kazi zilizopendekezwa, na kuishi maisha yanayokubalika na jamii.
Matokeo yake,
๐ Wanaacha kusikiliza #SAUTI ya NDANI ya #MIOYO yao. Hili ni kosa kubwa.
2. USUMBUFU WA MAISHA
Maisha yana kelele nyingi. Mitandao ya kijamii, majukumu, kazi, shinikizo la jamii na watu wa karibu. Mtu anakosa muda wa kutulia na kujitafakari.
Ni kama mtoto aliyetumwa dukani kununua chumvi, lakini akakuta wenzake wanacheza mpira, anaishia kusahau kabisa alichotumwa.
Hivyo ndivyo wengi wanavyopoteza mwelekeo wa maisha yao.
3. KUTOKUJIJUA
Watu wengi hawajijui wao kama wao: yaani,
Hawajui wanachopenda, hawajui nguvu zao, hawajui udhaifu wao, hawajui thamani zao.
๐ Bila kujijua, huwezi kujua kusudi lako.
4. HOFU YA KUSHINDWA
Kugundua kusudi si jambo la siku moja.
Ni mchakato wa kujaribu, kushindwa, kujifunza, na kujaribu tena.
Lakini wengi wanaogopa kujaribu kwababu wanaogopa kushindwa.Wanaogopa kuonekana hawajui wanachofanya.
๐ Na kwa hofu hiyo, wanaishia kutofanya chochote.
5. UGUMU WA MAISHA
Wakati mwingine kusudi lako halikulipi mara moja.
Lakini mahitaji yapo: chakula, kodi, nguo, maisha.
Hivyo mtu analazimika kufanya kazi asiyoipenda,
na kuahirisha ndoto yake “kwa muda”.
๐ Lakini huo muda mara nyingi hugeuka kuwa maisha yote.
6. KUAMINI KUSUDI LAZIMA LIWE KUBWA SANA
Watu wengi hudhani kusudi ni lazima liwe dude kubwa sanaaaa.
kama kuokoa dunia au kuwa maarufu kupita kiasi, kuwa tajiri saaana,
Lakini ukweli ni huu:
๐ Kusudi si ukubwa wa jina, bali ni ATHARI(IMPACT) unayoleta kwa wengine.
7. KUKOSA MISINGI YA MAISHA (VALUES)
Bila misingi, mtu hana dira na mwelekeo wowote.
Hajui nini ni sahihi kwake na nini siyo.
๐ Misingi ndiyo inayoongoza MAAMUZI yako,
na hatimaye inakupeleka kwenye KUSUDI lako.
8. KUDHANI KUSUDI NI LA SIKU MOJA
Watu wanataka majibu ya haraka. Lakini kusudi haliji ghafla. Ni mchakato unaohitaji:
muda, uvumilivu, kujitafakari na ujasiri wa Kujaribu
SASA BASI
Habari njema ni hii:
๐ Kusudi lako lipo. Halihitajikutengenezwa lipo tayari ndani yako toka unazaliwa.
Unachotakiwa kufanya ni:
Kujitenga na kelele za dunia.
Kujijua kwa undani.
Kusikiliza moyo wako.
Na kuwa na ujasiri wa kuanza.
Kwa sababu mwisho wa siku.
maisha yenye maana hayatoki nje yanaanzia ndani yako.
Je umejifunza chochote? Share na sisi, ikiwezekana ongezea sababu zingine na wewe tuendelee kujifunza
ujifunza zaidi tembelea
https://addvaluetz.blogspot.com
#SelfAwareness (#Kujitambua). #Investment (#Uwekezaji). #PersonalDevelopment (#Maendeleobinafsi). #MigongoElias. #zAddValueNetwork. #SeeYouNextLevel
+255767653697
