MAENEO 6 YA UWEKEZAJI YATAKAYOONGEZA THAMANI YAKO.

 


MAENEO 6 YA UWEKEZAJI YATAKAYOONGEZA THAMANI YAKO.


Watu wengi wanaposikia neno UWEKEZAJI, mara nyingi akili zao hukimbilia fedha, mashamba, mifugo, hisa, majengo, ardhi n.k. Hii siyo MAKOSA, lakini ni sehemu ndogo tu ya UKWELI.

Sasa hebu nikuulize swali rahisi tu hapa:
Nikikupa milioni moja(1M) leo, utawekeza wapi?

Majibu ya wengi yanafanana. Lakini, leo nataka nikufungulie mtazamo wa juu zaidi  uwekezaji ambao ukikosea hapa, hata uwe na fedha kiasi gani, bado unaweza KUKWAMA sehemu.

Haya ndiyo maeneo 6 ya msingi ya uwekezaji wa kweli unaopaswa kuzingatia:

1. WEKEZA KWENYE UJUZI (SKILLS)

Huu ndio uwekezaji usiopotea.
Unaweza:
Kupoteza kazi, Kuibiwa mali, Kuhama nchi
Lakini huwezi kupoteza ujuzi wako.

๐Ÿ‘‰ Ujuzi ni kama mashine ya kuchapisha pesa ndani ya akili yako.
Watu wengi wanafikiri wanaajiriwa kwa sababu ya kazi wanayofanya si kweli.

Unalipwa kwasababu ya  THAMANI unayotoa.
Na thamani = ujuzi boss.

Hebu fikria:
Ni rahisi mtu kutumia saa 5 mitandaoni akuzurula tu,  lakini akakosa walau dakika 30 za kujifunza kitu kipya.

Jiulize mwenyewe leo:
Ni ujuzi gani nikijifunza au kuuboresha mwaka huu, utaibadilisha kabisa story ya maisha yangu?

2. WEKEZA KWENYE ROHO YAKO (SPIRITUAL FOUNDATION).

Maisha huanzia ndani kabla hayajaonekana nje.
Wewe si mwili tu wewe ni roho, unanafsi na unaishi ndani ya mwili.
Kila kitu unachokiona leo:
mafanikio, kushindwa, mwelekeo wa maisha
Vilianza rohoni.
๐Ÿ‘‰ Kama msingi huu ni dhaifu, hata mafanikio yako yatakuwa na mashaka ndugu.

Njia rahisi za kuwekeza hapa:
Kusoma na kuishi Neno la Mungu, kugunga na kuomba, kutenda mema, kujenga maadili.

Katika hili jiulize:
Nifanye nini leo kuimarisha maisha yangu ya rohoni?

3. WEKEZA KWENYE AFYA YAKO
Watu wengi wanajua hili, lakini wengi wao hawalifanyi.
Goja nikwambia boss, unaweza kuwa na:
ndoto kubwa, idea nzuri.
Lakini bila nguvu (energy) na afya, hakuna utekelezaji hapo niamini mimi.
๐Ÿ‘‰ Ukweli: Afya yako ndiyo msingi wa mafanikio yako yote.

Kila eneo kila mtu anahitaji nishati (energy), wanasiasa, walimu, wanafunzi, wanasheria, wachoraji n.k

Bila afya njema: hutafurahia mafanikio utakayoyapata wala, hutakuwa na nguvu ya kuyasimamia na wakati mwingine unaweza usione hata maana ya kufanikiwa kwako kama afya yako uliibwaga.

Chakufanya: Fanya mazoezi, kula chakula bora
, Lala vizuri, badala ya kunywa soda sana, kunywa maji mengi,  Punguza junk food kula natural.
Waingeleza husema  Health is wealth.

4. WEKEZA KWENYE MTANDAO WAKO (NETWORK)
Maisha yako yanaakisi watu unaokaa nao.
๐Ÿ‘‰ Ukikaa na:
walalamikaji → utakuwa mlalamikaji
wazembe → utakuwa mzembe
wachapakazi → utainuka
Nakumbuka mentor wangu aliwahi kunambia, ukizungukwa na walalamikaji wa5 mlalamikajibwa 6 anakuja hivipunde.

Ndugu yangu, exposure huja kupitia watu.
Fursa nyingi: haziji moja kwa moja
zinakuja kupitia watu. Watu, watu watu.

Jiulize: Nani ananijenga?
Nani ananivuta chini?
Nani ninahitaji kumuongeza kwenye maisha yangu?
Nani naweza kupunguza muda naye?
Wekeza kwenye NETWORK inayokujenga, inayokusapot, kukushauri, kukuhamasisha, kukuaminisha kuwa unaweza.


5. WEKEZA KWENYE MUDA(TIME).

Kila mtu ana saa 24.
Hakuna tajiri au maskini mwenye muda zaidi.
Tofauti ni moja tu: ๐Ÿ‘‰ Namna ya kutumia muda.
Muda ni rasilimali: adimu isiyorudi baada ya kutumiwa.
Ni rasilimali yenye hamani kubwa kuliko pesa.
๐Ÿ‘‰ Unavyoutumia leo muda wako  ndiyo itakayo amua maisha yako ya kesho yatakavyokuwa.

Wekeza muda wako kwenye:
kujifunza,
kusoma,
kujitathmini,
kujenga maisha bora yako ya kesho.

6. WEKEZA KWENYE AKILI NA MTAZAMO (MINDSET)

Hapa ndipo kila kitu kinaanzia.
Kuna sababu kwanini kitabu cha Think and Grow Rich hakijasema: “Fanya kazi kwa nguvu uwe tajiri”
Badala yake kinasema: “Fikiri uwe tajiri.”
๐Ÿ‘‰ Kwa nini?
Kwa sababu: Kila mafanikio huanza kwenye fikra.
Unachofikiria, Unachoamini, Unachokubali.
๐Ÿ‘‰ Ndicho unachokifanya kuwa halisi.
Yaani, whatevee your mind can conceibe and believe can archieve it.
Ndugu ukweli ni kwamba hauwezi kufanikiwa zaidi ya fikra zako. Shuurika na hili kwanza.

Mtazamo wako unaathiriwa sana na mazingira yako:
watu unaokaa nao,
vitu unavyosoma,
vitu unavyosikiliza.

Mfano watu wawili wanaweza kupata changamoto moja: Mmoja atalalamika na kuanza kusema kwanini mimi
Mwingine anatafuta suluhisho, ma kusema hili linanifundisha nini, au ni kitu gani naweza kujifunza katika hili?.

Tofauti ya watu hao  ni  Mindset.


KUMALIZIA NI KWAMBA
Uwekezaji siyo fedha tu.
Ni; nani unakuwa,
unachojenga ndani yako,
namna unavyoishi kila siku.  Hii ni muhimu zaidi na hii, haimaanishi pesa tusiwekeze no no no ooooooo. Usinielewe vibaya.

๐Ÿ‘‰ Lakini, ukiweka nguvu zako kwenye maeneo haya 6: Thamani yako itaongezekana na pesa zitakufuata.

SWALI LA KUKUMBUKA (CHALLENGE)
Leo ukiangalia maisha yako ni eneo gani kati ya haya 6 umelipuuza zaidi? Umejipangaje kubadilika na utaanza lini?

Anza hapo. Na hapo ndipo breakthrough yako ipo.

Share na na mimi kupitia comment. Ikiwezekana share na wengine ujumbe huu ili wajifunze.

#SelfAwareness (#Kujitambua). #Investment (#Uwekezaji). #PersonalDevelopment (#Maendeleobinafsi). #MigongoElias. #AddValueNetwork. #SeeYouNextLevel
+255767653697

Popular posts from this blog

UKIJUA HILI KUHUSU WATU UTAFANIKIWA SANA.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.