KAMA UNASAHAU MARA KWA MARA, SOMA HAPA KWANZA.

Image
  KAMA UNASAHAU MARA KWA MARA, SOMA HAPA KWANZA. Boss! Siyo  kila mara, kusahau ni ishara ya Ubongo dhaifu, mara nyingi ni namna tunavyojifunza ndugu. Nimekutana na watu wengi wakisema: "Mimi sina akili kubwa." Wengine "Kumbukumbu yangu ni mbaya." Mara "Ubongo wangu hauhifadhi vitu." Lakini ukweli ni kwamba, mara nyingi tatizo si ukubwa wa akili yako wala uwezo wa ubongo wako. Tatizo ni kwamba watu wengi hawajawahi kufundishwa jinsi kumbukumbu (memory) inavyofanya kazi boss. Sikia ndugu; Ubongo wa binadamu umeumbwa kwa ustadi mkubwa. Kazi yake si kuhifadhi kila kitu unachokiona au kukisikia, bali ni kuchagua filtering taarifa muhimu na kuacha zisizo muhimu wala matumizi. Kwa hiyo, kusahau si kasoro ya ubongo ni sehemu ya kawaida ya jinsi unavyofanya kazi. Hebu tuangalie sababu kuu zinazowafanya watu kusahau mara kwa mara. 1. Kukariri Bila Kuelewa (memorising without understanding). Hili ndilo kosa kubwa zaidi ambalo wanafunzi na hata watu wazima...

MISINGI YA UWEKEZAJI: KWANINI WENGINE WANASHINDA NA WENGINE WANAPOTEZA PESA?

 


MISINGI YA UWEKEZAJI: KWA NINI WENGINE WANASHINDA NA WENGINE WANAPOTEZA PESA?
Dunia inaendeshwa kwa kanuni zisizobadilika
Na moja ya kanuni kuu inayotawala maisha ya binadamu ni KANUNI YA UWEKEZAJI.
Ukweli mchungu ni huu:
πŸ‘‰ Dunia haikupi unachotaka. Bali, Inakupa kile ulichowekeza.
Ni sawa kabisa na ile kanuni ya asili:
“Apandacho mtu, ndicho atakachovuna.”
Ukichagua kupanda maarifa — utavuna ujuzi.
Ukichagua kupanda nidhamu — utavuna mafanikio.
Ukichagua kupanda fedha kwa hekima — utavuna uhuru wa kifedha.
Lakini…
πŸ‘‰ Ukipanda tamaa, uzembe, au kukurupuka — utavuna hasara.
Kuna UCHUNGU mkubwa kwenye uwekezaji
Katika eneo la fedha, maumivu ni makubwa zaidi.
Watu wengi:
Wamepoteza mitaji yao, wametapeliwa
Wameingia kwenye “deals” zisizoeleweka
Wamebaki na majuto na lawama zisizokoma.

Na swali linabaki moja,  Tatizo ya haya yote  ni nini?
πŸ‘‰ Jibu kubwa ni moja pia: Kukosa uelewa wa misingi ya uwekezaji.
Watu wanaingia kwenye uwekezaji kama bahati nasibu, wakati ni mchezo wa maarifa + uchambuzi + Fedha + nidhamu.

✅ MSINGI WA KWANZA: FANYA UTAFITI YAKINIFU (FEASIBILITY STUDY)
Huu ndiyo msingi unaotenganisha: Wawekezaji halisi na wanaopoteza pesa
Kabla hujaweka hata shilingi 1 — tafiti kwanza
UWEKEZAJI siyo kubahatisha.
Ni sayansi ya kuchunguza kabla ya kuamua kuwekeza.
Ukiruka hatua hii: unapoteza mtaji wako, unapoteza faida na unapoteza muda pia tena kwa wakati mmoja.

Hapa nimekuandalia
🧠 AINA KUU 3 ZA UTAFITI WA UWEKEZAJI kabla hujawekeza kwa ufupi tu.

1. Fundamental Analysis (Uchambuzi wa Msingi)
Huu unaangalia moyo wa biashara au kampuni.
Jiulize:
Wanauza nini?
Wanapataje faida?
Biashara yao ina uhalisia au ni hewa?
Wanaongoza nani (leadership)?
Wana deni kiasi gani?
πŸ‘‰ Utafiti huu unakusaidia kujua:
“Je, hii ni biashara halali au mtego?”

2. Technical Analysis (Uchambuzi wa Mienendo ya Soko)
Huu unahusu zaidi:Mabadiliko ya bei, Grafu za soko, Timing (uingie lini / utoke lini)
πŸ‘‰ Huu hutumiwa sana kwenye: Forex, Crypto, Stocks.
Unajifunza kusoma tabia ya soko badala ya kubahatisha. Kama unapenda mambo ya forex hapa pananjia yako.

3. Quantitative Analysis (Uchambuzi wa Takwimu)
Huu ni wa kitaalamu zaidi.
Unahusisha: Namba, Data, Hesabu za hatari (risk), Uwezekano wa faida.
πŸ‘‰ Hapa unatumia akili ya takwimu kufanya maamuzi, siyo hisia boss.

USIPUUZE HILI.

Nilipokuwa chuoni nilishuhudia vijana wengi sana wakiingia kwenye huu mkenge na kupoteza pesa zao. Wengine walipoteza ada, pesa za kujikimu  kwasababu ya kufuata mkumbo badala ya  kutafiti kwanza.
Kama unaona: Hivi “Weka 50,000 upate 300,000 kwa wiki”,
“Faida ya uhakika bila hatari”
“Usiulize maswali mengi, ingia haraka”
πŸ‘‰ ELEWA HAPO KUNA  MTEGO SHITUKA.
Hakuna uwekezaji wa halali usio na risk.

ANGALIZO
πŸ‘‰ “Pesa hupotea haraka pale inapowekwa mahali ambapo akili haikufika kwanza.”
HATUA ZA KUCHUKUA SASA
Usikurupuke kuwekeza
Jifunze kabla ya kuanza
Uliza maswali mengi
Kagua uhalali wa biashara
Anza kidogo, jifunze, ndipo ukue

MWISHO KABISA
Uwekezaji siyo njia ya kutafuta pesa haraka.
Ni njia ya kujenga utajiri kwa nidhamu, maarifa , pesa na muda.
πŸ‘‰ Ukijifunza kabla ya kuwekeza — utafanikiwa
πŸ‘‰ Ukikurupuka kabla ya kujifunza — utalipa ada ya ujinga.
Tutaendelea na misingi mingine.

Je umejifunza chochote? Share na sisi, ikiwezekana ongezea msingi mwingine na wewe tuendelee kujifunza

ujifunza zaidi tembelea
https://addvaluetz.blogspot.com

#SelfAwareness (#Kujitambua). #Investment (#Uwekezaji). #PersonalDevelopment (#Maendeleobinafsi). #MigongoElias. #zAddValueNetwork. #SeeYouNextLevel
+255767653697

Popular posts from this blog

UKIJUA HILI KUHUSU WATU UTAFANIKIWA SANA.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.

HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 31