KAMA UNASAHAU MARA KWA MARA, SOMA HAPA KWANZA.

Image
  KAMA UNASAHAU MARA KWA MARA, SOMA HAPA KWANZA. Boss! Siyo  kila mara, kusahau ni ishara ya Ubongo dhaifu, mara nyingi ni namna tunavyojifunza ndugu. Nimekutana na watu wengi wakisema: "Mimi sina akili kubwa." Wengine "Kumbukumbu yangu ni mbaya." Mara "Ubongo wangu hauhifadhi vitu." Lakini ukweli ni kwamba, mara nyingi tatizo si ukubwa wa akili yako wala uwezo wa ubongo wako. Tatizo ni kwamba watu wengi hawajawahi kufundishwa jinsi kumbukumbu (memory) inavyofanya kazi boss. Sikia ndugu; Ubongo wa binadamu umeumbwa kwa ustadi mkubwa. Kazi yake si kuhifadhi kila kitu unachokiona au kukisikia, bali ni kuchagua filtering taarifa muhimu na kuacha zisizo muhimu wala matumizi. Kwa hiyo, kusahau si kasoro ya ubongo ni sehemu ya kawaida ya jinsi unavyofanya kazi. Hebu tuangalie sababu kuu zinazowafanya watu kusahau mara kwa mara. 1. Kukariri Bila Kuelewa (memorising without understanding). Hili ndilo kosa kubwa zaidi ambalo wanafunzi na hata watu wazima...

SIYO PESA PEKEE ZINAZOKUFANYA UWE MWEKEZAJI, NI MISINGI.

 


SIYO PESA PEKEE ZINAZOKUFANYA UWE MWEKEZAJI, NI  MISINGI.


Watu wengi wanapofikiria UWEKEZAJI, jambo la kwanza linalokuja akilini mwao ni pesa nyingi.
Ndiyo maana wengine husema, “Nikishapata pesa nyingi ndipo nitaanza KUWEKEZA.”.

Lakini ukweli ni tofauti kidogo.
Uwekezaji wa kweli hauanzi na pesa nyingi.
Unaanza na MISINGI sahihi ya KIFEDHA.
Watu wengi hupata na kuzalisha pesa siyo tatizo kwao, lakini hawajengi utajiri.

Kwa nini?
Kwa sababu hawajajifunza misingi ya kuitunza na kuikuza. Kila kitu kina misingi na kanuni zake.
Kabla ya kufikiria uwekezaji mkubwa, jifunze kwanza mambo machache ya msingi.

Jifunze kuishi chini ya kipato chako.
Jifunze kuokoa hata kama ni kidogo.
Jifunze kupanga matumizi yako.
Na jifunze kuwa na subira.
Kwa sababu uwekezaji si mbio za haraka.

Ni safari ya uvumilivu.
Ni kama kupanda mti.
Unapanda mbegu leo.
Unaimwagilia kila siku.
Unaipa muda ikue.
Halafu baada ya muda, inaanza kutoa kivuli  na baadaye matunda.

Tatizo la wengi ni kutaka matunda kabla ya kupanda mbegu na kuimwagilia
Lakini ukweli unabaki kuwa huu:

👉 utajiri wa kudumu hujengwa kwa uwekezaji na uwekezaji hujengwa juu ya misingi imara.
Hata kama unaanza kidogo leo, usidharau hatua hiyo.
Kila akiba ndogo ni mbegu.
Kila uamuzi mzuri wa kifedha ni maji ya kumwagilia mbegu hiyo.
Na kadri muda unavyopita, mbegu hiyo inaweza kukua na kuwa mti mkubwa.
Anza pale ulipo.
Anza na kile ulichonacho.
Lakini hakikisha unajenga misingi sahihi ya uwekezaji.
Kwa sababu mwisho wa siku,
sio pesa nyingi zinazounda utajiri…
bali ni nidhamu ya kifedha inayojengwa taratibu.

Je, unachangamoto katika uwekezaji na unahitaji usaidizi?

Naamini umejifunza kitu kujifunza zaidi tembelea
https://addvaluetz.blogspot.com

Self Awareness (Kujitambua).
Investment (Uwekezaji).
Personal Development (Maendeleo binafsi).
Migongo Elias.
+255767653697
Add Value Network.
Knowledge Is Power.

Popular posts from this blog

UKIJUA HILI KUHUSU WATU UTAFANIKIWA SANA.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29