TABIA ZAKO NDIZO ZINAZOAMUA HATIMA YAKO

 


TABIA ZAKO NDIZO ZINAZOAMUA HATIMA YAKO

Watu wengi wanapozungumzia mafanikio, kufika mbali na kuwa watu wakubwa, mara nyingi huangalia vitu vikubwa kama vile; elimu, mtaji, connections, bahati na hata urithi. Lakini kuna ukweli ambao wengi hawautaki kuukubali ambao ni huu: MAFANIKIO yako yamejificha ndani ya TABIA zako za kila siku.

Ndiyo TABIA zako. Siyo ndoto zako, siyo mipango yako, siyo marafiki zako, siyo juhudi zako, bali tabia zako ndizo zinazoamua utafika wapi kesho.
Ukweli mchungu mwingine ni kwamba huwezi kuwa na maisha makubwa ukiwa na tabia ndogo, never.

KAMA NDIVYO HIVYO,  TABIA NI NINI BASI?
Tabia ni yale mambo unayafanya kila siku bila hata kufikiria sana wala kutumia nguvu. Yale matendo na maamuzi madogo madogo unayorudia kila siku kuyafanya, kama vile;
Unaamka saa ngapi?
Unatumiaje muda wako au kupiga soga tu.
Unasoma au unateleza tu  mitandaoni
Unadhibiti hisia zako au zinaongoza maisha yako
Hivi vitu vinaonekana vidogo vidogo sana, lakini kwa muda mrefu vinajenga maisha yako yote.

MAFANIKIO NI MKUSANYIKO WA TABIA NDOGO
BOSS WANGU.
Hakuna mtu anayefanikiwa kwa tukio moja kubwa. Mafanikio ni matokeo ya:
Nidhamu ya kila siku. Kujifunza kila siku.
Kujirekebisha kila siku. Kujinidhamisha kila siku.

Ukifanya kitu kidogo sahihi kila siku, matokeo yake huwa makubwa sana baada ya muda.
Lakini pia ni kweli: Ukifanya makosa madogo kila siku, nayo hukusanyika na kukupeleka kwenye anguko nq kushindwa.
Ndugu huu ni uwekezqji kama tulivyojifunza somo lililopita. Unawekeza kwenye tabia njema, unawekeza kwenye afya yako, unawekeza kwenye bidii, unawekeza kwenye networks n.k hizi zote ni tabia njema  lazima zikupe unachokitaka na kinyume chake ni kweli.

Hiyo ndiyo inaitwa COMPOUND EFFECT.

HATA HIVYO NIMEGUNDUA KUWA, SABABU INAYOWARUDISHA NYUMA VIJANA WENGI
Siyo kukosa fursa.
Siyo kukosa pesa.
Siyo kukosa elimu, bidii, wala connections.
Bali ni kukosa KUKOSA TABIA SAHIHI.

Watu wengi wanataka matokeo makubwa lakini hawako tayari kubadilisha mfumo wa maisha yao: Wanataka mafanikio lakini hawataki nidhamu.
Wanataka pesa lakini hawataki kujifunza na kujishughulisha.
Wanataka heshima lakini hawana maadili hiii ni hatari sana.
Na hapo ndipo tatizo lilipo kama ulikuwa hujui.
SIRI YA NDANI AMBAYO INABADILISHA MAISHA,
Kila tabia unayorudia leo, inaijenga kesho yako. Rudia tena kusoma hapo.
Ukizoea uvivu → unajenga kushindwa
Ukizoea nidhamu → unajenga mafanikio
Ukizoea visingizio → unajenga maisha ya kawaida (moderate life).
Ukizoea uwajibikaji → unajenga maisha ya kipekee sana.
Hakuna njia ya mkato hapa. There is no shortcut boss wangu.

Unajua uchawi ulipo?
BADILISHA TABIA, BADILISHA MAISHA
Kama unataka mafanikio makubwa, usianze na ndoto kubwa, anza na tabia ndogo zitakazo kupeleka kwenye huo ukuu.
✔️ Anza kuamka mapema.
✔️ Punguza kupoteza muda wako.
✔️ Jifunze kitu kipya kila siku.
✔️ Jizungushe na watu wanaokujenga.
✔️ Fanya kile unachopaswa kufanya hata kama hujiskii kufanya(hii ndo nidhamu boss).
Hapo ndipo safari ya  mafanikio huanzia ndugu.

Ninapoelekea kumalizia, mwanzoni nilikuwa najua ni SIRI. Kumbe MAFANIKIO siyo SIRI. Bali ni MFUMO.
Na mfumo huo unajengwa na TABIA ZAKO.
Usiombe maisha mazuri bila kubadilisha tabia zako utaanguka, anguko kubwa.
Usitamani mafanikio bila kuishi maisha yanayozalisha mafanikio.
Kumbuka:
👉 Unachofanya kila siku, ndicho unachokuwa kesho.
Unataka kuwa mwanamziki mkubwa, mwana siasa, mfanyabiashara, mkulima, muhasibu n.k  kunatabiq zake anza kuziishi leo na iwe tamaduni yako.

Swali kwako: Ni tabia ipi moja utaanza kubadilisha kuanzia leo ili kubadilisha maisha yako?

Je umejifunza chochote? Share na sisi, ikiwezekana ongezea msingi mwingine na wewe tuendelee kujifunza

Kujifunza zaidi tembelea
https://addvaluetz.blogspot.com

#SelfAwareness (#Kujitambua). #Investment (#Uwekezaji). #PersonalDevelopment (#Maendeleobinafsi). #MigongoElias. #AddValueNetwork. #SeeYouNextLevel
+255767653697

Popular posts from this blog

UKIJUA HILI KUHUSU WATU UTAFANIKIWA SANA.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.