UMASKINI VS UTAJIRI: VYOTE HUANZIA AKILINI.

 


UMASKINI VS UTAJIRI: VYOTE HUANZIA AKILINI.


Watu wengi hudhani kuwa umaskini na utajiri ni ukosefu au wingi wa pesa na mali.
Kwa kiasi fulani hilo linaweza kuwa kweli, lakini kuna ukweli mkubwa zaidi ambao mara nyingi watu hawauoni.

Ukweli ni huu ni:
umaskini na utajiri huanzia akilini kabla ya kuonekana mfukoni.
Nakumbuka Mentor wangu mmoja kutoka Kenya, Konji Oloyi, aliwahi kuniambia maneno ambayo sikuyasahau:
"Poverty and wealth are in the mind; lack or abundance are just signs. Many people confuse these."
Akimaanisha kuwa umaskini na utajiri upo kichwani. Ukosefu au utele wa pesa ni dalili tu.

Ndugu yangu, umaskini huanza kichwani.
Kadhalika utajiri nao huanza kichwani.
Ukosefu wa pesa mfukoni unaweza kuwa dalili ya umaskini, lakini hata kuwa na pesa nyingi mfukoni kunaweza kuwa dalili ya utajiri.

Ndiyo maana Napoleon Hill aliandika katika kitabu kinachoitwa Think and Grow Rich.
Kwa lugha rahisi ni: FIKRA zako zina mchango mkubwa sana katika kile unachokuwa.
Sio kwamba ukiwaza UTAJIRI tu unakuwa TAJIRI.
Lakini ukweli ni kwamba, mtazamo wako (mindset) ndio jikoni ambako MAISHA yako yanapikwa.
Watu wengi wakisikia fursa za MAFANIKIO au njia za kubadilisha MAISHA yao, tayari wanakuwa wamejitoa kwenye MCHEZO.

Utasikia wakisema:
“Hayo hayatuhusu.”
“Hizo ni za watu fulani.”
“Sisi ni wa maisha ya kawaida tu.”
Huenda wanaona kama ni maneno tu.
Lakini kwa ukweli wanakuwa wanajenga MINDAET ya UMASKINI.

Hapo ndipo utaona tofauti ya TAJIRI na MASKINI.
Mtu mwenye fikra za utajiri anaamini kuwa:
fursa, mafanikio, mali na maendeleo ni sehemu ya HAKI yake katika maisha.
Huanza ndani kama fikra.
kisha huonekana nje kama tabia.
Ndiyo maana mara nyingi utaona MASKINI wengi wanafanana kwa tabia.
Wengi ni walalamikaji.
Wanalaumu serikali.
Wanalaumu viongozi.
Wanalaumu ndugu na marafiki.
Wakati mwingine wanamlaumu hata Mungu.
Wanaamini wameumbwa kuteseka na kuwa maskini.

Lakini watu wenye FIKRA za MAFANIKIO wanaamini tofauti kabisa.
Wanajua kuwa maisha yanaweza KUBADILIKA.
Na mabadiliko hayo huanzia ndani yao, Na wao ndio wenye JUKUMU la mabadiliko hilo.

Nakumbuka niliwahi kuandika maneno haya:
“Moyo wako ni kama akaunti ya benki.
Kile unachoweka ndani yake kila siku, ndicho utakachokuja kuvuna baadae.”
Ukijaza hofu… utavuna hofu.
Ukijaza woga… utavuna woga.
Ukijaza fikra za umaskini… utavuna umaskini.
Lakini ukijaza ujasiri, matumaini na fikra za Utajiri na mafanikio. Hayo pia ndiyo utakayokuja kuvuna.

Ndiyo maana maandiko yanasema:
"Mtu mwema katika akiba njema ya moyo wake hutoa matunda mazuri.
Na mtu mwovu katika akiba mbaya ya moyo wake hutoa matunda mabaya."

Hivyo basi jiulize maswali haya muhimu:
Mtazamo wako ukoje?
Unajaza akili yako taarifa gani?
Ni watu gani unaowasikiliza na kujifunza kwao?
Marafiki zako wanakujenga au wanakubomoa?
Huenda hawa wote wasionekane kama wanahusika moja kwa moja na maisha yako.
Lakini wana mchango mkubwa sana katika kumtengeneza wewe wa leo.

Kumbuka jambo hili muhimu sana:
Mabadiliko ya kweli huanzia ndani.
Ndani ya moyo wako. Ndani ya fikra zako.
Ndiyo maana Sulemani aliandika:
"As a man thinketh in his heart, so is he."
Aonavyo mtu nafsini mwake, ndivyo alivyo.

Habari njema ni hii:
Unaweza kuamua kubadilika. Unaweza kubadilisha mtazamo wako.
Unaweza kupanua MIPAKA ya FIKRA NA MOYO wako.
Kwa sababu MAISHA yako yanaendeshwa na MIPAKA iliyopo ndani ya moyo wako.
Huwezi kumiliki zaidi ya kiwango ambacho akili na Moyo wako unaamini kinawezekana.

Kama kuna hali (Tabia, magonjwa, umaskini, kipato n.k) katika maisha yako ambayo huipendi.
anza kubadilisha kile kilichopo ndani yako.
Panua fikra zako.
Ondoa mipaka uliyojiwekea.

Najua si rahisi. Lakini hii ndiyo njia ya UPONYAJI na MABADILIKO ya kweli.
Na mara nyingi mabadiliko haya huanza pale mtu ANAPOCHOSHWA kabisa na hali aliyonayo.

Kama utatazama maisha yako na kuridhika nayo, hiyo ni sawa.
Lakini kama moyoni unajua kuna zaidi ya hapo,
anza na kubadilisha mtazamo wako.
Kwa sababu huu ndio mwanzo imara wa kufika huko unapotaka kwenda.

Naamini umejifunza kitu kujifunza zaidi tembelea
https://addvaluetz.blogspot.com

Self Awareness (Kujitambua).
Investment (Uwekezaji).
Personal Development (Maendeleo binafsi).
Migongo Elias.
+255767653697
Add Value Network.
Knowledge Is Power.

Popular posts from this blog

UKIJUA HILI KUHUSU WATU UTAFANIKIWA SANA.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.