INUKA TENA

Image
  INUKA TENA Siku zote maisha siyo safari ya watu wasiopata changamoto. Ni safari ya watu wanaoanguka, wanajifunza, na kuinuka tena kwa nguvu zaidi boss. Watu wengi hudhani mafanikio ni safari ya moja kwa moja the straight line ambapo: unafanya vizuri kila wakati, hakuna kushindwa, hakuna maumivu. Lakini ukweli ni kwamba, kila mtu aliyefanikiwa amewahi kuanguka mara nyingi zaidi kuliko unavyofikiri boss. Tofauti yao na wengine si kwamba hawaanguki, noo, bali ni kwamba waliinuka tena baada ya kuanguka. BOSS, KUANGUKA SI MWISHO WA SAFARI. Kuanguka ni sehemu ndogo tu ya ukuaji. Kwasababu Unaposhindwa: unajifunza kitu kipya, unagundua makosa yako, unaelewa njia iliyo bora zaidi. na unapata uzoefu ambao hauwezi kufundishwa darasani ndugu yangu. Tatizo la watu wengi hufanya kosa moja kubwa: yaani,  wanaona kuanguka kama mwisho wa safari yao, mara wao ni wakushindwa tu. Wao si lolote. Hapo ndipo ndoto nyingi hufa kabla hazijakomaa kabisa ndugu. Sikiliza boss, Kuanguka haku...

USIISHI TU ISHI KWA KUSUDI.

 


USIISHI TU ISHI KWA KUSUDI.


Kuna watu wengi wanaamka kila siku, wanafanya kazi, wanatafuta pesa, wanapambana na maisha.

Lakini ndani yao kuna swali ambalo bado halijajibiwa. Ambalo ni,
“NIMEKUJA DUNIANI KUFANYA NINI?”

Kwa sababu ukweli ni huu:
sio kila mtu anayeishi anaelewa kusudi la maisha yake hapa duniani.

Wengine wanafuata mkondo wa dunia.
Wengine wanaiga maisha ya wengine.
Wengine wanapoteza miaka mingi wakikimbiza vitu ambavyo havina maana ya kudumu.

Lakini maisha hubadilika na kuwa na maana pale unapogundua kwa nini upo hapa duniani.

Kusudi la maisha sio tu kupata pesa.
Sio tu kuwa maarufu.
Sio tu kumiliki vitu vingi.
Wala si kuwa na kazi nyingi.
Bali,
Kusudi la maisha ni kugundua ZAWADI (uwezo, kipaji, karama, nguvu n.k) uliyopewa na Mungu.
na kuitumia kuleta MWANGA(wepesi) katika maisha yako na maisha ya wengine.

Ndiyo maana watu wanaoishi kwa kusudi huwa na nguvu tofauti.
Changamoto zinakuja, lakini hawaachi kufanya.
Wanakosolewa, lakini bado wanaendelea.
Kwa sababu wanajua wao ni akina nani, wametoka wapi, wapo wapi na wanaenda wapi?.

Labda leo unajiuliza maswali mengi kuhusu maisha yako.
Labda bado hujaona wazi KUSUDI la Mungu katika maisha yako.
Lakini kumbuka jambo moja muhimu:
Hakuna mtu aliyeumbwa bila sababu.
Hata kama wazazi wako hawakukutarajia, hata kama kama ulipatikana kwa njia isiyo sahihi. Elewa kuwa,
Hakuna maisha ya mtu yaliyoletwa duniani kwa bahati mbaya.

Na wewe pia haupo hapa kwa bahati mbaya.
Ndani yako kuna kitu ambacho dunia inakihitaji.
Utawezq kuipamba dunia na kuilemba kwacho.
Ndani yako kuna NURU ambayo inaweza kuwasaidia wengine kuona njia.
Usiishi tu kupita duniani.

Ishi ukigundua, ukikuza, na ukilitimiza kusudi la maisha yako.
Kwa sababu maisha yenye maana si yale unayoishi kwa mazoea.
bali yale unayoishi kwa kusudi ambalo Mungu amekuumba kwalo.


Self Awareness (Kujitambua).
Investment (Uwekezaji).
Personal Development (Maendeleo binafsi).
Migongo Elias.
+255767653697
Add Value Network.
Knowledge Is Power.

Popular posts from this blog

UKIJUA HILI KUHUSU WATU UTAFANIKIWA SANA.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29