KAMA UNASAHAU MARA KWA MARA, SOMA HAPA KWANZA.

Image
  KAMA UNASAHAU MARA KWA MARA, SOMA HAPA KWANZA. Boss! Siyo  kila mara, kusahau ni ishara ya Ubongo dhaifu, mara nyingi ni namna tunavyojifunza ndugu. Nimekutana na watu wengi wakisema: "Mimi sina akili kubwa." Wengine "Kumbukumbu yangu ni mbaya." Mara "Ubongo wangu hauhifadhi vitu." Lakini ukweli ni kwamba, mara nyingi tatizo si ukubwa wa akili yako wala uwezo wa ubongo wako. Tatizo ni kwamba watu wengi hawajawahi kufundishwa jinsi kumbukumbu (memory) inavyofanya kazi boss. Sikia ndugu; Ubongo wa binadamu umeumbwa kwa ustadi mkubwa. Kazi yake si kuhifadhi kila kitu unachokiona au kukisikia, bali ni kuchagua filtering taarifa muhimu na kuacha zisizo muhimu wala matumizi. Kwa hiyo, kusahau si kasoro ya ubongo ni sehemu ya kawaida ya jinsi unavyofanya kazi. Hebu tuangalie sababu kuu zinazowafanya watu kusahau mara kwa mara. 1. Kukariri Bila Kuelewa (memorising without understanding). Hili ndilo kosa kubwa zaidi ambalo wanafunzi na hata watu wazima...

USISAHAU KILICHOKULETA HAPO.

 

USISAHAU KILICHOKULETA  HAPO.


Kuna makosa mawili makubwa ambayo watu wengi hufanya wanapoanza kuyaona mafanikio yao:
wanasahau walikotoka, na wanasahau kilichowafikisha hapo. Haya ni makosa makubwa mawili, ni kesi ya kutokujitambua.
Hapo ndipo safari yao huanza kushuka bila wao kujua yaani, kimya kimya.

UKWELI AMBAO NIWACHACHE WANAUJUA,
Mafanikio hayakuji kwako kwa bahati mbaya.
Yalikuja kwa sababu ya vitu fulani ulivyofanya.
Yamkini huenda; Ulijituma sana, Ulijinyima, Ulijifunza, Uliomba sana, ulisave sana,
Ulijitoa zaidi kuliko wengine,
Ulivumilia wakati mgumu.

πŸ‘‰ Hiyo ndiyo “formula” yako ya mafanikio.
Lakini shida inaanza pale unapopata mafanikio walau kidogo, halafu ghafula unaanza kubadilika.
UNAPOSAHAU KILICHOKULIPA, UNAPOTEZA MWELEKEO WAKO.
Watu wengi wakianza kuona matokeo:
Wanaacha nidhamu,
Wanaacha kujifunza,
Wanaanza kujiamini kupita kiasi,
Wanasahau kujituma,
Wanaanza maisha ya anasa mapema sana. Kisa wameona matokeo kidogo tu.

Namatokeo yake,
πŸ‘‰ Wanarudi pale pale walipotokea, au hata chini zaidi ya hapo.
DAIMA KUMBUKA HILI,
Kile kilichokupa mafanikio ya kwanza, ndicho kitakachokupa mafanikio makubwa zaidi.
Hakuna uchawi wowote mpya. Iko hivi;
✔️ Kama kusoma kulikulipa → endelea kusoma
✔️ Kama nidhamu ilikulipa → linda nidhamu hiyo
✔️ Kama kujitoa kulikulipa → ongeza juhudi, n.k.

KWA MFANO,
Hebu fikiria mtu aliyefanikiwa kwa sababu ya:
Kuamka mapema,
Kufanya kazi kwa bidii,
Kujifunza kila siku,
Akipata mafanikio kidogo na kuacha hayo yote, nini kinatokea?
Jibu ni rahisi tu hapo,
πŸ‘‰ Anakata mzizi wa mti uliokuwa unamlisha.
Mafanikio yako yana “root” (mzizi).
Na mzizi huo ni: πŸ‘‰ Tabia + maamuzi + nidhamu
Ukikata mzizi, matunda lazima yanyauke na  kuanguka boss.

SOMO KUBWA la kujifunza ni kwamba,
Mafanikio siyo kufika kileleni tu,
ni kubaki kileleni baada ya kufika kileleni.

Lakini kubaki kileleni kunahitaji:
Nidhamu ile ile
Juhudi zile zile
Mfumo ule ule uliokufikisha hapo. Na kama utahitaji kupanda zaidi itakubidi kufanya zaidi.

HEBU JIPIME LEO KIDOGO TU.
Jiulize huvi kwa uaminifu mkubwa kabisa:
Ni kitu gani kilinisaidia kufika hapa nilipo?
Je bado nakifanya kwa kiwango kile kile?
Au nimeshaanza kuzingua?
πŸ‘‰ Hapo ndipo jibu la kuinuka kwako lilipo.

KANUNI KUU
Usibadili mfumo uliokufanya ushinde  UBORESHE TU au ubadilishe viwango tu (levels).

Badala ya kuacha: Soma zaidi,
Fanya kazi kwa bidii zaidi,
Jifunze zaidi,
Jiboreshe,
Jidhibiti zaidi. N.k

Mwisho kabisa,
Watu wengi hawashindwi kufanikiwa, yaani siyo kazi kwao kufanikiwa.
wanashindwa kudumisha mafanikio.
Na sababu kubwa ni hii:
πŸ‘‰ Wanasahau walikotoka na kilichowafikisha hapo.
Wewe usiwe mmoja wao.
Linda chanzo chako.
Linda tabia zako.
Linda nidhamu yako.
Kwani kila mmoja anasiri ya ukuu wake.

πŸ’¬ Swali kwako:
Ni kitu gani kimoja kilikusaidia kufika hapa ulipo na je bado unakifanya?
Share na sisi, ikiwezekana share na wengine ujumbe huu.

#SelfAwareness (#Kujitambua). #Investment (#Uwekezaji). #PersonalDevelopment (#Maendeleobinafsi). #MigongoElias. #AddValueNetwork. #SeeYouNextLevel
+255767653697

Popular posts from this blog

UKIJUA HILI KUHUSU WATU UTAFANIKIWA SANA.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.

HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 31