MAKOSA YA KAWAIDA KATIKA UWEKEZAJI.
MAKOSA YA KAWAIDA KATIKA UWEKEZAJI.
Uwekezaji siyo tu kuweka rasilimali kama pesa, muda au nguvu sehemu fulani ni mchakato wa kimkakati wa kukuza thamani yako ili upate faida ya baadaye. Na katika uwekezaji lengo kuu huwa ni moja kupata FAIDA.
Lakini ukweli ni kwamba, watu wengi wanaingia kwenye uwekezaji wakiwa na ndoto kubwa ya kupata faida, lakini wanatoka wakiwa na hasara, maumivu, na majuto boss.
We unadhani ni kwa nini boss?
Kwa sababu ya makosa ya msingi ambayo wengi huyafanya lakini yanaweza kuepukika kabisa boss wangu.
Leo tuyaweke wazi ili wewe usiwe miongoni mwa wanaopoteza.
Kosa la kwanza.
KUTAKA FAIDA YA HARAKA (GET RICH QUICK MENTALITY).
Hii ndiyo sumu kubwa zaidi ndugu yangu katika uwekezaji.
Watu wanataka mafanikio ya haraka bila kuvumilia mchakato wenyewe.
Na ukweli ambao hauujui ni huu:
Uwekezaji halisi unahitaji rasilimali, muda, nidhamu, na subira. Zingatia muda na subira bos
Ukikimbilia faida za chapu chapu:
Utadanganywa kwa urahisi, Utaingia kwenye miradi hatarishi
Utapoteza pesa zako.
Kumbuka: Faida kubwa ya haraka mara nyingi huja na hatari kubwa yaani, risk vs return boss.
Kosa la pili.
KUOGOPA KUWEKEZA KWA HOFU YA HASARA.
Ndiyo, uwekezaji una hatari. Lakini pia una fursa.
Wengi wanaangalia upande mmoja tu hasara na kusahau kuwa:
Hakuna mafanikio bila kuchukua hatua.
Ukiendelea kusubiri “wakati sahihi”:
Utachelewa kuanza
Utapoteza fursa nyingi
Na mwisho utaishia kulaumu muda na wakati mwingine utabaki unasubiri daima.
Katika uwekezaji Ujasiri wenye maarifa ndiyo ufunguo boss wangu.
Kosa la tatu.
KUFUATA MKUMBO (HERD MENTALITY).
Utakuta mtu akisema “Watu wote wanafanya, basi na mimi nifanye.”
Hili ni kosa hatari sana.
Kila uwekezaji una: mazingira yake
muda wake, na uelewa wake
Ukiingia bila utafiti: hapo Hujui unachofanya
Hujui hatari, Hujui lini utoke
Uwekezaji siyo fashion ni maamuzi ya kifedha boss wangu.
Kosa la nne.
KUTOKUWA NA LENGO WAZI (NO CLEAR PURPOSE)
Kwa nini unawekeza?
Unataka nini hasa? Na unataka lini?
Bila majibu ya maswali haya:
Utawekeza bila mwelekeo
Utaacha njiani
Au utafanya maamuzi ya kihisia
Kama alivyoeleza Simon Sinek, kwenye kitabu chake cha “Start with WHY.”
Jua sababu yako, jua muda wako, Jua malengo yako boss.
Kosa la tano.
KUACHA UWEKEZAJI MAPEMA SOKO LINAPOSHUKA.
Ndugu yangu Soko halikai sehemu moja linapanda na kushuka.
Wengi wanapokutana na changamoto:
Wanapaniki
Wanauza kwa hasara
Wanakata tamaa
Lakini wawekezaji wenye akili:
Wanabaki na mkakati wao
Wanatumia kushuka kama fursa
Wanavuna baadaye bei ikipanda.
Ndugu yangu Subira inalipa. Panic inagharimu.
Kosa la sita.
KUKOSA UTAFITI WA KINA (NO Research DILIGENCE).
Kuwekeza bila utafiti ni sawa na kuingia vitani bila silaha. Ama ni sawa na kubet.
Kabla hujawekeza kwenye biashara au sehemu yeyote jiulize: Hii biashara inaendeshwaje?
Faida inatoka wapi? Hatari zake ni zipi?
Hlafu boss usiwe wale watu wa: “Nimesikia…” et
“Wamesema…” mara “Inaonekana nzuri…”
Goja nikwambie boss we fanya hivi Chunguza. Elewa. Kisha amua kufanya kweli.
Kosa la saba.
KUWEKEZA PESA ZOTE SEHEMU MOJA.
Hili ni kosa linaloumiza wengi boss wangu. Inshu hii ni nzuri ka uta win boss lakin ubaya wake ni kwamba
Ukikosea tu, unapoteza kila kitu. Yaani one mistake 100 goals.
Ushauri wa bure boss: Gawanya uwekezaji wako (Diversification) kama tulivyoongea kipindi cha nyuma.
Linda mtaji wako kwanza boss wangu.
Kosa la nane.
KUWEKEZA BILA ELIMU YA KIFEDHA
Kitu cha ajabu ambacho nakiona kila mara ni kwmba, Watu wengi wana pesa kidogo lakini hawana uelewa hata kidogo. Hebu soma tena hapo.
Matokeo yake: wanadanganywa, wanapoteza pesa, wanarudia makosa yale yale.
Ndugu yangu Elimu ndiyo uwekezaji wa kwanza kqbisa.
UKWELI MUHIMU (REAL TALK)
Uwekezaji siyo mchezo wa kubahatisha kama ilivyo kwenye kamali.
Huu ni mchezo wa: rasilimali, maarifa, nidhamu
na maamuzi sahihi boss.
Ukifanya makosa haya, utapoteza.
Ukijifunza kuyakwepa, utashinda. Uchaguzi ni wako mwenyewe boss wangu.
Ndugu yangu kabla sijamalizia Leo fanya hivi:
Tathmini uwekezaji wako wa sasa
Angalia ni kosa gani unafanya
Anza kujifunza kabla ya kuwekeza zaidi
Chukua hatua kwa akili, si kwa hisia.
Usiwe mwekezaji wa hasara. Kuwa mwekezaji wa maarifa. Ndugu yangu.....
Share na mimi kupitia comment ulichojifunza. Ikiwezekana share na wengine ujumbe huu ili wajifunze pia.
Kujifunza tembelea,
https://addvaluetz.blogspot.com/2026/04/nguvu-ya-mawazo-yako.html
#SelfAwareness (#Kujitambua). #Investment (#Uwekezaji). #PersonalDevelopment (#Maendeleobinafsi). #MigongoElias. #AddValueNetwork. #SeeYouNextLevel
+255767653697.
