NGUVU YA KUELEWA NA KIDHIBITI HISIA ZAKO.

 


NGUVU YA KUELEWA NA KUDHIBITI HISIA ZAKO.


Watu wengi wanadhani kuwa, kuwa na nguvu ni kidhibiti, kushikiria na kukandamiza hisia zao. Lakini nimekuja gundua ukweli ni kinyume chake kabisa boss. Nguvu ya kweli ni kuelewa hisia zako, kuzikubali, na kuziongoza bila kuzifanya zikudhibiti wala kukucontrol boss.

Kuelewa hisia zako ni uwezo wa kutambua:
Unajisikiaje, kwa nini unajisikia hivyo,
Na unapaswa kufanya nini bila kuharibu hali
Huu ndiyo msingi wa kile kinachoitwa akili ya kihisia (emotional intelligence). Wakati mwingine huu ndo ustadi unaotofautisha kati ya watu wanaofanikiwa na wanaoishia kujilaumu wao wenyewe.
Ndugu yangu huu ni ufunguo ya utulivu wa ndani na maamuzi sahihi ya maisha.

MARA NYINGI TUMEFUNDISHWA KUELEWA HISIA NI ADUI KUTOKA NDANI YETU:  LAKINI UKWELI NI KWAMBA HISIA SI ADUI, BALI NI UJUMBE. Hii niflow of energy inayokuja na ujumbe maalum kwa muhusika.

Hisia si tatizo. Hisia ni lugha ya ndani ya nafsi yako boss.
Hata hivyo kila hisia unayopata ina kitu inajaribu kukuambia: hebu goja tuone mifano kidogo hapa;

Mfano ukipata hasira
Hii inakupa ujumbe kuwa kuna mpaka wako umevunjwa boss.

Ukipa Hofu
Hii inatuma ujumbe unakua tahadhari kuna kitu muhimu au kunahatari inahitaj ulinzi boss.

Huzuni
Hii inatuma ujumbe kuwa umepoteza kitu chenye thamani kwako.

Wivu
Inaashitia kuwa kuna kitu unachokitaka/kukitamani lakini huna.

Furaha
Hii inamaanisha upo kwenye mwelekeo sahihi.

Chuki
Huu ni ujumbe kuwa una jeraha la ndani au maumivu ambayo hujayashughulikia.

Mapenzi
Hii ni sawa na kusema kuna uhusiano, thamani au kitu kinachokupa maana ya kweli.

Ndugu yangu elewa kuwa tatizo si hisia. Tatizo ni kutoielewa hisia pamoja na ujumbe wake.

UKWELI MGUMU UNAOPASWA KUUJUA NI HUU,
Watu wengi: wanakimbia hisia zao, wanazificha
Au wanazipuuza.
Lakini elewa kuwa:
Hisia zilizozuiwa hazifi bali zinakusanyika na kulipuka baadaye kwa nguvu kubwa  zaidi.
Kwa mfano;
๐Ÿ‘‰ Hasira iliyofichwa hugeuka chuki.
Huzuni iliyopuuzwa hugeuka mfadhaiko na
๐Ÿ‘‰ Wivu usiotambuliwa hugeuka chuki ya kimya
Na hapo ndipo watu huanza kufanya maamuzi mabaya bila kuelewa kwanini. Sijui unanipata boss!

HATUA 3 ZA KUDHIBITI HISIA ZAKO
1. SIMAMA — USITENDE MARA MOJA.
Ndugu yangu, Hisia ni kama wimbi.
Ukiruhusu wimbi likupite bila kulipinga, linatulia lenyewe. We fanya hivi;
๐Ÿ‘‰ Usijibu ujumbe ukiwa na hasira
๐Ÿ‘‰ Usifanye maamuzi ukiwa na hofu
๐Ÿ‘‰ Usichukue hatua ukiwa umejaa chuki
Pumua polepole mara 3. Hapo tayari umeanza kushinda boss wangu.

2. IPE JINA HISIA HIYO.
Hii ni siri ambayo wengi hawaijui.
Badala ya kusema:  “Mimi nina hasira”
Sema:
✅ “Ninahisi hasira ndan yangu”
Tofauti yake ni hii:
Ya kwanza inakufanya uwe hisia yenyewe.
Ya pili inakutenganisha wewe na hisia.
Utafiti unaonyesha kuwa kuipa hisia jina hupunguza nguvu yake mara kadhaa .

3. TAFUTA UJUMBE WA HISIA
Jiulize kwa uaminifu:
Hisia hii inaniambia nini?
Kuna nini kimevunjika ndani yangu?
Ninahitaji nini sasa hivi?
Mfano:
Hasira → Labda umeheshimiwa kidogo
Chuki → Labda kuna jeraha hujapona
Mapenzi → Labda kuna kitu kinachokupa maana ya kweli
Halafu kama utagundua kitubni kwamba, hisia zako zinakuongoza ukizisikiliza vizuri boss wangu.

Leo nimechoka kuandika goja nimalize kwa kusema, JITAWALE KUTOKA NDANI kwan,
Kujua hisia zako si udhaifu.
Ni ustadi wa hali ya juu wa maisha yako.

Ukiweza: Kuzitambua, kuzielewa, kuzitafsiri,
Kuzipa nafasi Na kuziongoza.
Basi: Utakuwa na amani tena aman ya ndani THE INNER PEACE boss wangu. Kwasababu,
๐Ÿ‘‰ Utakuwa na maamuzi bora,
Na utaishi maisha yenye maana.

KWA KUANZA LEO  fanya hivi:
Tambua hisia moja uliyo nayo sasa, kisha
Ipe jina na jiulize inakuambia nini hiyo hisia.
Lakini pia, chukua hatua sahihi si ya haraka, wala
Usikimbie hisia zako. Zisikilize ndipo zitakuongoza zenyewe tu boss.

Share na mimi kupitia comment ulichojifunza. Ikiwezekana share na wengine ujumbe huu ili wajifunze pia.

Kujifunza tembelea,
https://addvaluetz.blogspot.com/2026

#SelfAwareness (#Kujitambua). #Investment (#Uwekezaji). #PersonalDevelopment (#Maendeleobinafsi). #MigongoElias. #AddValueNetwork. #SeeYouNextLevel
+255767653697.

Popular posts from this blog

UKIJUA HILI KUHUSU WATU UTAFANIKIWA SANA.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29