NGUVU YA MAWAZO YAKO

 


NGUVU YA MAWAZO YAKO

Mara nyingi tunadhani maisha yetu yanaamuliwa na mazingira, bahati, au watu wanaotuzunguka hili nilikaa nalo kwa muda mrefu sana. Hata hivyo nimekuja gundua, ukweli uliojificha ni huu: maisha yako yanaendeshwa na mawazo yako yaani, jinsi unavyofikiri boss. Ngoja nikwambie ndugu ndani yako kabisa, kuna sauti ya kimya inayokuambia wewe ni nani, unaweza nini, na una thamani gani, watu wanakuonaje n.k  na mara nyingi hata huihoji sababu ushaizoea.

HIVI UNAZANI MAWAZO YAKO NI NANI?
Jiulize kwa uaminifu tu:
Unapoamka asubuhi, unajiambia nini?
“Leo itakuwa ngumu?”
“Sitafanikiwa?”, "mimi ni mbaya", "siwezi"
“Maisha ni magumu sana?” n.k.

Kama hujui hayo si ukweli. Hizo ni imani ulizojijengea  labda kutokana na uzoefu, mazingira, kumbukumbu, mawazo au watu uliowahi kuwasikiliza. Na shida kubwa katika hilo ni kwamba, ukirudia mawazo hayo kila siku, yanakuwa sehemu ya utambulisho wako wa maisha.
Kingine boss, imani zilizofichwa ndizo zinazoendesha maisha yako.
Hazionekani, lakini zina nguvu kuliko kila kitu unachokiona hii ni ajabu sana.

Goja nikuambie ukwel (REAL TALK)
Kama unaamini huwezi — hutajaribu.
Kama hujaribu — hutapata matokeo.
Na ukikosa matokeo — utaamini zaidi kwamba huwezi sijui unanipata ndugu yangu?.
Hapo ndipo wengi wanakwama: sio kwa sababu hawana uwezo, bali kwa sababu wameamua kujiamini vibaya ndani yao.

NGUVU YA KUBADILISHA MAWAZO
Ndugu, habari njema ni hii:
Mawazo yanaweza kubadilishwa.
Na ukibadilisha mawazo — taratibu unaingia kwenye safari ya kubadilisha maisha yako boss.
Sasa anza kwa kufuatilia mawazo yako kila siku:
Unapojikuta unafikiria hasi, jiulize: “Hii ni ukweli au ni imani tu?”
Badilisha kauli: badala ya “siwezi,” sema “najifunza.” nilipogundua hili hii ni moja ya siri ninayotumia siku hizi kwangu nimeamua kulitoa neno SIWEZI na kuweka SIJAJIFUNZA. Yaani, kama utaniuliza kitu ambacho sikiwezi kwa imani yako nitasema bado sijajifunza sababu vitu vyote tunajifunza boss.
Badala ya “itakuwa ngumu,” sema “nitatafuta njia.”
Hii siyo uchawi qma kukataa ukweli — ni nidhamu ya ndani boss.

NDUGU KUJIFAHAMU NI NGUVU.
Unapojitambua kwa kina Utakuwa na amani sana kwasababu:
Utajua nguvu zako halisi,
Unatambua udhaifu wako bila kuogopa,
Unachagua maisha yako badala ya kuishi kwa mazoea,
Hapo ndipo unapochukua usukani wa maisha yako mikononi mwako boss wangu.

KAMA UMEELEWA NA UPOSILIASI ANZA LEO.
Andika mawazo yako makuu ya kila siku (journal)
Tambua imani hasi unazozirudia.
Badilisha kauli zako kwa makusudi,
Jizungushe na watu na maudhui yanayokujenga mtandao wako ni muhimu sana boss.
Jipe muda wa kukaa kimya — sikiliza sauti yako ya ndani hapa ndo penye siri sasa bwana.

KUHITIMISHA NDUGU YANGU,
Maisha yako ya nje ni kivuli cha maisha yako ya ndani. Kwa ufupi ni kioo.
Ukibadilisha unavyofikiria — utabadilisha unavyoishi.
Usikubali kuendeshwa na imani ambazo hujachagua ndugu.
Chagua mawazo yako. Chagua maisha yako boss.

👉 WITO WANGU KWAKO NDUGU:
Leo, chagua wazo moja hasi unalolirudia mara kwa mara, na ulipinge kwanzia leo.
Badilisha kauli yako — na uanze kuandika upya hadithi ya maisha yako. Hakika hautabaki kama ulivyo. Wache leo niweke kalamu boss.

Share na mimi kupitia comment ulichojifunza. Ikiwezekana share na wengine ujumbe huu ili wajifunze pia.

Kujifunza tembelea,
https://addvaluetz.blogspot.com

#SelfAwareness (#Kujitambua). #Investment (#Uwekezaji). #PersonalDevelopment (#Maendeleobinafsi). #MigongoElias. #AddValueNetwork. #SeeYouNextLevel
+255767653697.

Popular posts from this blog

UKIJUA HILI KUHUSU WATU UTAFANIKIWA SANA.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29