HUJAWAHI KUSHINDWA, NI VILE HUJATAMBUA TU NGUVU ZAKO.

 


HUJAWAHI KUSHINDWA, NI VILE HUJATAMBUA TU NGUVU ZAKO.


Boss hivi unajua, watu wengi hutumia muda mwingi kufikiria udhaifu na mapungufu yao kuliko kutambua uwezo na  zao za kweli.
Mara nyingi utakuta wanajua:
wanachoshindwa kukifanya, wanapokosea,
na maeneo wanayodharika ndani yao.

Hata hivyo jambo la kushangaza ni kwamba:
Wengi hawajui kabisa nguvu zao halisi.
Na hii ndiyo sababu watu wengi wanaishi maisha ya kawaida wakati ndani yao kuna nguvu ya ajabu na uwezo mkubwa ambao haujawahi kugundulika wala kutumika kikamilifu boss wangu. Hili ni kosa ndugu.

SWALI LINALOKUJA HARAKA HARAKA NI KWAMBA. NGUVU YA KWELI NI NINI?
Swali zuri boss, nami ntakujibu,
Nguvu ya kweli si kitu unachoweza kufanya tu au kufanya kitu kwa nguvu kubwa hadi uchoke kabisa.

Nguvu ya kweli ni kile:  unachofanya kwa urahisi bila kutumia nguvu kubwa na bado kisikuchoshe bali kinakupa nguvu, furaha na unatamani kuendelea kufanya tu.
Ni kile kitu, unachokifanya bila kujilazimisha sana
Na watu wengine wanaona thamani yako kupitia hicho kitu boss.

Goja nikupe mfano boss, kuna watu:
wakizungumza wanavuta watu kusikiliza wao tu.
wakifundisha wanaeleweka kwa urahisi
wakiongoza watu wanawaunganisha naturally
wakitengeneza vitu wanakuwa wabunifu sana
Na mara nyingi wao wenyewe hawaoni kuwa hiyo ni nguvu yao kwa sababu kwao inaonekana “kawaida.” na wala hawashangai wala kujivunia.

Lakini tambua, kile kinachoonekana kawaida kwako kinaweza kuwa zawadi kubwa kwa wengine. Ni kama kale kamethal utupacho wewe kwake ni dhahabu.

Hapa boss tunapata swali lingine kuwa, JINSI YA KUTAMBUA NGUVU YAKO YA KWELI?

Jiulize kwa kina hivi:
1. Ni kitu gani unafanya bila juhudi au nguvu kubwa?
Kuna vitu wengine wanaviona vigumu lakini wewe unavifanya naturally kabisa bila jasho, nguvu wala juhudi yeyote boss.

Mfano inaweza kuwa:
kuzungumza mbele za watu, kushauri watu.
kuuza bidhaa, kuunganisha watu, kuandika,
kupanga mambo master plan, kuimba, kuchora, kuburudisha na mengine kibao boss.

Hapo kuna dalili ya nguvu yako ndugu.

2. Ni kitu gani kinakupa nguvu badala ya kukuchosha?
Kuna kazi nyingine mtu akifanya anachoka haraka.
Lakini kuna kazi nyingine ukifanya:
unasahau muda, unafurahia, unasahau hata kula an na  unajisikia hai zaidi boss.
Na hapo ndipo mara nyingi nguvu yako ya kweli ipo hapo.

3. Watu wanakushukuru kwa nini mara nyingi?
Boss Wakati mwingine dunia huona uwezo wako kabla hata hujauona wewe mwenyewe.
Mfano watu wakianza kukuambia:
“Unaelezea vizuri sana”
“Unajua kuhamasisha watu”
“Ukiongea tunapata matumaini”
“Una akili ya biashara”, unafarijigi sana.
“Una uwezo wa kusikiliza watu”, unashauri vizuri.
Usipuuze hayo maneno boss.
Mara nyingi hapo kuna kitu kikubwa ndani yako.

BoSS KUJUA UDHAIFU WAKO PIA NI HEKIMA
Sikiliza ndugu angu kujitambua si kujua nguvu zako tu.
Pia ni kujua:
maeneo yanayokurudisha nyuma,
tabia zinazokuharibu, vitu unavyoohangaika sana kuvifanya na unatumia nguvu kubwa sana.
na vitu vinavyokupunguzia uwezo wako boss.
Watu wengi wanaharibikiwa maisha si kwa sababu hawana uwezo bali kwa sababu hawaujui udhaifu wao haswa.

Mfano:
hasira kali, uvivu(ujue kunawatu ni wavivu hadi wanakera boss), kukata tamaa haraka. Hii mbaya sana.
kuahirisha mambo duh. hofu, mis use ya hela.
kushindwa kudhibiti hisia. Kupoteza muda.
kutegemea validation ya watu.
Ukijua udhaifu wako, utaanza kujilinda dhidi yake.

BOSS UKWELI NI KWAMBA.
Huwezi kufanikiwa kwa kuiga maisha ya watu wengine. wewe ni orginal si copy.
Mafanikio ya kweli yanakuja pale unapogundua: wewe ni nani,
Una nguvu/uwezo gani?
Na unatakiwa utoe thamani gani duniani?
Kuna watu wanahangaika kuwa watu wengine wakati nguvu yao halisi ipo sehemu tofauti kabisa boss.
Mfano tu , Samaki hawezi kushindana na ndege kwa kuruka.
Na ndege hawezi kushindana na samaki kwa kuogelea hii iko wazi boss.
Kila mmoja ana eneo lake la kung’aa na kutamba.

NGUVU YAKO NDIO MWELEKEO WAKO Halisi.
Hata hivyo nmegundua kuwa mara nyingi:
purpose yako,  mafanikio yako,
na mchango wako hapa duniani.
vinafichwa ndani ya nguvu zako za asili boss.

Ukianza kuishi kwenye eneo la uwezo wako:  utaona maana na kufurahia maisha zaidi.
utaongeza confidence
utaacha kuishi kwa kuiga wengine.
✔️ na utaanza kutoa thamani kubwa kwa watu wengine.

Ndugu yangu,
Kujifahamu si anasa wala ujinga.
Ni msingi wa maisha yenye direction.
Usitumie maisha yote kurekebisha kila udhaifu ulio nao huku ukisahau kukuza nguvu zako.
Kwa sababu: 👉 Udhaifu unaweza kukuzuia
Lakini
👉 Nguvu zako zinaweza kubadilisha kabisa maisha yako boss.

CHUKUA HATUA LEO
1. Andika vitu 3 unavyofanya vizuri naturally
2. Andika udhaifu 3 unaokurudisha nyuma
✅ Jiulize: “Nikitumia nguvu zangu vizuri, maisha yangu yanaweza kubadilika vipi?”

Elewa tu kuwa, Dunia haisubiri watu wakamilifu.
Dunia inahitaji watu wanaojitambua na kutumia uwezo wao kikamilifu.

Share na mimi kupitia comment ulichojifunza. Ikiwezekana share na wengine ujumbe huu ili wajifunze pia.

Kujifunza tembelea,
https://addvaluetz.blogspot.com/2026/05/level-za-mafanikio-sehemu-ya-nne.html

#SelfAwareness (#Kujitambua). #Investment (#Uwekezaji). #PersonalDevelopment (#Maendeleobinafsi). #MigongoElias. #AddValueNetwork. #SeeYouNextLevel
+255767653697. 

Popular posts from this blog