Posts

KAMA UNASAHAU MARA KWA MARA, SOMA HAPA KWANZA.

Image
  KAMA UNASAHAU MARA KWA MARA, SOMA HAPA KWANZA. Boss! Siyo  kila mara, kusahau ni ishara ya Ubongo dhaifu, mara nyingi ni namna tunavyojifunza ndugu. Nimekutana na watu wengi wakisema: "Mimi sina akili kubwa." Wengine "Kumbukumbu yangu ni mbaya." Mara "Ubongo wangu hauhifadhi vitu." Lakini ukweli ni kwamba, mara nyingi tatizo si ukubwa wa akili yako wala uwezo wa ubongo wako. Tatizo ni kwamba watu wengi hawajawahi kufundishwa jinsi kumbukumbu (memory) inavyofanya kazi boss. Sikia ndugu; Ubongo wa binadamu umeumbwa kwa ustadi mkubwa. Kazi yake si kuhifadhi kila kitu unachokiona au kukisikia, bali ni kuchagua filtering taarifa muhimu na kuacha zisizo muhimu wala matumizi. Kwa hiyo, kusahau si kasoro ya ubongo ni sehemu ya kawaida ya jinsi unavyofanya kazi. Hebu tuangalie sababu kuu zinazowafanya watu kusahau mara kwa mara. 1. Kukariri Bila Kuelewa (memorising without understanding). Hili ndilo kosa kubwa zaidi ambalo wanafunzi na hata watu wazima...

SIMULIZI YA KUSISIMUA KUHUSU “HATIMA YA KIMUNGU”. SEHEMU YA PILI.

Image
  SIMULIZI YA KUSISIMUA, “KUHUSU HATIMA YA KIMUNGU”. >>SEHEMU YA PILI.     Alipotazama nje kupitia dirish a aliona giza ambalo liliashiria kuwa ilikuwa ni usiku umeingia tena sio mawio bali usiku wa manane.    "Mamaaaaaaa!" alipiga kelele na hakuna anayesikia   na cha ajabu zaidi ni kwamba hata wale watoto watatu walionekana kuwa bize na kucheza kwa staili za midundo ambayo haikuwa inasikika. Kama hujasoma sehemu ya kwanza bonyeza hapa. Sasa inaendelea......    Elvine alizidi kuchanganyikiwa maana hakujua kama ni kweli anaona, anaota ama anaona maono. Alizidi kulia lakini hakuna aliyesikia kilio chake. Mlango aliuona upo mbali sana na nje pia aliogopa kutoka kwa lile giza nene. Aliamua kukimbilia mlangoni lakini hata nguvu za kufungua mlango hakuwa nazo akajikuta amekaa chini huku akitetemeka na kuwashangaa wale mabinti wageni.    "Eee Mungu nisaidie... eeh Mungu nisaidie mwanao" alijikuta akitamka maneno hayo kwa wo...

GHARAMA 5 ZA KUUFIKIA UKUU UNAOUTAKA.

Image
GHARAMA 5 ZA KUUFIKIA UKUU UNAOTAKA.   “Ukiona vya elea, ujue vimeundwa.” “Hakuna vya bure duniani.” “Mkono mtupu haulambwi.”   Hizi ni baadhi ya kauli ambazo zimeenea karibia kila kona ya dunia. Na lengo lake si kutukomoa au kutusema vibaya, laah hasha! Bali   ni kutaka kutuonyesha kuwa katika kuyafikia mafanikio tunayoyataka ni lazima tulipe gharama. Kumekuwa na kasumba ya watu wengi sana kutamanani mafanikio makubwa na kufika mbali sana katika maisha yao. Lakini pamoja na kutamani huko, asilimia kubwa ya watu bado kuufikia ukuu wanao utaka imekuwa ni gumuzo mtaani. Watu wengi wanatamani sana mafanikio ya baadhi ya watu maarufu na waliofanikiwa katika maisha yao au kutimiza ndoto zao. Na hapa wengi wamekuwa wadau na wapambe wa mafanikio ya watu waliofanya vizuri kwa nafasi zao. Wakati huo, huwa wanaona kama watu wengine wanabahati, wamezaliwa na na neema kuliko watu wengine, na mara nyingi wameyachukulia maisha kuwa ni simpo sana. watu wa namna hii, huchukulia mafan...

HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 1.

Image
 HATIMA YA KIMUNGU   SEHEMU YA 1.   Moto mkubwa ulikua unawaka juu ya maji, Elvine alizidi kusogea pale huku akistaajabu sana , na aliogopa sana " haaa! hivi inawezekanaje Moto uwake ndani ya maji ? au ndiyo ile muvi ya j ana inajirudia ila huu ni mwendelezo wake?"    "Hapana , sioti Mimi jamani... a u..... naota ?". Gha fla alishituka kutoka usingizini. Kumbe ilikuwa ni ndoto tu!, alijiuliza sana lakini, kwakuwa alikua ni mtoto aliipotezea na asubuhi alikua ameisahau ndoto ile.      Elvine alikuwa mtoto mdogo mwenye miaka 10. Na alikuwa akiishi na mama yake tu na hakuwahi kumfahamu   baba yake, w ala ndugu yeyote toka aanze kujitambua. Maisha yao hayakuwa ya shida sana bali yalikuwa ya kawaida tu .       Asubuhi aliamka akamsalimu mama yake ambaye alikuta kamuandalia chai ya maziwa mezani.   " Shikamoo mama! "    "Marhabaaaa El umeamkaje?"    " Kama kawaida yangu ni ...

Popular posts from this blog

UKIJUA HILI KUHUSU WATU UTAFANIKIWA SANA.

LEVEL ZA MAFANIKIO SEHEMU YA KWANZA.

MISINGI YA UWEKEZAJI SEHEMU YA PILI..