MISINGI YA UWEKEZAJI SEHEMU YA PILI..
MISINGI YA UWEKEZAJI SEHEMU YA PILI.
Watu wengi wanapoingia kwenye uwekezaji, kitu cha kwanza wanachofikiria sana ni FAIDA.
“Nitapata kiasi gani?”, “Faida itakuwa kubwa kiasi gani?” hii itanilipa ndani ya siku 5 n.k
Lakini ukweli ambao wawekezaji wengi wanafanikiwa wanauelewa ni huu:
Sio faida inaanza, ni USALAMA WA MTAJI WAKO unaobebwa kwenye kanuni ya kwanza ya KUFANYA UTAFITI kama tulivyojifunza.
Kusoma sehemu ya kwanza bonyeza hapa
KWANINI USALAMA WA MTAJI NI MUHIMU SANA?
Fikiria hili kwa umakini:
๐ Kama ukipata faida — unakuwa mbele na kufanikiwa zaidi.
๐ Ukipoteza mtaji — unakuwa umetoka kabisa kwenye mchezo, hadi ukajipange tena.
Huwezi kuendelea kuwekeza kama mtaji wako umekwisha itakubidi kujipanga tena.
Ndiyo maana wawekezaji wakubwa wanaanza na swali moja kuu:
“Ninaweza kupoteza kiasi gani hapa?”
Sio: “Nitapata kiasi gani?”.
Na kama utagundua kuwa kiasi cha pesa utakachopoteza kama mambo yataenda ndivyo sivyo ni kidogo au cha wastani basi Wekeza. Na kama utagundua ni kiasi kikubwa au chote basi chunguza na fikiria mara mbili mbili.
MAKOSA MAKUBWA AMBAYO WENGI HUFANYA, ni kwamba watu wengi: Huona opportunity fursa.
Husikia ahadi za faida kubwa na,
Huchukua hatua haraka bila kuchunguza.
๐ Matokeo yake: Wanatapeliwa, Wanapoteza pesa, Wanajuta baadaye kusema siwezi kurudi tena kufanya biashara hii, hili ni kosa boss.
Kwa nini?
๐ Kwa sababu waliweka macho kwenye chambo cha FAIDA wakasahau USALAMA.
Kuna kanuni muhimu katika uwekezaji ambayo ni “SAFETY FIRST” yaani, usalama kwanza.
Kabla hujawekeza hata shilingi moja, jiulize maswali haya:
1. Je, mtaji wangu uko salama kiasi gani?
Je, hii biashara ina uhalali?
Je, naelewa inavyofanya kazi?
Je, kuna hatari gani zilizofichika?
2. Ikiharibika, nitapoteza kiasi gani?
Je, ni pesa ambayo naweza kuhimili kuipoteza?
Au ni pesa ambayo itanivuruga kabisa kifedha?
3. Je, nimefanya utafiti wa kutosha?
Au nimeingia kwa sababu ya kusikia tu?
Au kwa sababu watu wengine wanafanya?
Ujue watu wengi hufanya vitu kwa mkumbo boss!
Wallen Bufet moja kati ya wataalamu wengi katika sayari ya uwekezaji anasisitiza kanuni kuu mbili katika hili ambazo ni:
1. USIPOTEZE PESA
Hii ndiyo sheria kuu.
2. ZINGATIA KANUNI NAMBA 1
Hakikisha unalinda mtaji wako kabla ya kufikiria faida.
UKWELI AMBAO WENGI HAWAPENDI KUSIKIA
๐ Uwekezaji siyo mchezo wa kubahatisha.
๐ Sio kila fursa ni fursa nzuri.
๐ Sio kila kinachoonekana kina faida kina usalama ndani yake.
Wakati mwingine:
Kutoingia kwenye uwekezaji fulani ni FAIDA YENYEWE.
MOJA YA BUSARA ZA UWEKEZAJI NI HII,
Badala ya kuuliza: “Nitaongeza pesa zangu vipi?”
Anza kuuliza: “Nitalindaje pesa zangu kwanza?”
๐ Hii inabadilisha kabisa maamuzi yako.
HEBU GOJA NIKUPE MFANO KIDOGO RAHISI WA KUELEWA NDUGU YANGU
Hebu fikiria una milioni 1 yes 1M:
Ukiwekeza na kupoteza yote → hapo unarudi sifuri. Lakini,
Ukiwekeza na kulinda mtaji → una nafasi ya kujaribu tena.
๐ Ndiyo maana kulinda mtaji ni msingi wa pili wenye nguvu.
NAONA NIMESEMA SANA, SASA KWA KUMALIZIA NDUGU YANGU.
Tafadhari, Usiwe mwekezaji wa hisia.
Usiwe mwekezaji wa kusikia, na kufuata mkumbo.
Kuwa mwekezaji wa:
maarifa, uchambuzi, tahadhari.
Yaaani nasema, LINDA MTAJI WAKO KWANZA, FAIDA ITAFUATA.
Kwako msoma,
Kabla ya uwekezaji wako unaofuata, jiulize:
“Je, hapa ninalinda pesa yangu… au ninaweka matumaini tu?”
Jibu lako ndilo litakaloamua hatma ya fedha zako.
Share na na mimi kupitia comment. Ikiwezekana share na wengine ujumbe huu ili wajifunze pia.
Kujifunza tembelea,
https://addvaluetz.blogspot.com
#SelfAwareness (#Kujitambua). #Investment (#Uwekezaji). #PersonalDevelopment (#Maendeleobinafsi). #MigongoElias. #AddValueNetwork. #SeeYouNextLevel
+255767653697.
