Posts

Showing posts from May, 2024

MAAJABU YA AKIBA

Image
MAAJABU YA AKIBA Akiba (saving) ni kiasi cha fedha au rasilimali ambacho kimewekwa kwa matumizi ya baadaye, hata sasa kingeweza kutumika lakini umuhimu wake kwa kutumika baadaye ni mkubwa kuliko matumizi yake ya sasa. Hata katika biblia ``Mwanzo 41:35-36`` kama umewahi soma utaona Farao baada ya kutafsiriwa ndoto yake na kufahamu kuwa, imempasa kuweka akiba alilifanya hilo kwa uharaka ili kuhakikisha linaendelea vizuri ndio akamweka Yusufu kama msimamizi wa hili. Farao aliona kabisa kuwa nidhamu yake ya kujiwekea akiba haipo sawa hivo alihitaji msaidizi wa kumsaidia kama yeye alivyokuwa ndivyo tulivyo baadhi yetu siku za leo hatuwezi kujiwekea akiba ya vile tulivyo navyo. yaani huwa tunapenda kusema kesho itajisumbukia yenyewe,  Hata hivyo tangu zamani hata leo mataifa mbalimbali yamekuwa yakijiwekea akiba kwa manufaa na matumizi ya baadaye. Ukiangalia nabii Samweli alikuwa akijiwekea akiba na aliitoa pale Sauli alipomtembelea wakaila ile akiba ya chakula. Ni muhimu kujiw...

KWANINI UNAHITAJI PESA.

Image
  KWANINI UNAHITAJI PESA? Tunaishi kwenye dunia ambayo karibia kila kitu kina hitaji pesa. Chakula, maradhi, nguo na mengine kibao. Kama utaniazima dakika mbili za kusoma hadi mwisho ujumbe huu? Zitakuwa ni dakika 2 za matumizi bora kabisa ya muda kwenye maisha yako. Huta jutia bundle, muda wala nguza zako. Mara nyingi watu wakija kupata ushauri kwangu, kuhusu kupata pesa huwa siwajibu Kama walivyouliza. Wengi wao huuliza hivi, Mwl. nifanyaje ili nipate fedha zangu mwenyewe? Kama nilivyosema swali hili huwa silijibu kama lilivyo kusudiwa na waulizaji. Nami huwajibu kwa kuwauliza swali; KWANINI UNATAKA PESA? Kwa  bahati mbaya sana wengi huwa hawana majibu ya kueleweka ya swali hili. Wengine huseme ili nitumie tu, ili niinjoy maisha n.k. Nafahamu kabisa kuwa hata wewe unataka pesa. Ndiyo maana umeajiriwa, unafanya kazi, unakaba roba, unaomba, unalima n.k  moja ya sababu kubwa ya kufanya hivyo ni ili upate pesa. Si ndiyo rafiki!? Kama ndiyo napenda kukuuliza na w...

THANK DIFFERENT (FIKIRI TOFAUTI).

Image
  * THINK DIFFERENT"  (FIKIRI TOFAUTI) * . Ilikuwa kampeni kali na ya kuvutia iliyozinduliwa na Apple Computer ( Apple ) mnamo 1997. Kama ulikuwa umezaliwa tupungianešŸ«· Ilidumu kwa miaka kadhaa na bado inachukua hatamu katika historia ya uuzaji na utangazaji.  Think Different"  ilikuwa na mafanikio makubwa. Ilisaidia Apple kujionyesha kama chapa kwa ajili ya watu wenye * UBUNIFU, * na wanaofikiri tofauti. kampuni iliyounga mkono ubunifu na kutofuatana na desturi za kawaida. Kampeni hiyo haikuzidisha mauzo tu bali pia ili kuza picha ya Apple kama chapa nzuri na inayotamaniwa na wengi. Hata wewe ni shahidi tukizungumza kuhusu, apple na huduma zake. " * Think Different" *   ni zaidi ya maneno tu; ni * FALSAFA. * kali. "Ni kuhusu umuhimu wa kufikiri bila kutegemea Mwawzo ya wengine, kupinga hali ilivyo, na kuamini kuwa watu binafsi wanaweza kuleta mabadiliko makubwa sana duniani." Rudia kusoma tena. Ndugu, kufikiri tofauti ni chanzo cha maba...

HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 26.

Image
  HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 26. Ilipoishia.......... Alipomgeuza tu alishangaa kuona sura ya yule binti ni ya mbuzi. Aliogopa na kudondoka chini kwa kelele kuu alilia 'maaamaaaaaaa!!!!" Alijiokotaokota huku akiangukaanguka mpaka kwenye gari yake. Alipanda ndani ya gari na kuwasha gari. Alikimbiza gari mpaka akafika karibu na geti la nyumba ya Elvine, lakini kabla hajafika getini alishangaa kuona anaguswa mabegani ndani ya gari lake. Alitoa macho kwa uoga na mshtuko mkubwa mpaka akakosea njia na kwenda kugonga mti... Kusoma sehemu ya 25 bonyeza hapa. Sasa inaendelea......, Aligonga mti kwa nguvu mpaka naye akajipigiza kichwa kwenye usukani wa gari na gari ikaharibika sana upande wa mbele, alipona kwa neema tu kwa namna gari ilivyokuwa mwendo kasi angeweza hata kupoteza maisha lakini haikuwa hivyo. Alijikaza na kushuka kwenye gari akakimbia kuelekea kwenye nyumba ya Elvine,  njiani alikumbwa na kimbunga cha ajabu sana. Baada ya kile kimbunga kumpitia na kumzingazinga kwa muda ...

HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 25.

Image
  HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 25. Ilipoishia...... "Ooh asante YESU maneno yako yamenipa na kiburi juu ya hawa watu, sahizi siwaogopi na wala hawaniwezi na Elvine lazima arudi haijarishi kwa namna gani? Nataka nimpe Mungu Sababu ya kumsaidia Elvine" Elimina akafuta machozi na akawa kajua aombe nini kwa sasa maana hataomba tena maombi ya kulalamika na maombi ya kwanini!! Akatabasamu alafu akasema " SASA VITA IANZE NAJUA SILAHA YANGU... Kama hujasoma sehemu ya 24 bofya hapa. Sasa inaendelea.... Elimina baada ya kujipa moyo akapata kiburi mbele ya hao maadui zake maana alijua umuhimu wake katika kumlinda Elvine. Aliamua kutoka pale ndani na kufuta machozi yake na akajisemea sasa sitalialia tena nimaombi ya vita mwanzo mwisho.  Aliamua kutoka na kwenda dukani kwake ili kuendelea na kazi zake. Ilikuwa imepita wiki sasa pasipo yeye kufika dukani kwake hivyo hata wateja walipungua maana kila walipokuja hawakumkuta. Alifungua duka lake akakaa nje ya duka mpaka jioni, japo alipat...

HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 24.

Image
HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 24. Ilipoishia.... " Baba nimeshakwambia, ufalme wa hawa wenzetu unanguvu kuliko sisi. Huoni mpaka sasa Elvine tunae, lakini bado mtu mmoja tu huko duniani anasababisha tusikamilishe mambo yetu?.  Hili swala linaniuma sana kuona tunafeli mbele ya hawa watu. Yaani kumpata Elimina sio kazi nyepesi, maana analindwa mno na ufalme wake na anamsimamo sana yule mwanamke.  Ila mimi nakuahidi baba naenda kumuangusha na akianguka, atalipia haya yote aliyoyafanya kwenye ufalme wa giza nasema atalipia, tena naapa ntafanya ajute na ajute tena labda asijichanganye" Erijini (Erika), aliongea kwa uchungu na hasira mpaka macho yakageuka rangi na kuwa rangi ya bluu.... Kusoma sehemu ya 23 bofya hapa. Sasa inaendelea.........  Efraim hakutaka kubishana sana bali aliamua kufanya sawasawa na hitaji la binti yake. Erijini alitoweka na kurudi Duniani kutoka kwenye ardhi iliyomficha Elvine Kwa kazi moja kubwa ya kumuangusha Elimina.  Elimina alikuwa haachi kuomba...

Popular posts from this blog

NJIA 7 ZA KUOSHA UBONGO WAKO.

VITU 9 MUHIMU KWA MTU YEYOTE KUJIFUNZA KWENYE MAHAFALI.

SIRI ILIYOPO NYUMA YA TABASAMU.