Posts

Showing posts from June, 2024

HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 31

Image
  HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 31 Ilipoishia………. Elvine alipoteza amani kuliko hata mkewe maana kila alipomtazama mkewe basi moyo wake ni kama ulikuwa unachomwa na mwiba uliojishikiza huko kwenye mishipa ya moyo. Nafsi yake ilitaabika na ndipo alipoamua kutafuta muda mzuri, baada ya chakula cha jioni, azungumze na mkewe, maana ule ukimya wa siku mbili ulikuwa adhabu kubwa sana kwake. Kusoma sehemu ya 30 bonyeza hapa Sasa inaendelea………. Elimina mamy naomba kujua kwanini hutaki kuniuliza kuhusu sababu ya haya yote? Maana najua unajua kuwa kuna mahali mimi nilikosea, sasa unapokaa kimya hivyo… kiukweli unazidi kunichanganya maana ni kama hutaki kujua, sasa unadhani mimi roho yangu itatulia kweli?. Hata kama ungekuwa wewe lazima usingepata amani, ungekuwa hata unawaza hivi nakuwaziaje, nakuonaje na ninajisikiaje ninapokuona, sasa kwanini wewe umekaa kimya, sema neno tafadhali? (Elvine alikuwa akiongea bila kumtazama mkewe usoni maana moyo wake haukuwa katika hali ya utulivu). Pamoja na ...

MISINGI MITATU YA MAFANIKIO

Image
  MISINGI MITATU YA MAFANIKIO Hakuna mtu asiye penda mafanikio, lakini ni wachache tu hufanikiwa. Leo tutaangalia Jambo hili kwa mapana zaidi. Hili ni somo muhimu kuwahi kutokea.. Na mara baada ya kusoma hapa, utabadili fikira zako juu ya mafanikio. Utajua kwanini wengine huwa ni ngumu sana kufanikiwa hata kama ni wapambanaji. Utafahamu njia na kanuni sahihi za kufanikiwa kwako. Na mengine mengi....... Siku za nyuma kidogo, nilimtembelea rafiki yangu. Ambaye ilipita miaka mingi hatujaonana, kwa namna yake amepiga hatua katika mafanikio haya ya mwili. Tulijikumbusha mambo ya nyuma, kwa namna ambavyotuliishi, kwa kweli tulifurahi sana. Kwani kila mmoja alikuwa connected aseee. Ilikuwa special day ukilinganisha na kwamba ni miaka mingi hatukutiana machoni ingawa tulikuwa tunawasiliana. Bwana tuliongea vitu vingi na tulifurahia sana asee. To cut the story short, ilibidi tuanze kuulizana mambo ya point, kujitathimini na kujenga... Kama kawaida yangu nilikuwa na maswali meng...

MAMBO MATATU (03) YA KUEPUKA KWENYE MAISHA YAKO.

Image
  MAMBO MATATU (03) YA KUEPUKA KWENYE MAISHA YAKO. U hali gani ndugu msomaji wa addvaluenetwork! Nikukaribishe tena upate kujiongezea thamani yako kwenye maisha yako. Leo tunaenda kuangali vitu vitatu ambavyo hupaswi kuvidekeza kabisa kwenye maisha yako. Kwani vitu hivi vimekuwa ni kikwazo katika mafanikio ya watu wengi sana. Si unajua wengi wanatamani kusonga mbele na kufanikiwa lakini kwa kujua au kutokujua wamekuwa na tabia fulani ambazo badala ya kuwapeleka mbele zina wabakiza palepale na kuwavuta nyumaa. Hii ni changamoto kwa wengi. Ndiyo maana nimeamua kuzungumza hili na unapaswa kujitenganayo kabisa. Wacha nikupongeze kwa kuwa umepata nafasi hii ya kusoma hapa, kwani hutabaki kama ulivyo. Nami nikuahidi kuwa hujapoteza, hutajutia na utajishukuru kwa kusoma hadi mwisho leo. Wacha tuyaangalie Sasa........ JAMBO LA KWANZA:  TABIA YA KUMLAUMU (BLAMING HABIT). Tabia hii si nzuri hata kidogo. Kuna watu ni wazuri sana wa kulaumu, yaani kosa kidogo atalaumu kweli. A...

JE NI NANI UMWAMBIE MIPANGO NA NDOTO ZAKO ZA MAISHA?

Image
  JE NI  NANI UMWAMBIE MIPANGO NA NDOTO ZAKO ZA MAISHA? Kijana mmoja mdadsi, ambaye Ilikuwa ni kawaida yake kujiuliza na kudadsi vitu katika uhalisia wake. Na hufanya hivi kwa kujiuliza yeye au kuwauliza watu wengine... Ngoja kwanza nimwambie, dakika tano za kusom ujumbe huu hadi mwisho zinaenda kuchukua sura mpya ya maisha yako. Sasa wacha tuendelee, Siku moja kijina huyo alimuuliza baba yake ambaye alikuwa  mvuvi. Baba hivi ni sawa mimi kuwaambia watu malengo, na ndoto zangu kubwa? Yule mvuvi akanyamaza kwa muda kisha akauliza. "Kwa nini unataka kujua hivyo?" Bila shaka huyu mvuvi alikuwa Mtanzania  nahisi😁 Kijana akajibu, "Sawa, baba, nina ndoto nyingi kubwa, tena kubwa sana! Nataka kuwa mtu mwenye mgoso na athari chanya katika kizazi changu na nyanja zote za maisha. Lakini, sijui niseme au nisiseme kwa watu kuhusu ndoto hizi nilizo nazo." Mvuvi akatabasamu kisha akasema, "Unajua nini... twende tukavue samaki mtoni. Kisha, tutaendelea na mazungu...

AKILI NNE (04) ZA KUKUFAN

Image
  AKILI NNE (04) ZA KUKUFANIKISHA KATIKA MAISHA YAKO. Kuwa na akili, hekima na maarifa  ni jambo ambalo kila mtu hulitamani sana. Kitu hiki ni kizuri sana lakini ni wachache tu hufanikiwa kuwa nalo. Akili na hekima mara nyingi zimekuwa nyenzo mhimu sana katika kuyaendea mafanikio ya mtu. Kwa kuwa vitu hivi ni muhimu sana kuwa navyo, hivyo ni muhimu tukajifunze akili nne zitakazo tusaidia kufanikiwa katika maisha yetu. Goja tujifunze kupitia maandiko haya kwanza; MITHALI 30:24-28 [24]Kuna viumbe vinne duniani vilivyo vidogo; Lakini vina akili nyingi sana. [25]Chungu ni watu wasio na nguvu; Lakini hujiwekea chakula wakati wa hari. [26]Wibari ni watu dhaifu; Lakini hujifanyia nyumba katika miamba. [27]Nzige hawana mfalme; Lakini huenda wote pamoja vikosi vikosi. [28]Mjusi hushika kwa mikono yake; Lakini yumo majumbani mwa wafalme. Naam, kuna jambo kubwa sana nataka ulifahamu, kwani linaweza kuleta sura mpya katika maisha yako Soma uelewe......... Kama umesoma k...

VITU 9 MUHIMU KWA MTU YEYOTE KUJIFUNZA KWENYE MAHAFALI.

Image
VITU 9 MUHIMU KWA MTU YEYOTE KUJIFUNZA KWENYE MAHAFALI. Ilikuwa tarehe 25052024 Nilipata nafasi ya kuhudhuria, tukio la mahafali ya kuwaaga wahitimu wa Casfeta tayomi Chuo kikuu Mzumbe.  Iliyofanyika katika ukumbi wa Professor Kuzilwa uliopo Mzumbe Morogoro Tanzania. Shughuli ilifaana sana, tulikutana na jamaa, ndugu, rafiki na watu kibao. Pia tulifurahi, tulijifunza, tulikula n.k Baada ya siku chache kupita, wadau na marafiki kadhaa nilipo kutana nao walisema; Mwl. nilikuona kwenye sherehe!. Nami kujibu ndiyo nilikuwepo, Ilikuwa nzuri sana. Wengi waliuliza kuwa, kwanini hadi sasa hujasema chochote mwl? Ukwel mtupu, sikupanga kuandika chochote. Lakini kwasababu ya maswali mengi nikaona kunahaja ya kuzungumza.  Ukweli ni kwamba kuna mambo mengi sana nilijifunza kwenye shughuli hiyo. Laikini pia kuna mambo mengine  ambayo mtu yeyote anaweza kujifunza kwenye mahafali na matukio yafananayo na hilo: Na hapa naenda kukushirikisha mambo 9 muhimu ambayo mtu yeyote anawez...

Popular posts from this blog

MAAJABU YA AKIBA

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.