LEVEL ZA MAFQNIKIO (SEHEMU YA PILI)..

 


LEVEL ZA MAFANIKIO SEHEMU YA PILI.

Baada ya kutoka kwenye Hatua ya kujikimu/utumwa (Slavery/survival  Level). Ambapo mtu anakuwa anapambana na mahitaji ya msingi nq hapo kipato chake kina weza kuwa ni kidogo au sawa na mahitaji yake.

Kusoma sehemu ya kwanza bonyeza hapa

Sasa hatua hii ni ya kuanza kujitegemea
Mtu anaanza kuwema;
“Siwezi kuendelea kuuza muda wangu milele lazima nijitengenezee mfumo wangu.”

Na hapo ndipo anaingia hatua ya pili: HATUA YA
KUJIAJIRI/ KUJITEGEMEA(SELF-EMPLOYMENT LEVEL)
HII NI LEVEL YA KUAMKA
Hapa mtu: Anaanza kujitegemea
Anaanza kujitengenezea kipato chake
Anaanza kutumia ujuzi wake moja kwa moja
๐Ÿ‘‰ Anaacha kutegemea mshahara pekee
๐Ÿ‘‰ Anaanza kujitafutia njia zake mwenyewe

KWA MFANO HALISI WA HII LEVEL
Hapa ndipo utakuta:
Fundi anajifungulia gereji yake,
Mwalimu anaanza tuition zake,
Mjasiriamali mdogo anaanza biashara zake.
Writer anaanza freelancing.
๐Ÿ‘‰ Hapa unaanza “kumiliki kazi yako boss”.

UKWELI Kuhusu  HII LEVEL
Ingawa inaonekana ni hatua kubwa kwasababu na wewe unakuwa na kaofsi kako.

Hapo bado unaendelea kubadilisha muda wako na pesa.
๐Ÿ‘‰ Ukifanya kazi → unapata
   Usipofanya → hakuna kipato
Tofauti na level ya kwanza ni:
๐Ÿ‘‰ Sasa una uhuru kidogo
Lakini bado umefungwa na muda wako, lakini pia, hapa unakuwa unamiliki kazi yako moja kwa moja boss.

FAIDA KUBWA ZA HII LEVEL
Hii hatua ina nguvu sana kama ukiielewa vizuri:
1. UHURU (FREEDOM)
Unaamua muda wako,
Unaamua nini ufanye.

2. MAPATO YANAYOWEZA KUONGEZEKA
Tofauti na mshahara wa kudumu, hapa unaweza:
kuongeza wateja
kuongeza bei
kuongeza kipato, kama utaweka bidii na mikakati boss.

3. UJENZI WA BRAND
Hapa watu wanaanza kukujua kwa kile unachofanya kwa jina lakoo.

TATIZO KUBWA LA LEVEL HII,
Hapa ndipo wengi wanakwamia hapa:
1. WEWE NDIO KILA KITU
Boss, Mfanyakazi, Mhasibu, Marketing. Yaani, wewe ndo top top.
๐Ÿ‘‰ Ukichoka — kila kitu kinasimama.

2. KUCHOKA HARAKA (BURNOUT)
Unajikuta: unafanya kazi masaa mengi sana,
bila mfumo,
bila mapumziko.

3. KUKOSA MFUMO
Watu wengi hapa: ๐Ÿ‘‰ wanafanya kazi, lakini hawajengi mfumo wa biashara
Mdugu yangu KOSA KUBWA SANA KATIKA LEVEL HII
Wengi wakifika hapa: Wanajisikia wamefika
Wanaacha kukua na kuwekeza kwao wenyewe.
๐Ÿ‘‰ Wanakomaa hapo hapo.

Wanasahau kwamba: HII SIYO MWISHO — NI HATUA TU boss.

NAMNA YA KUTOKA LEVEL HII KWENDA JUU ZAIDI
Kama upo hapa, fanya haya:
1. ANZA KUJENGA MFUMO
Usifanye kila kitu wewe peke yako.

2. JIFUNZE KUGAWA KAZI (DELEGATION)
Anza kuwashirikisha wengine. Unajua kunawatu wanataka kufanya kila kitu wao wanaogopa kuwaamini wengine kwamba wataibiwa. Ndugu yangu kama unataka kwenda mbali jifunze Deligation mapema huko mbele kutakishinda oohoo.

3. BADILISHA MTAZAMO
Usifikirie tu:
“Nitafanya kazi vipi?”
Anza kufikiria:
“ kivip Nitajenga mfumo unaofanya kazi bila mimi?” yaani, fikiria kuhusu timu boss.

4. JENGA BRAND YAKO
Hii ndiyo itakuvusha kwenda level inayofuata. Fanya kwa uaminifu na kwa mwendelezo ili kufahamika kwa kile unachofanya.

SASA HEBU TUONE UTAJUAJE KAMA UPO LEVEL HII?
Jiangalie kama: Unapata pesa kupitia ujuzi wako moja kwa moja,
Ukiacha kufanya kazi kipato kinasimama.
Unafanya kila kitu mwenyewe.
๐Ÿ‘‰ Kama ndiyo, upo hapa. Lakini kama siyo tutacheck level zingine.

Ndugu yangu muhimu kuzingatia ni kwamba,
Hii ni hatua ya: kujifunza kujitegemea,
kujenga msingi wa biashara,
kuanza kuona uwezekano mkubwa.
Lakini pia: Usibaki hapa.
Kwa sababu:
๐Ÿ‘‰ Uhuru wa kweli hauji kwa kujiajiri pekee bali,
๐Ÿ‘‰ Unakuja pale mfumo unapoanza kufanya kazi bila wewe na kwa niaba yako.

Kwakumalizia ni kwamba,
“Usijenge kazi tu,  jenga mfumo.” utakao kusaidia kusimama badala yako boss.  Ndugu kwaleo goja niishie hapa tutaendelea tena wiki ijayo.

Share na mimi kupitia comment ulichojifunza. Ikiwezekana share na wengine ujumbe huu ili wajifunze pia.

Kujifunza tembelea,
https://addvaluetz.blogspot.com/2026/04/misingi-ya-uwekezaji-sehemu-ya-tatu.html

#SelfAwareness (#Kujitambua). #Investment (#Uwekezaji). #PersonalDevelopment (#Maendeleobinafsi). #MigongoElias. #AddValueNetwork. #SeeYouNextLevel
+255767653697.

Popular posts from this blog

UKIJUA HILI KUHUSU WATU UTAFANIKIWA SANA.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29