MISINGI YA UWEKEZAJI (SEHEMU YA TATU): FAIDA (RETURN).
MISINGI YA UWEKEZAJI (SEHEMU YA TATU): FAIDA (RETURN).
Katika safari ya uwekezaji, kuna mlolongo ambao haupaswi kuvunjwa kabisa kama unataka kupata matokeo halisi. Uwekezaji siyo bahati nasibu wala ubabaishaji, bali ni mfumo unaofuata kanuni maalum zilizowekwa boss.
Kama tulivyoona hapo awali:
Hatua ya kwanza ilikuwa kufanya utafiti wa kina (research).
Hatua ya pili ilikuwa kulinda pesa/mtaji wako (capital protection).
Kusoma sehemu ya pili bonyeza hapa
Na leo nataka nikupeleke kwenye kipengele pendwa, ambacho watu wengi hukikimbilia kwanza bila kufuata misingi. Si kingine bali ni FAIDA (RETURN).
Ukweli ni kwamba: Kila Mwekezaji Anatafuta Faida.
Hakuna mtu anayeweka pesa zake kwa lengo la kupoteza. Kila uwekezaji una lengo moja kuu: kuongeza THAMANI ya FEDHA yako boss.
Lakini pamoja na hayo, hapa ndipo wengi hukosea,
Wanaanza kwa kuuliza:
“Nitapata faida kiasi gani?”
Badala ya kuuliza:
“Je, huu uwekezaji ni salama? Na umechunguzwa?”
Najua unaweza kujiuliza fida Sahihi Ni Ipi? Swali lako ni zuri boss wagu, na mimi nitakujibu kama ifuatavyo;
Kwa uwekezaji wa muda mrefu, faida inayokubalika kitaalamu mara nyingi huwa:
10% – 13% kwa mwaka → hii ni faida yenye afya na endelevu kabisa tajiri. Hapa ni sawa na kusema ukiweka milioni 10 utapata milion 11 baada ya mwaka.
Faida ya 20%, 50%, 80%+ → inawezekana na ni nzuri sana, lakini inahitaji uchunguzi mkubwa zaidi boss.
⚠️ Kumbuka:
Faida kubwa sana mara nyingi huja na hatari kubwa sana pia.
Kipimo muhimu: Ni mfumuko wa Bei (Inflation)
Huwezi kusema umefaidika kama pesa yako inaongezeka kwa asilimia ndogo kuliko mfumuko wa bei.
Kwa mfano: kama inflation huo mfumko wa bei ni 5% – 8% (kama ilivyo mara nyingi Tanzania)
Na wewe unapata faida ya 4%, basi kwa uhalisia umepoteza thamani ya pesa yako boss.
๐ Hivyo: Faida yako lazima izidi inflation ili uwe kweli unakua kifedha tajiri.
Ndugu yangu kuna aina Kuu Mbili za Faida (Return).
1. Ongezeko la Thamani (Capital Gain).
Hapa mali au uwekezaji wako unaongezeka thamani kadri muda unavyokwenda.
Mfano: Ardhi, nyumba, Hisa, biashara, mazao.
๐ yaani, unanunua leo kwa bei fulani, baada ya muda unauza kwa bei kubwa zaidi.
2. Gawio (Cash Flow / Dividend)
Hapa unapata mapato ya mara kwa mara kutokana na uwekezaji wako.
Mfano: hisa zinazolipa gawio, Biashara,
Nyumba za kupangisha n.k
๐ Unapata kipato kila baada ya muda (mwezi, miezi 3, 6 au mwaka).
Ndugu yangu, kanuni Muhimu Sana ni kwamba, Usianze na Faida.
Hii ndiyo kosa kubwa ya watu wengi.
Et wakishasikia na kuona:
“Weka 50,000 upate 300,000 ndani ya wiki moja”
Wanavutwa na tamaa ya faida bila kujiuliza:
Hii biashara ipoje?, Inazalishaje pesa?, Ina uhalali?, Mtaji wangu uko salama?
๐ Matokeo yake: wanapoteza pesa, halafu ujue unauma ndugu yangu.
Sasa sikiliza boss, mpangilio Sahihi wa Uwekezaji (Golden Order) ni huu;
1. Fanya Utafiti wa Kina, kuhusu huo uwekezaji.
2. Hakiki Usalama wa pesa/Mtaji Wako.
3. Kisha Angalia Faida sasa boss.
Ukibadilisha mpangilio huu:
➡️ Utaanza na faida → utaishia hasara.
Goja nikupe tahadhari muhimu Sana boss, ambayo ni kwamba,
Baadhi ya miradi au “fursa” zisizo halali hutumia:
๐ Faida kubwa kama chambo
Ili: Kukuvutia, Kukuharakisha, Kukufanya usifikirie
⚠️ Hapo ndipo wengi huingia mkenge sasa.
Nataka nihitimishe kwamba, uwekezaji siyo mchezo wa tamaa, huu ni mchezo wa akili boss.
๐ Mwekezaji makini:
Huchunguza kabla ya kuamini,
Hulinda kabla ya kutafuta,
Hufikiria kabla ya kuwekeza. Namuomba mungu na wewe uqe mwekezaji wa akili.
Kitu cha kuzingatia ni kwamba,
“Usikimbilie faida kabla hujalinda mtaji,
Kwa sababu faida inaweza kuchelewa, lakini hasara huja haraka boss.”
Share na mimi kupitia comment ulichojifunza. Ikiwezekana share na wengine ujumbe huu ili wajifunze pia.
Kujifunza tembelea,
https://addvaluetz.blogspot.com
#SelfAwareness (#Kujitambua). #Investment (#Uwekezaji). #PersonalDevelopment (#Maendeleobinafsi). #MigongoElias. #AddValueNetwork. #SeeYouNextLevel
+255767653697.
