Posts

Showing posts from April, 2023

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29

Image
  Nashukuru kwa kushiriki nami link ya Hadithi hii tamu na Nzuri ya Hatima ya Kimungu Sehemu ya 29. 🙏 Nilichosoma katika sehemu hii, simulizi imeendelea  kwa mvuto mkubwa sana – linaonyesha mapambano ya ndani ya Elvine kati ya imani yake, hofu yakuwaza kumpoteza mkewe Elimina, na hatia ya makosa ya zamani. Kuna mambo yafuatayo nimeona  yaliyobeba msingi   wa  sehemu hii: 1. Mgongano wa nafsi ya Elvine 👉Anapokuwa mbele ya Malaika Elvila, anatakiwa kufanya maamuzi magumu: kati ya mke na mtoto. 👉Uamuzi wake unaonyesha upungufu wa mwanadamu, uchungu, na jinsi maumivu yanavyoweza kuathiri fikra na maamuzi. 2. Adhabu na Neema 👉Kupotea kwa mtoto na kutozaa tena kwa Elimina ni matokeo ya makosa ya Elvine, lakini bado neema ya Mungu inaonekana kwa kumrejesha mkewe. 👉Malaika anamkumbusha kuwa Mungu si mkatili, bali anamfundisha kupitia mateso na changamoto. 3. Ugeuzi wa Maisha (Turning Point) 👉Elvine sasa anaitwa kuwa mchungaji wa kondoo wa Bwana, ishara ...

EPUKA KUJILINGANISHA NA WATU WENGINE BADALA YAKE FANYA MAMBO HAYA.

Image
  FANYA MAMBO HAYA KUEPUKA KUJILINGANISHA NA WATU WENGINE. Tunaishi kwenye dunia ambayo kuona au kufahamu hatua, maendeleo na mafanikio ya watu wengine ni rahisi sana. Hali hii imefanywa kuwa rahisi kutokana na kuwepo kwa mitandao na intanet.  Kupitia mitandao unaweza kujua, mtu fulani anawaza nini, anapenda nini, yupo katika kipindi gani na mengine mengi sana.  Ulisha wahi kuona mtu anaamka asubuhi tu anapost mtandaoni, hivi ndivyo naamka sasa, akipiga mswaki anapost, akianza kutumia chai anapost, akila chakula cha mchana anapost, akienda kutembea sehemu anapost, akitumiwa ujumbe wa kupongezwa au kusifiwa anapost, akutumiwa hela anapost, akisaidia watu anapost, akiachwa anapost, akikorofishana na mtu anapost, akitumia chajio anapost, akiwa anaangalia muvi anapost, akienda kulala anapost na hapo anaweza kupost hadi alichoota kwenye ndoto akiwa amelala.  Huko status utakuta imejaa yaani, ni full kupost. Naomba tuelewane vizuri hapo si kwamba nakataa kupost noo! Tena...

MUDA WA KUINGIA NA KUTOKA (ENTRY AND EXIT TIME).

Image
                               MUDA WA KUINGIA NA KUTOKA (ENTRY AND EXIT TIME). Kwa kila jambo kuna muda na majira yake.Nadhani kila mmoja wetu angalau alisha wahi kusafiri kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.Inawezakuwa ndani ya wilaya au nje ya wilaya,ndani ya mkoa au nje ya mkoa,ndani ya nchi au nje ya nchi,kama ndiyo kweli utakubaliana na mimi kuwa,kuna wakati ulianza safari yako na kuna wakati uliimaliza safari yako.Hapo ndipo kusema kunawakati wa kuanza safari na wakati wa kuimaliza safari yako.Chukulia hata katika kusoma aidha shule ya msingi,shule ya sekondari,shule ya upili,Chuo cha kati au Chuo kikuu,utagundua kuwa kuna muda watu huingia kujiunga na masomo na kuna muda watu huhitimu masomo yao. Vivyo hivyo kwa wakulima kuna muda wa kupanda na kuna muda wa kuvuna.Hii yote hutokea angalau kwa kila jambo kuwa na wakati wa kuanza na wakati wa kumaliza ndiyo maana kuna wakati ulizaliwa na kuna...

KWELI TATU KUHUSU NDOTO YAKO.

Image
  KWELI TATU KUHUSU NDOTO YAKO. Kama unakumbuka shule ya msingi kwenye somo la Kiswahili, tulijifunza kuhusu utata katika maneno pamoja na sentensi. Maneno tata ni maneno ambayo yana maana zaidi ya moja.  Hata neno ndoto lina utata, kwani lina maana zaidi ya moja. Au ngoja nikuulize kwa mfano mtu akisema ”ndoto nzuri” kwa haraharaka utamwelewaje?  Bila shaka huyu mtu anaweza akawa amelenga, aidha ndoto zile mtu anaota hasa akiwa katika usingizi au ndoto kwa maana ya maono. Ni mesema maono ili   tu unipate kwa haraka kwani maneno haya yanarandana sana kimaana. Ingawaje maneno haya yanatofautiana. Sijui umenipata sasa! Kwa ujumla ndoto ni taswira au mtazamo wa mbele   ambao mtu anatamani kuufikia (tazama picha hapo juu). Na mtazamo huu unaweza kuwa ni halisi au sio halisi, wa wazi au siyo wa wazi, kujulikana au usio julikana n.k.  Kwa ufupi ni matamanio ambayo mtu anataka kuwa/kuyafikia. Ukweli ni kwamba matamanio na shauku hii kila mtu huwa anayo, pengin...

KATA TAMAA KUKATA TAMAA (GIVE UP TO GIVE UP)!

Image
  KATA TAMAA KUKATA TAMAA (GIVE UP TO GIVE UP)! Kukata tamaa ; Ni fiki ra   zinazo mfanya mtu kukosa tumaini la kusonga mbele au   kuendelea kufanya kile alicho jipangia kufanya, ili, kutimiza malengo yake. Fikira hizi humfanya mtu afikirie kuwa, changamoto alizo nazo ni kubwa kuliko uwezo alionao wa kukabiliana nazo. Ni hulka ya kila binadamu kupitia nyakati kama hizi za kukata tamaa. Hakuna binadamu asiye pitia kipindi hichi kwa baadhi ya nyakati. Nyakati kama furaha, huzuni, kukataliwa, kujichukia, kufeli, kudhalilika, kuheshimika, kudharaurika, kuwa maarufu, kupendwa, kuchukiwa, kutaka msaada, kutoa msaada, kukosea, kusamehewa n.k. Ni sehemu ya maisha ya kila binadamu kwa baadhi ya nyakati. Nyakati kama hizi ndizo huleta radha ya maisha. Vinginevyo maisha yangekosa radha kabisa. Na watu kwa kushindwa kulitambua hili wamejikuta wakikata tamaa na kushindwa kuendelea tena kwa yale waliyo jiwekea. Zipo sababu zinazo wafanya watu wengi kukata tamaa na kushindwa kusonga...

KUWA KIELELEZO (BE A REFERENCE)!

Image
KUWA KIELELEZO (BE A REFERENCE). Tunaishi kwenye dunia ambayo kila mtu anataka   kuwa maarufu,tajiri na mtu muhimu sana katika Dunia hii.Na wengine wanajitahidi kufanya kila linalowezekana ili tu kufikia lengo hilo la kuwa maarufu   ulimwenguni,Kubwa Zaidi watu wanasahau kuwa   kuna gharama za kuufikia umaarufu na kuwa mtu muhimu duniani. Mwalimu wangu wa shule ya Msingi aliwahi kunambia ukitaka kuwa maarufu na kujulikana sehemu yeyote ile basi inakupasa ufanye kitu kizuri au kibaya sana tena ufanye kwa bidii na utofauti .Nikamuuliza kivipi? Akasema ukifanya kitu kizuri cha kujenga na kuisaidia jamii watu watakufahamu tu tena watakufahamu kwa mazuri mfano, kutengeneza labda ndege,kuelimisha jamii,kuwa kiongozi bora n.k,mchango wako katika jamii utafahamika.Lakini pia ukifanya jambo baya la aibu katika jamii mfano, kama kuiba,kujiingiza kwenye makundi ya ugaidi,umalaya n.k watu watakufahamu tu tena watakufahamu kwa mabaya hayo. Hapa ndipo nikaja kugundua kuwa kumbe h...

MAMBO 6 YANAYOPUNGUZA THAMANI YAKO.

Image
MAMBO 6 YANAYOPUNGUZA THAMANI YAKO. Hivi ulishawahi kuona aina hizi mbili za watu? 1.watu ambao wanaheshimika na kuthaminiwa sana katika jamii. Yaani, hawa watu kwenye masuala muhimu yanayo hitaji ushauri, uamuzi, na mchango wowote wenye tija ni lazima wahusishwe katika kufanya hivyo. Iwe katika vikao na matukio mengine muhimu hapo utasikia wakisema kamwiteni fulani, mwandikieni barua fulani au mpigieni simu fulani atasaidia sana katika hili. 2. Upande mwingine Kuna watu ambao huwa wanapuuzwa sana na kuonekana hawana mchango wowote katika jamii, watu hawa ni ngumu sana kukuta wemeombwa hata ushauri au kushirikishwa kwenye masuala muhimu katika jamii. Utasikia tu hamuna chochote hapo, mtapoteza hela bure tu.Watu hawa wanapuuzwa na kuchukuliwa poa sana pengine kutokana na matendo yao, manrno yao, tabia na mionekano yao katika jamii. Zipo sababu nyingi zinazofanya mtu kupuuzwa na kuonekana wa kawaida sana, hizi tutaziangalia wakati mwingine. Lakini leo nataka tuangalie mambo ya yana...

Popular posts from this blog

MAAJABU YA AKIBA

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29