Posts

KAMA UNASAHAU MARA KWA MARA, SOMA HAPA KWANZA.

Image
  KAMA UNASAHAU MARA KWA MARA, SOMA HAPA KWANZA. Boss! Siyo  kila mara, kusahau ni ishara ya Ubongo dhaifu, mara nyingi ni namna tunavyojifunza ndugu. Nimekutana na watu wengi wakisema: "Mimi sina akili kubwa." Wengine "Kumbukumbu yangu ni mbaya." Mara "Ubongo wangu hauhifadhi vitu." Lakini ukweli ni kwamba, mara nyingi tatizo si ukubwa wa akili yako wala uwezo wa ubongo wako. Tatizo ni kwamba watu wengi hawajawahi kufundishwa jinsi kumbukumbu (memory) inavyofanya kazi boss. Sikia ndugu; Ubongo wa binadamu umeumbwa kwa ustadi mkubwa. Kazi yake si kuhifadhi kila kitu unachokiona au kukisikia, bali ni kuchagua filtering taarifa muhimu na kuacha zisizo muhimu wala matumizi. Kwa hiyo, kusahau si kasoro ya ubongo ni sehemu ya kawaida ya jinsi unavyofanya kazi. Hebu tuangalie sababu kuu zinazowafanya watu kusahau mara kwa mara. 1. Kukariri Bila Kuelewa (memorising without understanding). Hili ndilo kosa kubwa zaidi ambalo wanafunzi na hata watu wazima...

SIMULIZI YA KUFURAHISHA, “KUHUSU HATIMA YA KIMUNGU”. SEHEMU YA NANE.

Image
  SIMULIZI YA KUFURAHISHA,   “KUHUSU HATIMA YA KIMUNGU”. SEHEMU YA NANE.     Ilipoishia....   Walipokumbuka hili wote walicheka. Wakati huo kumbe mama alikuwa mbele yao. Akawauliza "nyie maadui wawili mnafanya nini sasa hivi hapa nje na usiku wote huu?" Walishituka sana na wakawa wanawaza namna ya kujitetea..   Sasa inaendelea.. Kama hujasoma sehemu ya saba bonyeza hapa       "Ni kwamba tuuu!!! " Mama usituelewe vibaya tulikuwa tunaagana tu, kwahiyo nilipomkuta Elimina hapa nikaona nimuage" Elvine alieleza. " Na wewe Elimina ulikuwa unafanya nini nje saizi usiku? "      " Nilikuwa na.... "      " Alisema anajisikia vibaya kidogo kwahiyo anapunga upepo "      " We Elvine vipi mbona unamsemea kwani yeye hawezi kujieleza? "       " Kwanza nyie mmeanza lini kuongea, nyie si mnatuigizia mmenuniana? "       " Mama...

JIFUNZE KUJIFUNZA PART III.

Image
JIFUNZE KUJIFUNZA PART III. JINSI AKILI YA BINADAMU INAVYOFANYA KAZI. kusoma part II bonyeza hapa U hali gani ndugu msomaji! Mimi niko vyema na ninaendelea vizuri kabisa. Kama utakuwa unafuatilia somo hili   la jifunze kujifunza kwa makini   nadhani leo tupo part 3 ambapo tuliamua tufahamu kinaga ubaga kwa namna gani akili ya mwanadamu hufanya kazi ilikuweza kulowea ndani kabisa ya somo letu la jifunze kujifunza. Na, kama utakumbuka part 2 iliyopita tulizungumza kuhusu sehemu ya kwanza ya ubongo ambayo ni, Conscious mind (CM). Na hii, tulisema kuwa ni sehemu ya ubongo ambayo tupo na uelewa nayo . ni sehemu ya ubongo ambayo   inashughulika na matendo yote ya hiali ambayo mtu   anaweza kuyazuia au kuyaruhusu yafanyike, wakati mwingine wamombo wanasema its a logical portion of our mind , na inauwezo wa kufikri kwa mantiki(logically), kuchakata na kufanya maamuzi kupitia matukio. Mfano kujifunza kupitia makosa, kuweka malengo. Kwa ujumla tunaweza kusema mambo na ...

SIMULIZI YA KUFURAHISHA, “KUHUSU HATIMA YA KIMUNGU”. SEHEMU YA SABA.

Image
  SIMULIZI YA KUFURAHISHA,   “KUHUSU HATIMA YA KIMUNGU”. SEHEMU YA SABA.   Ilipoishia..... Kule chumbani Elimina aliamua kunywa panado na mseto(dawa za malaria) ambavyo jumla yake vilikuwa ni vidonge 47. Wakati huku sebuleni maongezi yakiwa yanaendea mama Elimina aliona aende chumbani kwa binti yake akamfariji, lakini oooh!! Hakuamini kabisa alichokiona baada ya kuingia chumbani. Kusoma sehemu ya sita bonyeza hapa   Sasa inaendelea   Mama Elimina hakuamini wala hakufikria kama binti yake an ge weza kufanya uamuzi kama ule. Yule mama alipiga kelele kama aliepatwa na kichaa baada ya kumkuta binti yake kalala chini huku akitokwa na povu mdomoni.      K elele zile ziliwashitua sana Elvine na mchungaji Moses ambao waliku w a bado katika mazungumzo s e buleni, baada ya kusikia kelele na wao wa k aamua kukimbilia kelele zilikosikika ili wakajue ni nini kilichotokea. Walipofika hawakuamini kabisa . Elvine alishituka hadi akaajikuta kaishi...

Popular posts from this blog

UKIJUA HILI KUHUSU WATU UTAFANIKIWA SANA.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.

LEVEL ZA MAFANIKIO SEHEMU YA KWANZA.