Posts

Showing posts from May, 2023

MAAJABU YA AKIBA

Image
MAAJABU YA AKIBA Akiba (saving) ni kiasi cha fedha au rasilimali ambacho kimewekwa kwa matumizi ya baadaye, hata sasa kingeweza kutumika lakini umuhimu wake kwa kutumika baadaye ni mkubwa kuliko matumizi yake ya sasa. Hata katika biblia ``Mwanzo 41:35-36`` kama umewahi soma utaona Farao baada ya kutafsiriwa ndoto yake na kufahamu kuwa, imempasa kuweka akiba alilifanya hilo kwa uharaka ili kuhakikisha linaendelea vizuri ndio akamweka Yusufu kama msimamizi wa hili. Farao aliona kabisa kuwa nidhamu yake ya kujiwekea akiba haipo sawa hivo alihitaji msaidizi wa kumsaidia kama yeye alivyokuwa ndivyo tulivyo baadhi yetu siku za leo hatuwezi kujiwekea akiba ya vile tulivyo navyo. yaani huwa tunapenda kusema kesho itajisumbukia yenyewe,  Hata hivyo tangu zamani hata leo mataifa mbalimbali yamekuwa yakijiwekea akiba kwa manufaa na matumizi ya baadaye. Ukiangalia nabii Samweli alikuwa akijiwekea akiba na aliitoa pale Sauli alipomtembelea wakaila ile akiba ya chakula. Ni muhimu kujiw...

MAMBO YA KUJIFUNZA KUTOKA KWENYE PICHA HII.

Image
  MAMBO YA KUJIFUNZA KUTOKA KWENYE PICHA HII. Tunaishi kwenye karne ya 21. Katika dunia hii kwa kweli pesa yaani, hela ni muhimu sana. Kwani, ukitaka kusafiri utahitaji pesa, ukitaka kula utahitaji pesa, ukitaka kusoma utahitaji pesa, ukitaka kutibiwa utahitaji pesa, ukitaka huduma nzuri  za viwango utahitaji pesa n.k. Watu wengine wameenda mbali sana na kusema, pesa ni kila kitu katika ulimwengu tulionao.  Kwa mkutadha huu ni shauku ya kila mtu  kuwa na pesa za kutosha angalau kutawala kila eneo. Si unajua pesa inanguvu ya kutawala eeh! Utakubaliana na hili pale utakapoona hata katika vikao vya familia mtu mwenye pesa anapewa umuhimu na kuungwa mkono kwa kila jambo hata kama anaongea utumbo, lakini kinyume kabisa, kwa wenye pointi ambao hawana pesa, utasikia ananini na yeye huyu? Full kupuuzwa. Kumbe pesa inatusaidia kujikimu, kupata mahitaji yetu ya msingi, inatoa kibali, inarahisisha mambo, ina ongeza umaarufu, inaongeza marafiki, na mengine ya kufanana na hayo. P...

HATUA 4 ZA KUSEMA HAPANA KWA HESHIMA.

Image
  HATUA 4 ZA KUSEMA HAPANA KWA HESHIMA. Asilimia kubwa ya watu duniani, wanakumbwa na changamoto ya kushindwa kusema hapana kwa ombi waliloombwa kufanya.  Hii inatokea mara nyingi wakati mwingine wanapohitajika kuwafanyia hivyo wapendwa wao, rafiki zao, majirani zao, wazazi, ndugu na jamaa wa karibu.  Pia inatokea pale unapohitajika kufanya hivyo huku huna uwezo kabisa wa kufanya au kutoa msaada huo.  Lakini kwa kuogopa kuwaumiza, kuwavunja moyo na kupoteza heshima, watu wengi hujikuta wakisema ndiyo hata sehemu walipotamani kusema hapana.  Hii husababisha mtu kuishi maisha ya watu wengine na yenye maumivu makali sana.  Kama unachangamoto hii usiogope, kwani hauko pekee yako ni watu wengi sana duniani wanapitia changamoto hii.  Lakini habari njema ni kwamba hapa nimekuandalia hatua nne za kusema hapana bila kuogopa, bila kuvunja heshima yako au kuharibu mahusiano yako na watu wengine,  Soma hadi mwisho nina imani utasaidika; HATUA YA KWANZA: ...

NJIA 5 ZA KUACHA ALAMA DUNIANI.

Image
       NJIA 5 ZA KUACHA ALAMA  DUNIANI. Kutokana na kamusi sanifu  ya kiswahili alama ni mchoro unaoonyesha ishara fulani. Yaani, kwa ufupi alama ni ishara ya kitu fulani. Lakini mimi nitaeleza alama kuwa ni utambulisho wa kitu au mtu wakati na baada ya uhai au kuwepo wake.  Kwa maana fupi ni kwamba alama ni vile ambavyo unaweza kugusa maisha ya watu wa sasa na hata baada ya kuondoka kwako duniani. Kwa mfano tukimuangalia mtu kama Stive Jobs mwanzilishi wa simu janja ya kwanza, huyu mtu pamoja na kwamba amekufa lakini bado tunatambua thamani ya kuishi kwake hapa duniani. Robin Sharma kwenye kitabu chake cha nani atalia utakapokufa, ameandika vitu vitatu vitakavyo kufanya uache alama  duniani hata baada ya uhai wako. Vitu hivi, hata wewe utakapo vifanya utakuwa na uwanja mzuri wa kuacha alama, vitu hivi ni; 1. KUANDIKA KITABU. Vitabu ni vyanzo vizuri na muhimu sana linapokuja suala zima la maarifa ambavyo hudumu karne kwa karne. Sharma ameandika ku...

CHANGAMOTO KATIKA MAISHA

Image
               CHANGAMOTO KATIKA MAISHA.  Changamoto inaweza kuwa na maana nyingi, lakini wacha tukubaliane kuwa changamoto ni ugumu au vizuizi anavyokutana navyo mtu katika kuyaendea yale aliyoyakusudia. Yaani, malengo na ndoto zako.  Wakati mwingine changamoto ni jaribu katika eneo fulani la maisha ya mtu husika.  Katika hili nimegundua kuwa changamoto haiji kwa lengo la kukuharibu, kukukomoa, kukurudisha nyuma, au kukufanya ushindwe kabisa.  Lakini, changamoto ipo kwa lengo la kukupima na kukuthibitisha kwamba umekizi vigezo vya kuwa au kuvuka katika hatua fulani ya maisha uliyopo na kwenda hatua nyingine. Wakati mwingine ugumu au changamoto ni kipimo cha kuufikia ushindi.  Ukweli ni kwamba, huwezi kuwa mshindi pasipo kushindana, kama ndivyo hivyo, sasa katika mashindano hayo utakutana na ugumu fulani ambao ndiyo changamoto zenyewe. Kadiri unavyotatua na kushinda changamoto nyingi na kubwa ndivyo unavyokuwa bingwa na ms...

SHUKURU KWA KILA JAMBO

Image
Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu......  Moja ya kitu muhimu na kinachohitajika sana angalau kwa Kila mtu ni Kushukuru.Nimekuja gundua kwamba asilimia kubwa ya waamini katika dini yeyote ile ulimwenguni, wamekuwa wanatumia muda mrefu sana kumuomba Mungu vitu ambavyo hawana, kuliko kushukuru kwa yale ametenda. Wengi wamekuwa wakilaumu na kulalama kwa vitu wanavyo tamani kuwanavyo lakini hawajavipata bado. Ndugu msomaji kunakitu natamani ukijue kwamba "kushukuru ni kuomba tena". Kumbe unaposhukuru unatengeneza mazingira ya kuomba tena. Waingereza wanasema "Is a polite expression used when acknowledging a gift, service, complement, accepting or refusing an offer" Yaani, Ni usemi wa heshima unaotumiwa wakati wa kukiri zawadi, huduma, inayosaidia, kukubali au kukataa ofa. Hii maana ina maana sana. Kwani, inaonyesha kushukuru kwa kila jambo iwe ni kibaya au ni kizuri kimetokea yakupasa kushukuru.  Nakumbuka siku moja nilienda saluni nilipofika...

SABABU 7 ZA HOFU YA KUZUNGUMZA MBELE YA WATU (REASONS FOR FEAR OF PUBLIC SPEAKING).

Image
  SABABU ZA HOFU YA KUZUNGUMZA MBELE YA WATU (REASONS FOR FEAR    OF PUBLIC SPEAKING). Nakumbuka nilipokuwa sekondari kidato cha kwanza, mara nyingi nilipokuwa nikipangwa kuzungumza hotuba ya asubuhi ( Morning speech ). Nilikuwa nahisi kuchanganyikiwa, kuugua, kukosa utulivu, kutokwenda shule   na wakati mwingine nilikuwa nawaza hadi kuacha shule. Yaani, nilikuwa na hofu isiyokuwa ya kawaida lilipokuja suala la kujieleza na kuzunguza mbele ya kadamnasi. Lakini Namshukuru Mungu kwakuwa alinikutanisha na waalimu pamoja na watu sahihi wakanisaidia nikawa nafanya vyema katika eneo hilo. Katika mizunguko yangu hadi sasa nimekuja kugundua kuwa siyo mimi tu niliyekuwa na tatizo hilo, kumbe ni watu wengi sana wakubwa kwa wadogo, waume kwa wake   tena karibia watu wote duniani. Kwani hata tafiti zinaonyesha kuwa asilimia(75%) ya watu duniani wanasumbuliwa na hofu hii . Hofu hii ni moja ya hofu zinazo ogopeka na kutesa watu wengi sana duniani. Hapo ndipo utakuja kusha...

JAMBO HILI HALITAKUACHA SALAMA.

Image
  KITU HILI HAKITAKUACHA SALAMA. Mtu mmoja alikuwa analalamika sana huku akidai kuwa, amejifunza vitu sana ikiwemo kulima, kushona nguo, amesoma sana kompyuta, kufanya biashara, kama ni vitabu amesoma sana. Kimsingi alidai kuwa anajua karibia kila kitu. Lakini alichokuwa analaumu kwamba haoni badiliko lolote kabisa katika maisha yake, licha  ya kujifunza vitu na maarifa kama yote. Nilipo muuliza, kwenye kompyuta anajua kitu gani? Akasema anafahamu kompyuta yote na amejifunza miaka miwili iliyopita na notisi aliandika zote sema hakumbuki daftali alipoliweka, lakini akituliza akili atalipata mara moja. Nikamuuliza nikileta kompyuta hapa unipangie kazi yangu utaweza? Akasema, hivyo vyote nilisha visoma na niliviandika tena vipo kwenye lile daftali, sema kompyuta mi sijawahi kutumia lakini nikiangalia kwenye lile daftali naweza afu mbona ni simpo tu.  Nikagundua kuwa mtu huyo alikuwa ametumia muda mwingi na gharama kubwa sana katika kujifunza vitu vingi sana. Alikuwa a...

KWANINI HUWEZI KUPENDWA AU KUCHUKIWA NA KILA MTU?

Image
  KWANINI HUWEZI KUPENDWA AU KUCHUKIWA NA KILA MTU? Ni hulka ya kila binadamu kutaka kupendwa na watu wote popote anapokuwa.  Ndiyo maana utakuta watu wanafanya kila namna ili tu kuwafurahisha watu wote popote waendako.  Na kama mtu atakosa upendo huu kutoka kwa watu walio mzunguka, na utashangaa atakuwa na msongo wa mawazo (stress), hasira kupita kiasi, wivu kupita kiasi, kujichukia, kuwa mnyonge sana, kujidharau mwenyewe na mengine yanayofanana na hayo. Watu wengi kwa kutaka kuwafurahisha watu wote na kulenga kupendwa na kila mtu kwa 100%, wamejikuta kwenye gubiko kubwa la kudharaulika na kuchukiwa zaidi. Rafiki yangu mmoja alisikika akisema “kama ukitaka kuwafurahisha wote basi jiandae kuwaudhi wote ”. Soma tena uelewe tafadhli .  Sasa zipo sababu zinazosababisha watu wengine wasikupende hata kama utafanya mengi ya kuwafurahisha said.  Hapa ndipo tunaenda kujibu swali letu la kwanini huwezi kupendwa au kuchukiwa na watu wote kwa 100%.  Na baa da ya...

Popular posts from this blog

NJIA 7 ZA KUOSHA UBONGO WAKO.

VITU 9 MUHIMU KWA MTU YEYOTE KUJIFUNZA KWENYE MAHAFALI.

SIRI ILIYOPO NYUMA YA TABASAMU.